SHEM MI NATAKA (02)

SEHEMU YA 02

Tunaendelea tulipoishia
Kutokana na Husna kuwa hana kazi yoyote inayomuweka bize sana, aliitumia siku ile kupiga story na Sadiki, zilikuwa Hadithi tofauti tofauti za kuhusiana na maisha ya huko Singida maana hakuwahi kufika kabisa wala hakutambulika kisheria kama mke japo nyumbani walitambua kwamba kuna mtu anaishi na mtoto wao

“Shem nimekaa na wewe siku moja tu nimeamini kwamba kumbe hata watoto wakiwa wa familia moja huwa hawafanani kitabia”

“Kwanini unasema hivyo shemeji?” Aliuliza Sadiki

“Kwa sababu unafurahisha sana kila story yako inapoisha inaanza nyingine tamu zaidi, nashindwa kufanya kazi zangu halafu umenifanya nikasahau kwenda kwa mashoga zangu kupiga umbea”

“Shem unaweza kwenda tafadhali wala usiwaze”

Husna alichukua kiswaswadu chake na kuangalia majira
“Khee shemeji ni saa 9 halafu sijapika cha mchana”

“Saa tisa wewe ulijua mapema?” aliuliza Sadiki huku akitabasamu

Husna aliinuka haraka na kuanza kuhangaika kuandalia chakula cha mchana alitia mkaa jikoni na kuuwazha, kwa kawaida alijua mumewe atarudi kwenye saa kumi na lazima akute chakula.

Alichacharika haraka na kwenda gengeni kutafuta angalau dagaa mchele na viungo vingine kisha akapitia kwa mpemba ambapo alichukua simu ya Sadiki akalipia 300 na kuondoka nayo.

Alipofika nyumbani alimpatia simu ilikuwa imeshajaa chaji tayari

“Oh asante shemeji, shika hii” alisema Sadiki huku akimnyooshea noti ya shilingi 1000 moja

“Ya nini shem?” aliuliza mtoto wa kike

“Ya chaji”

“Ah nimeshalipia wala usijali”

“Shika bwana”

“Hapana shem” Husna aliongea kisha akaenda moja kwa moja na kuangalia mkaa wake kama umeshakuwa tayari kwa ajili ya kupikia.

Haraka haraka Husna alichukua sufuria ya ugali akatia maji halafu akaweka jikoni na kusubiri yapate moto ndo atie unga.

Wakati anasubiri vile ilibidi achukue nyanya, pilipili na vitunguu akaviosha kwa ajili ya kutengeneza kachumbari maana dagaa mchele huwa hawapikwi baada ya kukaangwa tu na muuzaji, mtumiaji hununua na kutafunia chakula

Husna alianza kukata kachumbari ila ghafla simu yake iliita na alienda kuipokelea mbali kabisa bila Sadiki kuelewa kwanini aende mbali naye.

Sadiki muda huo alikuwa anachezea simu yake, anasoma soma message, baada ya kuchezea kwa muda alipigiwa simu na mpenzi wake wa Singida akapokea na kuanza kuzungumza naye

“Dikiii” Yule mpenzi wake aliongea kwa sauti ya kudeka huku akibana pua

“Nambie Bite, unaendeleaje?” Sadiki aliuliza

“Mwenzako najisikia vibaya mwili unachoka sijui naumwa na nini” alisema binti

“Pole sana, tatizo nini”

“Tatizo wewe, nimekumiss jamani siku moja tu mi ntaweza kweli kuvumilia mpenzi wangu”

“Beatrice please usilalamike hivyo nikishafanya interview lazima nije, nimekumiss pia”

“Lini interview?” aliuliza binti

“Jumatatu mpenzi”

“Oh sasa mbona hata simu ulikuwa hupatikani mpenzi chakula hakishuki hata kidogoo yaani nimeenda mara kibao mpaka pale kwenu siamini kama haupo mpenzi wangu” yaani Bite alikuwa anaongea kama vile anataka kufa, muda huo huo akiwa anaongea ndipo Husna naye anawahi kuja kusonga ugali baada ya kumaliza kuongea na simu

“Simu ilizima hapa kwa kaka hamna umeme, hivyo basi nimezima nikapeleka kibandani kuchaji”

“Sawa mpenzi usinisaliti Diki nitaumia kwani tumetoka mbali halafu kumbuka ahadi zetu nyingi”

“Wala usiwe na wasiwasi, nakupenda pia mpenzi”

“Uko bize sana Diki?” alimuuliza

“Kidooogo niko bize kwani vipi?”

“Nilitaka unipigie zile story zako tamu japo za uongo ila mume wangu unajua kunipa story tamu i miss you, tafuta muda tuongee muda mrefu please”

“Usijali sawae?”

“Okay”

Sadiki na Beatrice waliagana na simu ilikatwa, alipomaliza hivi Sadiki alitabasamu alijua msichana wake anamfia vibaya sana

“Yaani huyu bana” alisema Diki na kuweka simu mkekani, Husna alimgeukia huku akisonga ugali

“Ndio mke mwenzangu?” aliuliza Husna

“Yes, ananipenda sana”

“Shem hawezi acha kukupenda”

“Kwanini unasema hivyo shem?” aliuliza Sadiki

“You are very charming, very interesting” alimsifia huku akimuambia kwamba ni mcheshi na anavutia sana

Sadiki alitabasamu tu, hakuna mtu asiyependa kusifiwa, alisogea na kukamata vile viungo vya kachumbari halafu akaendelea kuvikata kata
“Hapa si ulikuwa unatengeneza kachumbari?” aliuliza

“Ndio”

“Ok ngoja nikate” alisema Sadiki na kuendelea kukata

Baada ya ugali kuiva ndipo Husna akampigia simu Mumewe, Mandi akawa amemuuliza alipo ili wamsubiri katika kuja kula chakula kwa pamoja

“Niko mbali kidogo mpenzi, nitakuja baadaye ila nyie endeleeni tu”

“Sawa mume wangu” Husna alijibu

Basi alitenga ugali na dagaa kidogo kidogo pamoja na kachumbari halafu wakaanza kula pamoja na shemeji yake. Huku wakifurahia sana ile hali ya kuwa pamoja

Kumbe muda huo Mandi alikuwa naye amepata lift ikamleta kwa haraka mpaka karibia na nyumbani, alishuka na aliwaona kwa mbaali wakiwa nje wakila pamoja, hakujali ila alisogea huku akiwatazama sana

Aliona jinsi Husna alivyokuwa akicheka wakati anakula pamoja na Sadiki. Alisogea mpaka akawakaribia, hata hivyo Husna hakujali maana walikuwa hawafanyi chochote kibaya

“Jamani mmeshindaje?” Aliuliza

“Salamaaaa” Husna alijibu

“Broo pole na majukumu mazito”

“Asante dogo” alisema na kumgeukia Husna “Yaani tangu asubuhi mnakula muda huu?”

“Yaani acha nimetafuta mboga sana” Husna alisema

“Utakuja kuniulia mdogo wangu ujue wewe” Alisema Mandi huku akimnyooshea kidole mkewe na kutoa tabasamu fulani hivi

“Hahah, usijali siwezi kumuua shemeji yangu” alisema Husna na kuinuka “Keti hapo nikupe chakula ule”

“Hahah, hayaaa naketi” Alisema na kusogea mkekani akaketi halafu akamcheki Sadiki “Hawa dagaa wapo Singida?”

“Sijawahi waona”

“Vipi umewaonaje ni wazuri au mizinguo”

“Wazuri sana yaani sijui nitanunua niweke niwe najitafunia” alisema wote wakacheka

Husna alimpatia mumewe chakula akaanza pale pale kumlisha, unajua tena watoto wa Tanga kwa mahaba mazito hawajambo……! Diki aliwatazama tu.

**
Ilipofika usiku saa moja na nusu Mandi aliondoka tena, alikuwa anaenda kuvua samaki baharini.
Sadiki na Husna walibaki wawili tu nyumbani
ITAENDELEA…..JE ITAKUWAJE? USIKOSE SEHEMU YA 03

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!