KIAPO CHA MASIKINI (98) MWISHO

SEHEMU YA 98

ILIPOISHIA SEHEMU YA TISINI NA SABA: Huku kanisani nako, mambo yalikuwa yana endelea, na baada ya kutangaza tangazo la mwisho la pinga mizi, na kuona kimya, kwamba akuna mtu alie toa pingamizi, Padre akawageukia maharusi, kwaajili ya kuendelea na kipengele kinacho fwata. Lakini kabla ajasema chochote, ghafla ukasikika ukulele toka kwenye mlango wa kuingilia ndani ya kanisa, “pingamizi!! Jamani pingamizi!!! naomba msaidie” ilikuwa ni sauti kali yakike…….…..Endelea…

watu wote waigeuka kutazama kwenye ule mlango ulikotokea sauti ile, na hapo waliweza kumwona mtu ambae kila mmoja alisisimkwa na mwili kwa mwonekano wake, maana alikuwa amefungwa POP, kwenye mkono wa kulia na mguu wakushoto, pia bandage nyingine ilifungwa kichwani kwakuzunguka kichwa chote, akitembea kwa kujikongoja akisaidiwa na gongo flani la mti, lililoonekana wazi kuwa alikuwa ameliokota sehemu, niwazi mwanamke huyu, alikuwa amepatwa na hajari au kipigo toka kwa kundi la watu wabaya.

Kila mmoja alishtuka, watu walibakia midomo wazi, kwa mshangao, camera zote zilimgeukia mwanamke huyo, ambae mwonekano wake, ulimshangaza kila mmoja mle ndani, na kuanza kuzuka minong’ono ya chini chini, “jamani nini hiki” “nani huyu jamani” watu wailizana kwa mshangao, wengi wao walikuwa awajuwi habari za maisha ya nyuma ya Peter na Sada.

Siyo mwingine huyu ni Sada Nyoni, ambae hapa alionekana peke yake, akijikongoja na ile fimbo yake, kanisa lote kimya macho kwa mwanamke huyu mwenye mwonekano wa kushangaza, siyo tu kwa waumini wasio mfahamu, ata wale wazazi wa Peter na wazazi wake yeye Sada, yani mzee Nyoni na mke wake, walishangaa sana kwa ujio na mwonekano wa binti yao, ambae alikuwa anaendelea kujikongoja taratibu kuelekea mbele ya kanisa, “jamani naomba nafasi ya kueleza pinga mizi langu” alisema Sada, ambae sasa alibakiza hatua chache kufika madhabahuni.

Naam wakati huo huo Polisi watatu, wakiume wawili na wakike mmoja, ambae ndie alieonekana kuwa mkubwa wao, nazani tuna mfahamu, huyu ni SP Shanie, niwazi walikuwa wanataka kumkamata Sada, na kumrudisha hospital, lakini ghafla aliwaonyesha ishala askari wake kwamba watulie kidogo, kuona kile Sada alichokuwa anataka kukifanya, pale kanisani, ambae sasa alishafika mbele kabisa ya kanisa, “luksa imetolewa, unaweza kujitamburisha na na kutueleza pinga mizi lako” alisema Padre, akitumia kipaza sauti, na sauti ikasika vizuri sana, ndani na nje ya kanisa.

Hapo mmoja wa watumishi wa pembeni wa Padre, alisogeza kipanza sauti mdomoni kwa Sada, kwanza Sada akamtazama Peter alie kuwa anamtazama kwa machi tulivu, na uso wa tabasamu, Sada akamtazama Careen, ambae pia alikuwa anamtazama kwa uso tulivu wenye tabasamu, Sada akatazama kule walikokaa waumini, “mimi naitwa Sada Nyoni, ni mke halali wa Peter Jacob, nimezaa nae mtoto moja, aliniacha kijijini na kuja kuishi na mwanamke mwingine, nimekuja huku mjini kumtafuta, nilipokutana nae amenipiga sana, na kunitelekeza hospital bila huduma yoyote” alisema Sada, akimaliza kwa kilio cha kwikwi, na kuwafanya watu watoa mguno wa udhuni, sambamba na minong’ono ya kumlahumu Peter.

Sada akuishia hapo “mimi sina cha ziada ninacho itaji, mume wangu nime msamehe, lakini naomba ndoa isifungwe, na mimi nipewe mume wangu tuondoke nae” alisema Sada huku akiendelea kujiliza kile kilio ambacho, ingekuwa vigumu, kwa mtu yoyote kugundua kuwa kilikuwa ni kilio cha uongo, walioweza kugundua ilo ni wakina mzee Jacob, mzee Nyoni na wake zao, Peter na Careen, pia Kadara ambae alikuwa amejibanza nje kwenye mlango ambako sasa palikuwa na watu wengi waliosogea kushuhudia kinachoendelea, wengine ni polisi wale watatu, ambao walikuwa wanafahamu kila kitu kuhusu Sada.

Naam hapo Padre akamtazama bibi harusi, ambae muda wote, alikuwa ametulia, huku anamtazama yule mwanamke, kama vile alikuwa anamfahamu, na wala onyesha wasi wasi wowote, Padre akamtazama bwana harusi, ambae kiukweli ilimuwia vigumu, kutambua alikuwa katika hali gani, maana wakati macho yake yalikuwa yana mtazama yuke mwana mke huku tabasamu likishamili usoni mwake, pia macho yake hayo hayo yalikuwa yana tililisha machozi, huku maneno ya kimtoka kinywani mwake, “kweli nimeamini KIAPO CHA FUKARA hakina nguvu” alinong’ona bwana Harusi, kwa sauti ya chini kabisa, huku akimtazama mwanamke huyu alie chakaa akizidi kusogea madhabauni.


naam hapo Padre akamtazama bibi harusi, ambae muda wote, alikuwa ametulia, huku anamtazama yule mwanamke, kama vile alikuwa anamfahamu, na wala hakuwa na wasi wasi nae, Padre akamtazama bwana harusi, ambae kiukweli ilimuwia vigumu, kutambua alikuwa katika hali gani, maana wakati macho yake yalikuwa yana mtazama yule mwana mke huku tabasamu likishamili usoni mwake, pia macho yake hayo hayo yalikuwa yana tililisha machozi.

Kanisa lilizizima kwa mshangao na taharuki, kwa kile walicho kiona, ambacho nikitu adimu sana kutokea, yani kuwekewa pingamizi katika ufungaji wa ndoa, waliomfahamu bwana harusi yani Peter Jacob, walishangaa sana, kusikia kuwa alitelekeza mke na kujakuowa mwanamke mwingine, minong’ono ilitawara ndani ya kanisa, watu wakiulizana kulikoni, aikujarisha kama mtu unae mwuliza unamfahamu au mme kutana na nae mle mle ndani ya kanisa, lakini hakuna alie onekana kuwa jibu sahihi, la kwanini bwana harusi alimkimbia mwanamke huyu, ambae anaonekana kuwa katika wakati mgumu sana, na kwenda kufunga ndoa na mwanamke huyu mrembo mwenye sifa za kuitwa mzuri, ambae sasa alikuwa simama nae madhabauni, ambae pia alionekana kumtazama mwanamke mlalamikaji, bila wasi wasi wowote wala dalili ya mshangao, ilo pia lili washangaza watu waliokuwepo mle kanisani, maana walitegemea kuona pengine akiangua kilio au kuanguka na kuzimia kabisa.

Naam hapo Padre akashika kipaza sauti na kukisogeza mdomoni kwake, “tumepata pinga mizi, hvyo atuwezi kuendelea nah ii harusi, lakini pia ilipinga mizi aliwezi kuwa sababu ya kuvunjia kwa ndoa hii, mpaka pande zote mbili zitakapo thibitisha, ukweli wa ndoa ya kwanza ya bwana harusi” alisema Padre, kwa sauti iliyosikika wazi kabisa, “naomba sasa bwana harusi atuthibitishie ili, kwamba anamfahamu huyu mwanamke hapa mbele yetu, na atueleze kama ni kweli, alicho kiongea” alisema Padre na hapo akamkabidhi, Peter kipaza sauti, kwanza Peter alitabasamu, ni tabasamu lililo jaa uchungu, “hakika nime amini, KIAPO CHA FUKARA AKINA NGUVU, namaanisha kuwa fukara awezi kutunza kiapo” alisema Peter kwa sauti tulivu, ambayo ilipenye masikioni mwa watu na kuwaacha na maswali mengi sana, lakini Peter akuweza kuwaacha na maswali yao, maana alie leza kila kitu kama kiliyo tokea, mpaka viapo alivyo kula Sada, ambae aambae muda wote alikuwa anajiliza kilio cha uongo, huku akisisitiza kuwa Peter anasema uongo, wakati mwingine akimtazama Peter, na kumkonyeza, kwamba aache kile anacho kisema, “acha Peter tutaenda kuongea nyumbani, nimeamua kurudiana na wewe” alinongona Sada, huku Careen pia akisikia, na kuchekea tumboni, huku Peter akiendelea kusimulia, na kueleza kila alichoongea Sada, wakati wanawakataa yeye na mtoto wao Michael, “nandipo nilipoona kuwa Sada asingeweza tena kuwa na mimi hivyo nilikutana na bi Careen na kuanza maisha mapya” alisema Peter akimaliza kuelezea, huku Sada akiendelea kulia, wazazi wa Careen awakuonekana kushtuka kwa lolote, maana tayari walisha wai kusimuliwa mkasa wa maisha wa Peter ya hapo mwanzo.

