SEHEMU YA 05
TULIPOISHIA
Ghafla, wakati binti anataka kutaja wakasikia salam “Habari zenu?” , wote waliinua macho na kutazama alikuwa Husna ameshatoka kwa msusi
“Aahaha, safi tu shem….vi….vi….pi” Sadiki alisema kwa aibu
“Safi” Husna alisema na kumsogelea akamshika mkono “Twende nyumbani” alisema huku akimvuta hakutaka achukue namba ya Chiku
ENDELEA
Husna na Sadiki walipofika nyumbani Husna alimuachia Sadiki na kuketi juu ya dumu la maji
“Shem vipi?” Sadiki alimuuliza
“Kaa hapa unazurura nini?” alisema na kuvua kofia kichwani akajikuna kidogo kwenye nywele na kuzipiga piga
“haaah, ndo uninyime fursa ya kuchukua namba?” aliuliza huku akitabasamu
“Sitaki uchukue namba ya Chiku, ana tabia mbaya hakufai” alisema na kuinuka Husna akaenda ndani kuchukua kioo akajitazama halafu akaita “Shemeji” alisema mtoto wa kike
“Nambie shem” Sadiki alisema
“Kumbe nimependeza hivi halafu hunisifii”
“Ah, umenikera” alisema Sadiki
“Mi nakusaidia halafu wewe unalalamika? Au unahisi nini?” Husna kwa hasira “Kama vipi mfuate basi” Alisema Husna
*
Upande wa Chiku alikuwa nyumbani muda huo ndio alikuwa ameanza kufua, alikuwa amekaa na rafiki yake mmoja hivi
“Ila shogaa angu, Da Husna anaboa” alisema Chiku
“Kwanini?” Rafiki yake aliuliza
“Kuna shemeji yake alikuwa ananiomba namba, yaani Husna alivyotukuta alimvuta kwa hasira na kumpeleka nyumbani”
“Usiniambie”
“Ndio yaani kanikera hatari, wanatutia nuksi ndo maana hatuoelewi”
“Hahahahaaaaaa.” walicheka sana
“Au anamtaka nini?” Aliuliza rafiki yake
“Nahisi kwa kweli maana sio kwa kiburi kile”
**
KESHO YAKE SIKU YA JUMATATU!
Sadiki aliamka mapema sana akajiandaa na kuondoka pamoja na kaka yake kuelekea katika ofisi zilizoko katika jiji la Tanga kwa ajili ya mahojiano (interview)
Walipanda bajaji barabarani wakaenda mpaka mjini kabisa, ndipo walipofika
“Diki” alisema Mandi huku akitoa noti ya sh 10000 (Elfu kumi) mfukoni
“Broo”
“Wewe si mtoto wa kiume?” aliuliza
“Yap?”
“Shika hii hela” alisema na kumkabidhi ile noti, Sadiki aliipokea “Nenda ulizia Saad Lal kwenye interview watakuonyesha”
“Haunipeleki?”
“Naenda kuna demu moja nataka nikaonane naye” aliamua kumuambia mdogo wake maana ni wa kiume aliamini hawezi kumsemea kwa mkewe
“Haina noma kaka, nashukuru sana” Alisema Sadiki
“Pamoja”
Waliagana na Diki aliondoka, ila njiani alijiuliza maswali mengi, moja ya maswali aliyojiuliza ni kwamba kumbe kaka yake anamchepuka mkewe, alihisi vibaya maana alikuwa amemuona shemeji kuwa ni mtu poa sana, alikuwa amemzoea kwa kifupi
Basi, muda wa interview ulifika na wote waliotuma maombi waliitwa ndani ya bwalo fulani (Hall fulani)
Muda waliokuwa wanazidi kusubiri itakavyokuwa basi upande wa kaka yake ni kwamba alikuwa na mwanamke mmoja huko mjini, alikuwa anaitwa Sharifa, Mandi alikuwa amemshika mtoto mchanga akiwa anamtazama huku akitabasamu
“Sherry…”
“Abee mpenzi” alisema mtoto Sharifa
“Unajua nawaza sana nitamuacha vipi yule mwanamke wangu maana yeye hajaweza kunizalia mtoto”
“Mmmh mi nilishakuambia uhamie huku ila kwa sababu hunipendi hukutaka” alisema Sharifa kisha akaenda kuketi kando yake na kumbusu shavuni
“Woow…..nina sababu za msingi kidogo, nataka niweke mtaji mkubwa ili mtoto wetu akuwe vyema, na pia tufungue biashara hapa mjini ndo maana nimekupangishia huku mjini”
“Haya bhana, but unajua sana kujali, vipi mdogo wako mbona hajaja?” aliuliza
“Atakuja yuko kwenye interview hapo Saad Lal”
“Sawa, ngoja nikuandalie chapati”
“Ok, andaa halafu……” alisema kumaanisha anataka kitu, lakini hakumalizia sentensi ikabidi wote wacheke
“Yaani wewe” Sharifa alisema
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU