SHEM MI NATAKA (07)

SEHEMU YA 07
TULIPOISHIA
“Shem” Husna aliita kwa mtetemo, kumbuka ana miaka 2 hajawahi kubusiana mdomoni na mwanaume, halafu alikuwa amemzoea Sadiki vibaya sana, halafu alishaona jinsi Sadiki anaushughulikia ulimi wa Bite kwenye video

Udenda ulimjaa na kuanza kumsogelea Sadiki mdomoni taratiibu

ENDELEA
Sadiki alirudi nyuma, alikuwa hataki hilo suala “Sorry shem” alisema Sadiki na kuokota miwa yake akatoka nje na kwenda kula huko mwenyewe

Husna alibaki amesimama katikati ya chumba huku akiwaza, hajui afanyeje moyo ulikuwa ukimuenda kasi kisha akaingia chumbani akaketi kitandani a kushika tama halafu akaendelea kuwaza

“Mimi ni mpumbavu, kidogo ningempa mate….yaani ni shemeji yangu kabisa, alaah Mungu niepushie hili” aliwaza Shemeji Husna

Sadiki naye pia alokuwa na mawazo katika upande wake huku akila vile vipande vya miwa
“Shit, hivi imekuwaje nikamshika shemeji vile? Yaani broo angenikuta angenikata mapanga oh Mungu wangu…..halafu nilisimamisha” aliwaza sana

Mawazo yalimzidi pia kwa kukumbuka ya kaka yake “Ila broo kwanini anaamua kum-cheat huyu mwamamke mzuri namna hii?….yaani daah asingekuwa shemeji yangu, haki ya Mungu ningemla” aliwaza sana.

“Shem” akiwa katikati ya mawazo ghafla alisikia sauti iliyotokea puani mwa Husna ikimuita, iliita kimideko binti alikuwa anajisikia tofauti mwilini.

Sadiki aliondoka kwenye mawazo kisha akamtazama shemeji aliyekuwa mlangoni na mkononi ameshika mfuko

“Naam shemeji” aliitika Sadiki

“Twende bhaaasi” alisema huku jicho limemlegea anaangalia kama vile anataka kusinzia

“Wapi???” Sadiki aliuliza kwa mshangao, akili yake iliwaza labda shemeji anataka kumpeleka ndani ili akampelekee moto

“Mh, si ulisema unaenda kwa mpemba kupeleka simu wewe?” aliuliza huku akitabasamu “Au ulidhani nataka twende wapi jamani shem wangu” alisema Husna

“Hapana shem, niliwaza mbali”

“Mbali wapi?” aliuliza huku akitoka pale mlangoni na kurudishia mlango halafu akapiga hatua za madaha “Eti ulidhani nataka twende wapi?” aliuliza zaidi

“Hamna shem, twende kwa mpemba”

“Mh, wewe nambie tu unaogopa nini?” aliuliza Husna

“Ahahaa, shemeji nawe kwa kukazia kitu” alisema sadiki na kutaka kumpatia shemeji yake mfuko wa miwa

“Mi sili” alisema Husna huku akiendelea kutembea na sketi yake ndefu kaishikilia kwa mkono mmoja

“Kwanini? Au haupendi?” Diki aliuliza na kumfuata “Ah halafu nimesahau chaja” alisema

“Yeye mwenyewe ana chaja za kutosha”

“Ok, twende” Diki alisema

Walitoka kwa pamoja halafu wakatembea kwa mwendo wa taratibu kuelekea maeneo ambayo kidogo yalichangamka, kulikuwa na magenge na vituo mbali mbali kama bodaboda na maduka mengi mengi, pia pub za kupiga vinywaji

“Ndo pale” alisema Husna

“Wap?” Sadiki aliuliza huku akiangaza macho

“Pale kwenye frem nyeupe”

“Oh, twende basi, au ngoja niende peke yangu”

“Nenda, nitakupitia hapo ninanunua vitu vichache vya kwenda kupika” Husna alisema

“Okay”

Sadiki aliachana na shemeji yake halafu akaenda kwa mpemba kupeleka simu yake, kabla hajafika alisikia sauti nyuma yake
“Dikiii….We Sadiki”

Aligeuka haraka na kukutana na Chiku muuza mboga akiwa anamfuata nyuma kwa tabasamu zito

“Mamboow” Alisema Chiku

“Safi tu mrembo mzima wewe?” aliuliza

“Mi mzima za tangu juzi” aliuliza

“Safi tu kumbe unalijua jina langu”

“Mh ndio, kwani vibaya?” aliuliza Chiku huku akimfikia na kumpa mkono wakasalimiana

“Nope, ila nawaza umelijuaje”

“Hahaha, kaniambia kaka yako, vipi unaelekea wapi mbona uko mwenyewe huogopi kupotea akati wewe mgeni?” aliuliza mtoto wa kike

“Ahahaha siwezi potea, niko na shemeji ameenda gengeni tu hapo” alisema Sadiki maneno ambayo yalilikata tabasamu la Chiku

“Uko na shemeji yako?”

“Yeap”

“Ok, basi poa mimi naenda hapo mbele kwa rafiki yangu labda tutaonana tena siku nyingine”

“Ok” Sadiki alimaliza kihivyo alikuwa tayari ameshaambiwa binti sio mtu mzuri na shemeji yake

Chiku alipiga hatua mbili tatu halafu akamgeukia Sadiki kuna kitu alitaka kumuambia ila aliogopa yeye ni mtoto wa kike bwana, lazima asubiri aanzishwe yeye

Aliendelea kutembea Chiku kuelekea mtaani huko huku akiitukana nafsi yake
“Yaani najisikia vibaya nikimuona nawaza sana, ila kesho nikipita na mboga sijui itakuwaje” alkwaza mengi sana kiukweli huyu msichana alikuwa ameshadondoka kwa mwamba ila sio kwamba alikuwa na mapenzi kivile ka hasha, alikuwa anahitaji kuolewa maana aliona umri umeshamtupa sadakalawe

Sadiki alimpa mpemba simu, mpemba akaibandika kagundi kenye jina la Husna na sio la Sadiki maana Sadiki asingefahamika pale kwani alikuwa ni mgeni, alisogea kumsubiri shemeji yake

Alisubiri kama dakika tano ndipo akamuona Husna akija pamoja na mumewe bwana Mandi na kumfikia pale Sadiki

“Broo” Sadiki alisema

“Vipi dogo”

“Poa, umerudi?”

“Ndio, nilishindwa kupokea simu yako bwana nilikuwa katika harakati ngumu” alisema

“Hamna shida kaka” waliongea huku wakitembea kuelekea nyumbani

“Vipi interview?” aliuliza

“Ah, Mungu ajalie tu, ilikuwa ya kawaida sio ngumu wala rahisi, ilikuwa wastani tu”

“Usijali dogo mambo yatakaa powa”

“Ni kuombeana kaka”

Walizidi kutembea muda wote Husna alikuwa kimya hana usemi wowote na hata walifika nyumbani.

“Leo nimechoka siendi kuvua” alisema Mandi”

“Aah?” aliuliza Husna kwa mshtuko

“Yes” alisema, kumbe yeye alichoshwa na viuno vya sharifa

“Itakuwa vizuri, ni muda sijalisikia joto lako usiku” alisema Husna

“Et ee”

“Ndio mume wangu” alisema Husna

Husna alianza kuandaa chakula cha jioni Sadiki alikuwa ameketi anacheza gemu kwenye kiswaswadu cha shemeji yake, ghafla Husna alikuja kisirisiri na kumpatia tunda mkononi

Sadiki alilitazama bila kaka yake kuona, akagundua ni tufaa (Apple), juu limebandikwa kakaratasi kadogo kameandikwa “that’s my heart” alishtuka kidogo lakini alihisi ni apple tu tunda kama matunda mengine

“Asa…..” alitaka kushukuru ila Husna alimuonyesha ishara akae kimya asiongee chochote, aliendelea kupika huku Mandi akiwa amejilaza kitandani anasubiri msosi uive

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!