Sasa watu wote mle ndani , walibakia midomo wazi kwa mshangao wasijuwe wa mwamini nani, “je kuna yoyote anaweza kuthibitisha ilo, iwe mzazi au rafiki ndugu au jamaa, pia cheti cha ndoa ya mwanzo” aliuliza Padre huku wakiwatazama wausika kwa zamu, pamoja na waumini, Sada akatazama chini, maana alifahamu kuwa, akukuwa na ndoa iliyofungwa hapo mwanzo, kimya kilitawara kusubiri jibu toka kwa mmoja kati ya upende wa Sada au Peter.

Ukweli kulikuwa na wakati mgumu sana, kwa upande wa Peter, maana upande wa Sada yeye akuwa na mtu wa kuthibitisha upuuzi wake, lakini Peter, angeweza kuwa tumia wazazi wake yani mzee Jaco na mama yake, swali lililokuja na kwamba, je ataaminika, au ataonekana kuwa niupendeleo wa wazazi wake.

Lakini wakati hali hiyo inaendelea mala ghafla ikasikika sauti toka upande wa waumini, “mimi nitathibitisha ilo” watu wote waka tazama upande ule ilikotokea sauti, ni karibu kabisa na alipokaa mzee Jacob na mke wake, nisehemu waliyokaa wawakirishi toka Mwanamonga.

Na huyu alikuwa ni mzee Nyoni, aliekuwa amesimama, ukweli Sada au mama Michael alikuwa ameshikwa na mshangao mkubwa sana, kwa kumwona mzee Nyoni ambae mwanzo akuwa amemwona, ni kutojana na jinsi alivyo vaa na kupendeza,

Wakati Sada anaendeea kumshangaa baba yake, na wakati huo huo ikasikika sauti ya pili, hii ilikuwa ni yakike, “na mimi pia ninathibitisha” huyo alikuwa mama Sada, ambae alisema hivyo huku anasimama toka kwenye kiti alicho kalia, karibu kabisa na mume wake yani mze Nyoni, “na mama nae yupo?” Sada alishangaa kwa sauti, huku sura ikimshuka, kwa kukumbuka kile alicho wafanyia wazazi wake mala ya mwisho, hakika akujuwa kuwa mshangao mkuwa zaidi unafwatia.

Maana wakati akiwa ana toa macho kwa mshangao, mala ikasikika sauti nyingine ya kike, toka upande wa lango la kuingilia, “Queen, na mimi nipo hapa nitathibitisha kila kitu, kabla ya kukurudisha hospital kuchukuwa luksa yako, maana umeonyesha umesha pona, baada ya kutoroka hospital, kisha utaamia mahabusu ya jeshi la polisi, kabla ya kufikishwa mahakamani, kwa makosa mawili, moja udanganyifu, kwa jeshi la polisi, ukimchafua bwana Peter, ambae aulimwibia mala mbili na kumtelekeza hotelini akiwa na mtoto mdogo, pili kushi na kutunza siri za jambazi Emmanuel Msengi, ambae nae tayari yupo chini ya jeshi la polisi, na kesi yake inaendelea kusikilizwa” huyu alikuwa ni SP Shanie Mohamed, ambae maneno yake kwakifupi yalizidi kufungua masikio ya watu wote mle ndani.

Naam Padre aliluhusu mashuhuda kutoa ushuhuda wao, juu ya ndoa ya awali ya Peter na Sada, wakwanza alikuwa ni mzee Nyoni, ambae maelezo yake yalifanana na maelezo ya shuhuda wapili yani mke wake, “Sada ni binti yetu wakwanza na wamwisho, akuwai kuolewa hapo mwanzo, ila aliwai kuishi na bwana Peter, ni baada ya kupata ujauzito” alieleza mzee Nyoni, ambae bila kupepesa, alielezea kila kitu, kuanzia wizi wa fedha na kumtoroka mume wake, uongo aliowadanganya, juu ya maisha anayo ishi mjini, na kitendo cha wakukataa mbele zawatu, na wao kusaidiwa na Peter.

SP Shanie, yeye alieleza jinsi Sada alivyo okotwa akiwa amepoteza fahamu, kufwatia kipigo alicho kipata toka toka kwa bwana wake Emma, ikiwa ni matokeo ya fumanizi, Shanie akaelezea uongo wa Sada, kuwa ni mke wa Peter alie mtelekeza kijijini, na yeye Shanie kufanya uchunguzi na kubaini uongo wa schana huyo tapeli.

Mpaka hapo Sada alijihisi miguu inakosa nguvu, akaanza kulia kwa sauti akiomba msamaha kwa wazazi wake, kwamba wamsamehe, kwakile alicho wafanyia, yani kuwa kataa kwamba siyo wazazi wake, pia akaomba msamaha kwa Shanie, lakini aikusaidia, maana aliagiza polisi wale wambebe juu juu, na kumwingiza kwenye gari, kisha wakampeleka hospital kisha kituo cha polisi.

Ndoa ilifungwa na ratiba zote zikafwata, sherehe za harusi zilidumu kwa week moja zaidi, watu wakila na kunywa masaa 24, huku wanandoa hawa, wakisafiri kwenda #mbogo_land kwa king Elvis wa kwanza, ambae aliwapokea na kuwafanyia sherehe kubwa sana, pamoja na kuwapatia zawadi nyingi sana, ikiwa pamoja na jumba kubwa sana, mtaa wa King Eric, uliopo pembezoni mwa Trech Town City, kuwaongezea fedha kwaajili ya mradi wao mpya wa kilimo na vyakula.

Naam kesi ya wakina Kalonga ilifikia mwisho, wote walifungwa miaka sitini jela, yani kuanzia kalonga na vijana wake, pamoja na OCD Mwanauta na askari wake, Sada aifungwa miezi sita kwa udanganyifu, huku kiepuka kosa la kutunza siri, baada ya ushaidi kukosekana, hivi sasa yupo mwanamonga kwa wazazi wake, ambao walimsamehe, kutokana na ushauri wa watu mbali mbali, akiwepo Peter na Careen, mguu mmoja ume shindwa kuunga vizuri, na sasa anatembelea gongo, Michael ameshindwa kumtambiua Sada kama mama yake, zaidi kila anapo mwona, umwita kama mwizi wa viatu vyake, atuwezi kujuwa hapo baadae pengine akisahau na kumtambua kama mama yake. yani Sada, ambae kiukweli alijilahumu sana, kwa kukimbilia starehe, za muda mfupi zilizo mkalisha chini, kwa muda mrefu, huku wakati yeye anakaa chini mwenzie Peter ndio anasimama, na kuanza kula starehe.

Hakika Sada akuisha kutoka machozi kila siku, asa pale anapo iona nyumba kubwa sana ya kisasa, ambayo ilijengwa pale pale ilipokuwa ile yumba ndogo, ambayo sada aimfungia mtoto na kutorokea mjini, Sada aliumia zaidi alipo yaona magari makubwa yenye maandishi makubwa ubavuni, PeterCaren Co ltd, yanayoenda kwenye kiwanda cha Peter, iwe kuleta au kuchukuwa bidhaa, zinazozalishwa kiwandani pale, kiwanda ambacho kilizalisha ajira nyingi kewa vijana wa mwanamonga, ambao sasa licha kufanya kilimo, lakini pia, walifanya kazi kwenye kiwanda kile cha kijana mwenzao wa pale kijijini, yani bwana Peter Jacob, ambae ukiachilia kuendesha gari zuri, kuingiza fedha nyingi, ambazo wakati mwingine alisaidia kijiji chake kwa kujenga zahanati, na kiboresha shule ya msingi na kuahidi kujenga sekondali, pia alizidi kupenda na mke wake, ambae alikuwa bega kwa bega na mume wake huyu, kuhakikisha biashara zao zina fanikiwa, na sasa alikuwa na ujauzito mkubwa tu, ambao muda wowote, ange shusha engine, na kuanza kulea.

MWISHO

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!