SHEMEMU YA 09
TULIPOISHIA
“Yaani nikivaa shangaa tu nawashwa hatari sijui kwanini”
“Yaani kivipi unawashwa wapi?” aliuliza Diki maana naye kwa kumaanisha hajambo
“Heeeh, yaani wewe shemeji mawazo yako, mi nawashwa kiuno” alisema Husna huku akikishika kiblauzi chale na kukinyanyua akaacha kiuno kilichojaa shanga kama mistari minane (8) na tumbo wazi, “Onaa shem” alisema Husna huku alizishika shika zile shanga “Yaani zinawasha hatari” alisema na kujitazama halafu akajishika kitovuni na kupaachia.
Sadiki alishindwa kumeza funda la ubwabwa akabaki anamtazama shemeji yake kiunoni……
ENDELEA SASA
Husna alipomtazama Sadiki akagundua Sadiki ameanza kuteseka, ndo kabisa akaamua kufanya makusudi akajigeuza huku akicheka cheka akamuonyesha upande wa nyuma mgongoni, na makalio
“Zinawashaa” alisema binti makusudi huku akiangalia mbali. Sadiki aliona vidimpo viwili viko mgongoni maeneo ya kiuno cha shemeji yake kisha akaangalia chini akijua kabisa anahitajika kwa muda ule
Shemeji alijifunika na kupiga hatua kuelekea jikoni ili ajichukulie chakula pia, “Diki umeshiba au nikuongeze?” alisema Husna
“Nimeshiba tayari” Sadiki aliongea na kumalizia vijiko viwili vya ubwabwa halafu akapeleka sahani na kusimama jikoni “Shemeji” alisema Sadiki
Husna aliinua jicho legevu na kumtazama “Abe shem wangu” alisema
“Tafadhali acha tabia hii mimi najisikia vibaya unapofanya vituko mbele yangu, sio vizuri mimi ni shemeji yako
Husna alimtazama kwa muda wala hakujibu chochote, halafu aliendelea kupakua chakula.
“Asante kwa chakula” Sadiki alisema halafu akaondoka na kuingia ndani ya nyumba
Japo ilikuwa ni mapema sana, lakini Sadiki alishusha chandarua, mbu walikuwa ni wengi hivyo alishusha chandarua kisha akajilaza ndani yake
Mawazo yalikuwa ni mengi sana mpaka pale ilipofika saa mbili usiku ndipo usingizi mkali ulipomkamata
Husna alijitahidi, kumalizia malizia kazi naye akaingia ndani ya mjengo na kujirusha kitandani. Huwezi amini, kwa jinsi mwili ulivyokuwa unamuwaka moto, alijikuta anajipapasa mwenyewe, hajui afanyeje, alijishika shika maziwa na kiunoni huku akithubutu hata kuupeleka mkono kwenye sehemu zake nyeti na kupapachezea chezea
Sadiki hakuwa na lile wala hili, hakujua kuna mtu anahitaji huduma ambayo yeye alikuwa nayo, vivyo hivyo Mandi naye alikuwa kando ya bahari akipata kufanya kazi ngumu ya kutafuta chochote kitu, hakujua mkewe amemmiss sana
Mpaka muda wa saa sita bado Husna alikuwa macho, kuna muda alijiambia “Nimfuate shem kwake au?” aliketi kitandani lakini alipofumbua macho hivi akaona dirishani kama vile kuna mtu anachungulia ndani
Ni mara ya pili binti alikuwa akimuona huyu mtu, hakujua alikuwa anafanya nini pale dirishani na hakuelewa ana nia gani. Husna hakujitikisa aliendelea kumtazama ajue anataka kufanya nini
Yule mtu aliondoka pale kwenye dirisha la chumba cha Husna na Mumewe halafu akahamia cha Sadiki na kujaribu kuchungulia. Kwa kuwa kulikuwa na giza nene, hakuweza kuona ndani kinachoendelea, zaidi alimsikia tu Sadiki akikoroma kwa maana nyingine alikuwa kwenye usingizi mzito sana
Husna alishuka kitandani taratibu na kusogea dirishani halafu akachungulia dirishani ndipo akamuona yule mtu anaondoka taratiibu na alipofika mbele kidogo aliwasha mwanga wa simu yake na kuendelea kutembea huku akiichezea
“Huyu ni nani?” aliwaza Husna “Kwanza anataka nini?” alijiuliza hadi akapata hofu.
Husna siku ile hakupenda kukaa kimya aliamua kumfuata shemeji yake sebuleni na kumuamsha “Shem shem…..shemeji…..wewe Sadiki” alisema
“Mmmh” aliitika kwa sauti nzito halafu akajigeuza na kuendelea kuuburuza
“Wewe shemeji” alizidi kumuita halafu akachomoa chandarua kidogo na kumgusa akawa anamtikisa tikisa
Sadiki alikurupuka usingizini na kutazama kwa macho makali akakuta Husna anammulika na kisimu chake kidogo “Shemeji amka” Alisema Husna
“Vipi shemeji” Sadiki alisema huku akijibanza kwenye godoro
“Kuna mtu anakuja kila siku kuchungulia hapa dirishani usiku sijui ni nani” alisema
“Eeh?” Sadiki aliuliza “Anakuja kila siku?”
“Ndio, juzi nilimuona na hata leo tena nimemuona sijui ni nani na anataka nini” alisema
“Mh, yuko wapi” alisema huku akiketi na kutazama dirishani
“Ameshaondoka”
“Basi kalale mimi niko macho ntaangalia kama atakuja”
“Sawa shem” alisema Husna na kuinuka akatembea kuelekea chumbani
Sadiki bado usingizi ulikuwa ni mzito na alitamani aendelee kupata fursa ya kulala ndipo akavuta pumzi na kutoka ndani ya neti akasimama dirishani na kuchungulia nje, aliona kuna taa za umeme zinawaka katika nyumba za majirani ila hakuona chochote.
Sadiki bila kujiamini alitoka nje ya chumba kwa sababu alikuwa na mkojo, alienda haraka nje akakojoa na kurudi ndani.
Alipofika ndani alifunga mlango kisha akakisogelea kigodoro chake na kuingia ndani yake, alipofika ndani anataka ajifunike alishangaa kumuona shemeji yake anamfuata tena chumbani
“Shem vipi?” Sadiki aliuliza
“Shem naogopa kulala mwenyewe” alisema mtoto wa kike kwa mideko
“Kivipi shem”
“Shem…..” alisema huku akisogea katika eneo alilokuwa analala Sadiki akachuchumaa “Huyo mtu aliyekuwa anachungulia ameniogopesha halafu pia nahisi baridi sana kule peke yangu” alisema
“Please kalale shemeji haya ni majaribu”
“Sadiki” alisema Husna huku akitaka kuingia ndani ya Chandarua cha Sadiki ikabidi Sadiki amsukume
“Tafadhali nenda kalale unataka kufanya nini Shemeji lakini?” aliuliza “Huoni watu wanachungulia huko unahisi wakituona tukiwa hivi itakuwaje? Au huelewi inawezekana ni broo? Au hata kama sio broo labda amemtuma mtu aje atuchunguze”
“Mh” aliguna Husna huku akijiokota chini na kusimama “Sorry shem” alisema Husna na kuinuka
“Samahani nimekusukuma ila please naomba ukalale kule shemeji, sio vizuri” alisema Sadiki na Husna aliondoka akaenda kulala zake
***
Asubuhi saa mbili Sadiki alikuwa ameshaamka anaswaki nje ya nyumba, aliswaki huku akitafakari mengi sana. Akamaliza akarudi ndani
Akiwa amesimama katikati ya chumba cha sebuleni Husna alitoka na khanga hii…moja, halafu akatoka nje pia akaswaki na kurudi ndani
“Umeamkaje Shem” alisema Sadiki maana Husna alikuwa hajamsalimia
“Safiii tu” Alisema Husna na kumgeukia macho yakagongana yalikuwa yanaongea peke yake yakisema ‘shem ninakuhitaji’ halafu akaingia ndani ya chumba chake huku akijitikisa
Sadiki alimtazama huku naye shetani akimuambia “Diki, usimsamehe huyo”
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU