SEHEMU YA 01
Sadiki Ndaru ni kijana mcheshi sana, alikuwa na ndoto za kuwa daktari lakini kidogo maisha ya chuo yalimbadilikia na kufeli akarudi nyumbani.
Mwezi wa 12 mwaka 2021 Sadiki akiwa kwao Singida, alipata kupigiwa simu na kaka yake aitwaye Mandi ambaye anaishi jijini Tanga, ni mvuvi wa samaki
“Diki” kaka alimuita kwa kufupisha lile jina la Sadiki
“Kaka shikamoo”
“Marahaba, vipi hivi una mishe gani hapo Singida?” Kaka alimuuliza
“Kaka maisha yamekuwa magumu sina mishe yoyote”
“Sasa sikiliza, kuna kampuni moja inahitaji watu wenye elimu kuanzia ya kidato cha sita kama vipi njoo ufanye maombi unaweza ukapata kuliko kukaa na bi mkubwa hapo nyumbani”
“Poa, nije lini?”
“Ngoja nikutumie nauli”
“Nauli ninayo wewe niambie tu nije lini”
“Leo ni jumanne, njoo alhamisi au ijumaa nafikiri nitakuwa nyumbani”
“Poa kaka ngoja nijiandae”
“Poa”
Sadiki alimueleza mamaye suala hiyo na mama aliweza kufurahi sana, alimpa baraka zote na hata siku ya ijumaa ilipowadia Sadiki alipanda gari na kuelekea mkoani Tanga.
Alipofika tanga tu hivi alipokelewa na kaka, na alimpeleka katika nyumba aliyokuwa akiishi, ni nyumba ambayo ilikuwa haina hata umeme, wala maji, ila walipapenda maana walikaa bure bila kulipia kodi
Mandi alikuwa akiishi na mkewe Husna, alikuwa mwanamke mzuri sana japo walikuwa hawana ndoa halali ila walikaa pamoja zaidi ya miaka mitatu. Husna alikuwa ni mtoto wa kidogo lakini hakubahatika kupata mtoto kipindi chote hicho cha maisha.
“Shem karibu, hapa ndo tunakaa kwa tabu tabu tu hivi” alisema Husna
“Pazuri, nafikiri panavutia sana” Sadiki alipasifia sana pale kwa kaka yake lakini alipasifu tu bure, kulikuwa hamna kitu.
Aliandaliwa sehemu ya kulala kwenye godoro chini na hata ilipofika asubuhi ndipo mambo yakawa sawia.
Asubuhi asubuhi Mandi aliondoka akaelekea katika harakati fulani, hivyo akamuacha sadiki akiwa anachota maji pamoja na shemeji Husna.
“Shem umedondosha hela” Sadiki alisema huku akiwa anatembea nyuma ya shemeji yake
Husna aligeuka nyuma na kutazama nyuma
“Wapi, hela ipi mbona mi sina hela?” Alisema Husna
“Hahaha…..sasa shem kama hauna hela unageuka nini?” Aliuliza Sadiki
Husna alitabasam “Halafu wewe” alisema huku akimnyooshea kidole “Mimi huwa sipendi utani” alisema shemeji Husna
“Haya samahani” alisema sadiki na safari kuelekea kisimani iliendelea
Walichota maji kama madumu 12 kwa pamoja, ndipo Sadiki akaona shemeji yake amechoka sana akampa likizo
“Shemeji pumzika, kwani yamebaki madumu mangapi?” aliuliza Sadiki
“Madumu 4 na ndoo kubwa 8” Alisema
“Wewe pumzika hizo nitazoa mimi”
“Jamani Shem pumzika usijichoshe sana” Husna alisema huku akiketi mkekani
“Wala usijali, mimi kule kwetu nazoa maji mabondeni huko, yaani huku hamna hata kilima? Ngoja nikuonyeshe” Sadiki alisema na kuondoka chapu
Haikuchukua dakika nyingi sana, Sadiki aliifanya kazi yake na kuyaweka ndani vizuri
“Wooow, sijawahi kuchota ndoo zote humu ndani, hapa nitapumzika muda sana bila kuchota maji”
“Haha,” Diki alisema na kuketi
“Pole, najua umechoka shem ngoja nikupikie chai” alisema
“Sawa”
Sadiki alichukua simu yake, alikuwa amekuja na smartphone aina ya tecno, alianza kuangalia vichekesho facebook vya Nigeria, alikuwa anapenda sana
Mara Shem Husna aliacha chai ikiendelea kuchemka jikoni halafu akaondoka kwenda kununua mihogo
“Shem, vipi simu huwa mnachajia wapi?” aliuliza
“Oh, tunachajia kwa mpemba hapo mbele dukani”
“Shi ngapi?” aliuliza
“300” alijibu
“Daa, simu yangu ina asilimia 12, naomba uniendee nayo uweke chaji basi”
Husna alirudi na kuichukua simu ya Sadiki kisha akaondoka nayo, ilikuwa haijajifunga kwa ufunguo bado, hivyo ilimpa fursa Husna kuangalia baadhi ya vitu
Husna alipopita facebook kule kwenye vile video alivyokuwa aliviangalia mtaalam, aliona kijana mmoja aitaye Lord Lamba akiwa anamnyonya ulimi mwanamke kwenye video.
