SEHEMU YA 11
TULIPOISHIA
Sadiki alitembea tembea akaona anunue mihogo wakanywee chai halafu akondoka kuelekea nyumbani, kweli alipofika alimkuta shemeji akiwa anaandaa chai na kaka Mandi amesharudi, hata hivyo shemeji alikuwa amevuta mdomo maana alikuwa amenuna kisa Diki kukataa busu lake
“Kaka za asubuhi” Sadiki alimsalimia kaka yake
“Salama vipi?”
“Poa poa” alisema Sadiki kisha akampeleka mihogo Husna akaikamata na kuitupa juu ya ndoo kwa hasira
Sadiki alielewa lakini je angefanyaje? Ni shemeji
EDELEA SASA
Sadiki aliingia ndani akachukua mkeka na kuutoa nje halafu akauweka barazani na kuketi hapo.
Aliwasha data kwenye simu yake halafu akaanza kuchati na Bite online
“Nisamehe Beatrice nilishakuambia kwa bro hakuna umeme hivyo chaji inasumbua
“Chaji kivipi? Mbona nilikuwa nakuona online?” Beatrice alikuja juu
“Aah, sorry naingia mara moja moja”
“Mara moja moja ndo usinitext, ukiingia unamtafuta nani eti?” aliuliza Beatrice (Bite)
“Naangalia kama kuna mtu amenitafuta”
“So mimi messages zangu huzioni si ndio? Ok anyway endelea na unayoyafanya Diki nakuambia utanikumbika kama hunipendi si useme?”
“Hamna nakupenda”
“Kwanza unarudi lini?”
“Interview ya kwanza tayari, nasubiri kama matokeo yakitoka niitwe kwa ajili ya kwenda kufanya ya pili”
“Ok goodluck, japo saa nyingine najikuta nakuombea hata usipate ili urudi nyumbani mi sipaamini huko kabisa”
“Mmmh”
“Ndio, ila kama hujapangiwa kuwa wangu basi tu” alisema binti
“Ok bye bye”
“K”
**
Sadiki, Mandi na Husna walipata kifungua kinywa halafu baada ya kunywa tu Husna alitoa nguo zake na kuanza kuzivua.
Mandi alilala zake kama kawaida, mchana alilala halafu jioni aliondoka nyumbani kila mara.
Sadiki alikuwa hana kazi alichezea tu simu yake ya mkononi na hata ilipofika saa sita kasoro alimuona Chiku akiwa anapita barabarani huku akiwa na beseni tupu kwa maana alikuwa amemaliza kuuza mboga zake.
Chiku na Sadiki walitazamana wote wakatabasamu, hii Husna hakuiona na hata Chiku alimpungia na kupita akiwa na furaha
Sadiki alichukua fursa ile kumtumia message lakini Chiku hakujibu kwa sababu alikuwa ameacha simu nyumbani tangu asubuhi. Alipofika Chiku alikuwa amevuja jasho hivyo akaamua kuoga za kubadili nguo kisha akaketi kitandani na kuanza kupiga mahesabu yake ya biashara hiyo ya mboga mboga
Baada ya dakika moja alimaliza na alihifadhi pesa, aliishika simu na kukuta jumbe kadhaa, moja ilikuwa ya namba mpya na hii ilitoka kwa Sadiki, binti alitabasam
“Mambo vipi pole na kazi” ilikuwa meseji kutoka kwa Sadiki
“Asante, pole na wewe kwa kuchat 😂😂😂” alijibu binti kwa mbwembwe
Sadiki aliutazama ule ujumbe akatabasam “Nachat sana et?” aliuliza
“Ndiyo kila mara huwa nakukuta ukichezea simu inaonekana wifi yetu anakuweka sana bize”
“Hahahaha, wala!” Sadiki alijibu
“Nini? Ina maana unataka kukataa?” alimuuliza
“Yeah, haniweki bize” alisema Sadiki
“Ila yupo?” aliuliza Chiku, hii yote ni kwa sababu alitaka adanganywe, yaani alitaka angalau Sadiki aseme hana mtu ili binti ajipendekeze
Kwa kuwa Sadiki naye alikuwa na uchu wa madaraka alijikuta anawadanganya wapiga kura
“Kwani mnaeleweka basi? Mimi naogopa sana” alisema ila kumbuka ana Beatrice kamuacha huko kijijini kwao
“Hahah wewe acha mambo yako, eti hatueleweki tena najua kabisa hauwezi kukosa mtu, mkaka mzuri, handsome na upo hivyo uwe single kabisa kabisa? Hapana” binti aliendelea kumchimba ikabidi Sadiki apotezee
“Hivi unaishi wapi?” Sadiki alimuuliza
“Sio mbali na hapo kwenu unavuka nyumba kama 6 tu unafika kwetu”
“Haya baadaye nitakuja kukusalimia”
“Karibu sana!” binti alisema
“Thanks, hivi unaitwa Chausiku ee?” Sadiki aliuliza “Maana namba nimesevu kwa jina Mrembo” alisema Sadiki
“Hahaha, wewe mkaka wewe sasa urembo upi jamani, hahaha umejua kunifurahisha” alisema binti akaongeza na nyingine “Mi naitwa Chiku bhana”
“Anhaa basi ngoja niiongezee iwe mrembo Chiku”
“Hahaha, hayaa” binti alifurahi sana “Ushakula lakini?” alijifanya ameanza kumjali
“Bado” alisema Sadiki
“Ule bhana, kwanini hujala sasa?” Binti alisema
Sadiki alipoona wanaelekea pabaya na yeye bado hajaridhia aliamua kupotezea ule ujumbe na kuendelea na mambo mengine.
Ilipita muda mrefu kidogo ndipo shemeji Husna akaandaa chakula cha mchana, ni kweli siku ile Husna alikuwa amemnunia kabisa Sadiki, alichokuwa anamaindi ni kwamba Sadiki alikuwa hataki hata busu, yaani haya mambo haya kukataliwa tu unanuna ndo mambo gani hayo?
Sadiki akiwa anakula alimuuliza shemeji “Mbona kama vile hauko sawa shem?” aliuliza Sadiki wakati huo bado Mandi anauburuza usingizi
Husna alimgeukia shemeji yake na kumuongelesha “Niko sawa shem” alisema mtoto wa kike
“Hapana shem hauna furaha”
“Diki” Husna aliita huku akimtazama na mkono mmoja kashikilia dera lake “Unajua kila siku huwa sina furaha na naamini unaifahamu sababu” alisema na kugeuka akaendelea na kazi zake
Sadiki alitafakari akakumbuka ni kweli kuna siku shemeji yake alishawahi kumuambia kwamba hana furaha kwa sababu hana mtoto na pia haridhiki na penzi analolipata kwa Mandi
Sadiki alikaa kimya akaendelea kula ugali huku Husna akichacharika na kazi zake.
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU