SEHEMU YA 03
Tulipoishia ndipo tunaanzia
Ilipofika usiku saa moja na nusu Mandi aliondoka tena, alikuwa anaenda kuvua samaki baharini.
Sadiki na Husna walibaki wawili tu nyumbani
Ilipofika muda wa kulala
Kama kawaida shemeji alilala chumbani ambapo ni chumba chake yeye na mume wake, na Sadiki alilala sebuleni ambapo ni godoro tu lilitandikwa chini.
Nyumba ile iliyokuwa ni kwamba hata kama mpo vyumba viwili tofauti lazima mtu wa chumbo kimoja asikie sauti unayoongea ukiwa chumba kingine, hii ilifanya story zikawa zinaendelea kati ya Husna pamoja na Sadiki
“Ahahahahaa shemeji lalaa bana mimi sitaki huo uongo wako” alisema Husna baada ya kupewa story ya kuchekesha na Sadiki
“Hahahahah” Sadiki yeye alicheka
“Hivi vituko utaacha lini?” Husna aliuliza
“Hivi unajua shem mimi sijuagi kama nina vituko ila tu nikiongea watu wanacheka”
“Una vituko sana hata sauti yako umavyoitoa ni kichekesho tosha”
“Ok nitajaribu kuwa serious” alisema
“Sawa tutaona kama utaweza” alisema Husna
“Ok kuanzia sasa nitakuwa serious”
“Sawa tuone”
Husna alinifunika vizuri na khanga, unajua hata Tanga kuna asili fulani ya joto hivyo mara nyingi kipindi cha mwezi wa 10, 11 na 12, 1 kunakuwa na joto hivyo watu huweza kulala bila hata kujifunika
Husna alikuwa ndani ya neti yuko na khanga yake moja amejifunika nayo lakini hajavaa kitu, mipaja iko imetuna mwenyewe anajisikia kama vile yuko single maana alikuwa haridhishwi na show ya Mandi
Dakika kama kumi zilikuwa zimepita tangu Sadiki aliposema kwamba atakuwa serous, muda huo alikuwa amejifunika ndani ya neti Bite anatuma message kibao anataka apigiwe lakini sasa Diki hakuwa na dakika
Husna alijilazimisha kusinzia ila bado usingizi ulikuwa hautaki kumchukua, aliwaza mengi sana, alitamani kuwa na mtoto kabisa lakini alikuwa hashiki mimba kabisa, pia mapenzi yake na Mandi yalikuwa hayanogi kivile
Mara kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake ya batani, akaichukua na kuufungua, ulikuwa ni wa shoga ake mmoja aitwaye Sharifa alikuwa amemtumia ujumbe wa kusongeza (forward) na ulikuwa hivi
“Jamaa mmoja alikufa alipofika mbinguni malaika wa zamu akamuambia kwamba muda wake wa kufa bado ulikuwa haujafika hivyo anapaswa arudi duniani ila sasa akirudi kama binadamu watu watamkimbia, aliambiwa achague kurudi duniani kama kiumbe yeyote ndipo akachagua kurudi kama kuku
Ghafla mtu yule alitokea katika banda la kuku huku akiwa kama mtetea, alishangaa sana, akiwa anashangaa aliisi kama vile kitu kinamuuma uma tumboni na hakujua ni nini, hivyo akaamua kumfuata jogoo na kumuuliza ni dalili gani ile, Jogoo akamuambia hilo ni yai hivyo asogee kwenye kiota kisha asukume na atataga. Alifanya hivyo na aliposukuma mara moja likatoka yai alisikia ‘paaa paaa’ amepigwa vibao vizito “Wewe mpumbavu unakunya kitandani” ilikuwa ni sauti ya mkewe kumbe alikuwa anaota……hahahaa usicheke peke yako watumie wengine nao wacheke”
Kiukweli huu ujumbe ulimchekesha sana sana Husna na kujikuta anamuita shemeji yake
“Diki, Dikiii sikiliza hawa wajinga wenzako” alisema Husna lakini Sadiki akakaa kimya “Shem ee” alisema “Umelala?……aaah kuna SMS inachekesha” aliongea ila Sadiki kimya.
Husna alisogeza neti kidogo na kushuka kitandani akasogea mlangoni na kumchungulia shemeji yake amelala ila hakujua kama kasinzia.
Husna alichukua simu na kummulikia Sadiki akagundua hajasinzia maana macho yalifumbwa ila yalicheza cheza
Husna alicheka sana na kuendelea kummulika mpaka pale Sadiki aliposhindwa kuvumilia akajikuta amecheka kwa nguvu
“Mh, mbona nakuita hauitiki mi nkajua umelala”
“Shem nimeamua kuwa serious” alisema
“Hahahaa wewe unaigiza ee” alisema na kuifunga kanga yake vizuri halafu akachungulia dirishani, kutazama hivi, kama vile kuna mtu anawatazama kwa dirishani, Husna alishtuka sana na kuzima tochi
“Huyo nank anatuangalia shem” alisema na kukimbilia chumbani halafu akaingia ndani ya neti na kujifunika, wasiwasi wake alihisi labda ni mumewe
“Sadiki alijaribu kutazama lakini hakumuona mtu maana yule aliyekuwa anawachungulia alikuwa ameshaondoka
Sadiki hakuamini kama kuna mtu alikuja maana alihisi shemeji alikuwa amemtania tu kisa anapenda utani……walilala ila nafsi ya Husna ilikosa amani kabisa.
Muda wa saa 11 alfajiri Mandi alirudi nyumbani akiwa na samaki wachache kwa ajili ya ugali, alioga kisha akajirusha kitandani na kuanza kuuburuza
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU