SEHEMU YA 08
Ghafla simu ya Mandi ilipigwa akiwa kitandani, na alipoitazama namba alisevu kwa jina la Zuberi. Aliipokea
“Oi” alisema
“Oya wapi kaka njoo kuna mchongo….Mwanangu”
“Mi nimelala bwana” alisema Mandi
“Njoo bwana, Medi mchuuzi katuletea pesa yetu ile”
“Eenh???” aliongea kwa mshtuko mara baada ya kusikia neno pesa
“Njoo fala wewe unalala lala nini?” Zube alikata simu
Mandi alishuka kitandani haraka na kuvaa shati halafu akabeba begi lake na kutoka nje akakuta Husna akiwa anakuna nazi huku Sadiki akipembua mchele
“Khee mume wangu wapi tena?” aliuliza Husna
“Nimeitwa fasta kuna dili, nimechoka ila ngoja nikapambane nitapumzika kesho”
“Mmmmh, chakula hauli jamani?” aliuliza Husna
“Kesho nitakula” Alisema huku akiondoka
“Mh bhana Mume wangu nilikuambia hujalala muda mr…..” alikuwa akiongea ndo mandi anaondoka haraka kuwahi pikipiki.
Husna alikasirika maana alijua siku ile wangeweza kuburudishana, halafu isitoshe muda ule aliokuwa amesimama karibu na Sadiki wakasogezeana midomo, ilimpelekea mwili wake kubadilika siku yote akawa anawaza mambo yale tu.
Sadiki alikaa kimya, ila binti alikuwa akisonya sonya tu.
“Diki huogi leo?” aliuliza Husna
“Lazima na nisipooga sitalala mwili utaniwasha sana”
“Basi kaoge ndo uje ule”
“Sawa shemeji” alisema Sadiki
Diki alijiandaa kwenda bafuni ndipo akaenda kuoga na baadaye kutoka akavaa suruali ya traki suti halafu akaketi huku akiiwaza simu yake “Ningekuwa hapa nachati tu” aliwaza
Husna alimletea chakula baada ya kumaliza kupika vizuri halafu akamuacha akila naye akaenda bafuni kuoga
Husna hakutumia dakika nyingi bafuni, alitoka akakuta Sadiki hajamaliza kula bado
“Hee hujamaliza kula bado”
“Yeah, umeoga muda mfupi, halafu mimi siwezagi kula haraka haraka” alisema Sadiki
“Mwanaume gani usiyeweza kula haraka haraka?” aliuliza wote wakacheka kidogo sana na Husna aliingia ndani
Baada ya dakika 7 Husna alirudi akiwa na sketi na blauzi halafu akasimama karibu na Sadiki, ilikuaa ni muda wa saa 12, kagiza ka usoni usoni hivi, akaanza binti kujikuna
“Mh, yaani siku hizi nawashwa” alisema binti
“Unawashwa kwanini?” aliuliza Diki
“Yaani nikivaa shangaa tu nawashwa hatari sijui kwanini”
“Yaani kivipi unawashwa wapi?” aliuliza Diki maana naye kwa kumaanisha hajambo
“Heeeh, yaani wewe shemeji mawazo yako, mi nawashwa kiuno” alisema Husna huku akikishika kiblauzi chale na kukinyanyua akaacha kiuno kilichojaa shanga kama mistari minane (8) na tumbo wazi, “Onaa shem” alisema Husna huku alizishika shika zile shanga “Yaani zinawasha hatari” alisema na kujitazama halafu akajishika kitovuni na kupaachia.
Sadiki alishindwa kumeza funda la ubwabwa akabaki anamtazama shemeji yake kiunoni……JE ITAKUWAJE? HAWA WATU HAWA WANAKOELEKEA MIMI NA WEWE HATUJUI, TUWAOMBEE WASIJE WAKAHARIBU….
JE WATAWEZA KUVUMILIANA?
USIKOSE SEHEMU YA 09
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU