SHEM MI NATAKA (04)

SEHEMU YA 04
*
Ilipofika asubuhi kabisa, Husna aliamka na kwenda kufanya usafi wa nje kwa kufagia fagia na kupanga vitu. Alipomaliza tu alitengeneza chai.

Sadiki alishtuka usingizini, kumeshakucha akaishika simu yake na kutazama ni saa moja na dakika 39
“Kumbe kumekucha hivi” alisema kwa sauti ndogo na kujitoa kwenye neti halafu akatoka nje huku alipiga mihayo ya kutosha

Sadiki alimkuta Husna akiwa anatengeneza chai

“Shem kumekucha?” alimuuliza

“Kumekucha vipi umeamkaje?” alisema Husna huku akimtazama machoni Sadiki

“Safi” alijibu Diki na kuanza kutembea tembea nje huku akichezea simu yake kwa kujibu baadhi ya messages zilizokuwa zimetumwa kabla hajaamka hasa hasa zikitoka kwa bite

“Hodiii” Ghafla kuna binti alibisha hodi pale nyumbani ndipo sadiki akageuka na kukutana uso kwa uso na msichana mmoja mweupe sana ambaye alikuwa amebeba beseni lililojaa mboga za majani

“Aah Chiku karibu” alisema Husna

“Asante dada umeamkaje?” aliuliza

“Safi tu, leo una mboga gani?” aliuliza Husna

“Kuna Chinese, Mchicha, Matembele na Mnavu” alisema Chiku

“Mh Chinese ndo nzuri” Alisema Husna na kumgeukia Sadiki “Shem unatumiaga Chinese au mchicha?” aliuliza

“Ah, mimi chinese ndo naipenda tamu bwana”

“Mh mwanaume unapenda chinese huogopi?” aliuliza Husna huku akitabasamu

“Niogope nini? Kwamba zitaua nanilii” aliuliza huku naye akitabasamu

“hahahah” Chiku na Husna walicheka kwa pamoja

“Hii haifi hata ipigwe kwa nyundo itazidi kupiga kazi sana tu” alisema kijana huyo wakaendelea kucheka
Yaani walimaanisha kwamba mboga aina ya chainizi huwa zinauwa nguvu za kiume lakini yeye aliendelea kuzitaka

“Embu nipe Chinese fungu moja na Mchicha fungu moja” alisema Husna na kuinuka akaenda ndani kwa ajili ya kwenda kuchukua pesa

“Sawa” alisema Chiku

Baada ya dakika moja Husna alirudi akiwa na noti mbili za shilingi elfu mbili mbili, akampa noti moja Chiku halafu akapokea mboga na kuziweka pembeni juu ya mfuniko wa ndoo

Chiku alimrudishia sh 1000 kama chenji, ndipo Husna akaziweka kwa pamoja na ile noti ya elfu mbili aliyobaki nayo halafu akatia ndani ya blauzi kwenye kifua chake akazibana kwenye maziwa.

Sadiki naye alirudi ndani na kuchukua mswaki akatoka akiswaki halafu akachota maji, kaka Mandi yeye bado alikuwa akikoroma kitandani kwenye usingizi mzito sana

Chiku alipomaliza aliondoka zake kwenda kuwauzia watu wengine huko mtaani

*
Siku hiyo ilikuwa ni jumapili, na kesho yake jumatatu Sadiki alitakiwa akafanye interview katika kampuni aliyokuwa ameambiwa na kaka yake

Kwa sababu ilikuwa ni Mandi aliona angalau apumzike mchana maana alikuwa amechoka sana, walibaki nyumbani na ndugu wakawa wanapiga story tofauti tofauti.

Ilipofika muda wa mchana saa 8 Husna aliondoka na kwenda kwa mama mmoja ili akasuke nywele za 1000 yaani mistari kadhaa tu kichwani

“Broo” Sadiki alimuita kaka yake

“Nambie dogo” Mandi alijibu

“Kesho nitaweza interview kweli?”

“Kwanini usiweze? Si umesoma?”

“Sijasomea hivyo vitu ila anyway Mungu anisaidie”

Simu ya Mandi iliita na kuitoa mfukoni akapokea na kuanza kuongea huku akiinuka na kutembea kuelekea nje na pale nyumbani

Aliondoka moja kwa moja bila hata kumuaga Sadiki, kitendo kilichopelekea Sadiki kubaki mwenyewe pale nyumbani akichezea simu yake maana bado ilikuwa na chaji

Kwenye saa 10 jioni Sadiki alisimama na kupiga piga hatua njiani karibu na nyumbani, ndipo ghafla alikutana na Chiku muuza mboga mboga akiwa muda huo hakuwa na beseni la mboga ila alibeba tu simu sabuni ya unga mkononi

“Mambow” Chiku alimsalimia Sadiki

“Oh, poa kama vile nilihisi nishakuona vipi mbona hujabeba mboga?” Sadiki aliuliza

“Hapana jamani nimeshamaliza kuziuza mpaka kesho asubuhi tena” Alijibu Chiku huku akimpita

“Mbona uko hurry hurry sana?” aliuliza Sadiki huku akimtazama binti ni mweupe peee

“Nataka nikafue”

“Ah kumbe haukai mbali na huku….” Sadiki alisema huku akianza hatua kumfuata “Mbona unatembea haraka subiri basi tuongee”

“Ndio nakaa huku huku ndo nyumbani” Alisema Chiku na kusimama akawa anamtazama Sadiki “Mandi ni kaka yako au?” aliuliza

“Ndio, kwanini umeuliza?”

“Mnafanana”

“Oh, hahaa, ni kweli watu wanasema hivyo, anyway unawahi sana au tunaweza kuongea?” Sadiki aliuliza

“Nawahi, kama unataka tuongee kwanini usichukue namba yangu?” Chiku alisema mwenyewe alikuwa anaulilia wembe sasa ukimkata atajuta

“Oh, hapo umeongea” alisema Sadiki na kutoa m-tecno wake mfukoni akagusa fingerprint “Nitajie sasa”

Ghafla, wakati binti anataka kutaja wakasikia salam “Habari zenu?” , wote waliinua macho na kutazama alikuwa Husna ameshatoka kwa msusi

“Aahaha, safi tu shem….vi….vi….pi” Sadiki alisema kwa aibu

“Safi” Husna alisema na kumsogelea akamshika mkono “Twende nyumbani” alisema huku akimvuta hakutaka achukue namba ya Chiku NA MIMI NA WEWE HATUJUI NI KWANINI HAKUTAKA, LABDA TUTAJUA KATIKA VIPANDE VYA MBELE
USIKOSE SEHEMU YA 05

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!