Aliitazama sana, na hata akajikuta ananuna ghafla. Husna alipopita pia kwenye gallery ya Sadiki alikuta baadhi ya video ambazo kijana alijirekodi akiwa anampiga mate mpenzi wake huko singida.
Husna alikata zile video na kisha kuizima simu halafu akaipeleka kwa mpemba maana masharti ya mpemba ukitaka kupeleka simu kwake lazima uizime kwanza ili isimsumbue
Baada ya kuiacha, aliondoka na kwenda kununua mihogo akarudi nayo nyumbani, alimkuta Sadiki ameshaepua ile chai na kuiweka kwenye chupa yaani alikuwa kama vile mwenyeji kabisa
“Shem umerudi?”
“Nimerudi shemeji” alijibu Husna alikuwa hana furaha, aliketi kwenye mkeka na kuwaza
Sadiki alipomtazama alijua kabisa shemeji yake hana furaha, aliamua kumsaidia majukumu, alichukua sahani safi na kuitia ile mihogo, halafu akachukua pia vikombe na kumimina chai
“Tunamuachia broo?” Sadiki aliuliza
“Hapana huwa hanywi chai kaka yako”
“Haya sisi tuendelee”
Walianza kunywa chai taratibu ila Husna bado hakuwa na furaha, Sadiki alimsoma vyema na kisha akamuita
“shemeji” alisema Sadiki
“Abee”
“Najua hauna furaha, na najua sababu ni nini”
“Sababu ni nini?” aliuliza Husna
Sadiki alitabasamu na kutia muhogo kinywani “Najua sababu ni kwa sababu bado haujabarikiwa mtoto” Alisema Diki
“Ni kweli shemu, lakini sio hilo tu, kuna mengi sana shem wangu” alisema binti
“Mengi ni yapi? Au kaka anaku-cheat?” aliuliza
“Hapana, ila ni mwanaume wa ajabu sana, sio mcheshi kama wewe tena ninashangaa, kwanza nilijua labda watu wa Singida wote mpo hivi kumbe hapana wewe mchangamfu”
“Kivipi shem”
“Hivi shem unajua tangu nioane na kaka yako, hajawahi hata kunipiga busu?” aliuliza
“Acha masihara, kwanini?” aliuliza Diki
“Simuelewi, hata nikimsogezea mdomo ninajaribu kumbusu mdomoni huwa anaukwepesha mbali, yeye anachojua kuitumbukiza tu, sasa ndo mapenzi gani?”
“Pole sana Shem, ni kawaida sisi kwetu hivyo ni vitu vigumu sana”
“Kivipi? Mbona nimeona kwenye simu yako wewe unafanya wonders?” alimuuliza ndipo Diki akashtuka
“Haaah, umeona nini?”
“Mh hujui kile ulichojirekodi wewe na msichana mnafanya nini?” aliuliza
“Anyway, ni kweli ila mimi hii mitandao imenifundisha mengi, lakini yeye bro na mitandao wapi na wapi? Halafu pia chuoni nilijifunza mengi sana”
“Shem, hakuna kitu nilikuwa napenda kama ulimi kipindi nipo sijaishi na mwanaume, nilikuwa tayari nisifanye chochote na mwanaume ila tu akishaninyonya ulimi tu naridhika”
“Hahaaa…..shem bwana story gani hizi? Wewe ni mke wa kaka yangu tuongee mambo mengine bwana”
“Oh I’m sorry nimejisahau Shem, tunywe chai nikaoshe vyombo”
“Sawa, usinune sasa tabasamu maana ukinuna unakuwa m-bayaaaa ila ukitabasam unakuwa na kasura kama kamtoto, bor anajua sana kuchagua” alisema maneno mazito yaliyomsababisha Husna afurahi na kutabasamu kwa furaha huku akimtazama kwa aibu
“Halafu wewe, shem wewe” Alisema Husna, ghafla alipaliwa na muhogo na kuanza kukohoa
“Mh. Umbea mbaya ona hadi unapaliwa shem”
“Hahaha, niache bhana story zako ndo zinanifanya ninapaliwa mimi” alisema Husna na kumpiga kofi shemeji yake kakofi kadogo tu “Mi sipendi shem ujue”
“Hahahaa….” walicheka sana maana Sadiki alikuwa mcheshi sana…..USIKOSE SEHEMU YA PILI
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU