SHEM MI NATAKA (12)

SEHEMU YA 12

*
JIONI MUDA WA SAA KUMI NA MBILI NA NUSU
Mandi aliacha shilingi elfu kumi na kuondoka kama kawaida yake, Sadiki muda huo alikuwa nyumbani bado na alikuwa akiendelea kuchezea simu kama ilivyo kawaida yake

Ghafla ujumbe kutoka kwa Chiku “Shikamoo kaka” si unajua yale mahaba yanavyoanzaga kama utoto fulani

“Mmmh, marahaba ila unanisalimia unataka kuninyima nini?”

“haaa, jamani mimi ni mtoto kwako”

“Mtoto? Kwani mtoto ndo haiingii”

“Wewee….haiingii nini? Acha mambo yako, uko wapi?” aliuliza binti

“Niko nyumbani”

“Si ulisema utakuja kwetu mbona hujaja?”

“Aaah nilisahau”

“Haya njoo sasa hivi” alisema

“Mh nije wapi?”

“Si kwetu jamani?” Aliuliza

“Utanibusu?” Sadiki aliuliza

“Chitaki” Binti alijibu kimahaba

“Mmmh”

“Unaguna nini mi chitaki, katoto katambusuje mkaka mkubwa hivyo”

“Basi siji mimi”

“Njoo bhaaaana!!!” binti alisema “Mi ntalia sisi watoto tunapenda kulia ujue” Chiku alibembeleza sana

“Hayaaaa usilie”

“Haya njoo basi na wewe, nitakupa hilo busu lako” alisema

“Hapo sawa nakuja ila nataka la mdomoni”

“Mdomoni?, wewe!!! Mh”

“Nini sasa”

“Naogopa mdomoni huko tatizo ila njoo tutajua namna ya kufanya” alisema Chiku

“Ok Powa, nipitie mtaa upi?” aliuliza

“Pitia pale tulipoonana muda ule”

“Okay poa”

“Usichelewe, sawa?” aliuliza Chiku

“Sawa”

*
Sadiki hakutaka Husna ajue kwamba anaenda wapi, aliinuka taratibu na kwenda mpaka barabarani huku akijifanya anaongea na simu, Husna hakuelewa chochote maana alikuwa ndani

Baada ya dakika 3 Husna aliongea akiwa ndani kwa kujua Sadiki bado yupo pale nje

“Shem na jua utakuwa na njaa, vipi? Utakula tambi?” Husna aliuliza lakini kimya kikatanda “Eti shem, wewe” alisema binti

Alipoona hakuna anayeitika, alitoka nje na kuangalia akaona kweli Sadiki hayupo “Kaenda wapi?” alijiuliza.

Alipokaa kaa muda bila Sadiki kurudi aliona bora akachukue Tambi dukani aje azipike chap.

Alifunga tenge kisha akabeba mfuko na pesa akatembea kuelekea dukani.

Njiani hakukutana na Sadiki wala chiku ila baada ya kununua wakati wa kurudi, alisikia kando ya barabara ndimi zikilia, akajua kuna watu wanapigana lita, akaamua kuchungulia maana alikuwa anateseka na mapenzi sana.

Alipochungulia hivi aliona tisheti ya Sadiki iliyokuwa na mistari meupe na meusi ikiwa imemkumbatia mtu chochoroni huku wakipapasana. Alijua ni shemeji yake akaamua kupita zake

Alipofika nyumbani alikuwa na hasira sana maana mwenyewe alikuwa anampenda huyo shemeji halafu anampa fursa binti mwingine yeye anaachwa na utamu wake

“Haa ila huyu mvulana ni hatari, hana hata wiki ameshapata mwanamke” alijisemea na kupiga makofi halafu akaanza kupambana na kazi zake

Akiwa anaenda kumwaga maji, ghafla barabarani alimuona chiku amepita kwa, mwendo wa haraka haraka kwa sababu alifahamiana naye kwa muda mrefu basi alielewa kabisa yule ni Chiku halafu Chiku siku zote huwa hapiti kwa bila kumchangamkia, ila siku hiyo alipita. Husna alihisi kitu na kubaki anatazama tazama

Baada ya sekunde chache tu, aliona tisheti ya miraba meusi na meupe ikitokea kule kule alipotokea Chiku

Husna alikasirika sana na hata kujikuta anataka kulia. Husna alikuwa ameshampenda shemeji yake kupitiliza na alikuwa na wivu naye tayari “Kumbe ndo maana alikuja kumuulizia asubuhi” alianza kuunganisha matukio “Haya bwana”

Sadiki alifika nyumbani anaona ona aibu yaani mtu akifanya uovu huwa anajishtukia sana

“Pole na kazi” Husna alianza uswahili ndipo Sadiki akashtuka

“Pole for what?” aliuliza Sadiki

“Si umetoka kazini?” aliuliza Husna

“Aah shemeji bhana si nimetembea tembea tu?” aliuliza mtoto wa kike

“Kutembea tembea ee? Nimemuona kapita hapa si ndo mlikuwa naye kwenye ukuta wa rangi ya pinki pale” alisema

Sadiki alikaa kimya alijua ameshaonekana hakusema neno

“Ogopa sana hili eneo, kuna UKIMWI mno” alisema

Sadiki alikuna kichwa na kumtazama “Shem unapika nini?” aliuliza kupotezea ila Husna alikaa kimya akaendelea na kazi zake

Baadaye muda wa saa 3 chakula kilikuwa tayari, alimpakulia shemeji yake akampa na kikombe cha chai inayonukia sana.

Sadiki alivifeka mkekani halafu baada ya kula alikusanya vyombo na kupeleka ndani.

Alipofika ndani alishangaa kusikia kwikwi kama vile shemeji Husna analia chumbani

“Shem” aliita kwa mshangao kidogo hakujua shemeji yake analia nini “Shemeji vipi kuna tatizo?” aliuliza

“Daaah” shemeji alizidi kulia chumbani, masikini ya Mungu hakuna raha anayoipata zaidi ya kula chakula

Hana utajiri, hana mapenzi ya kweli kutoka kwa mumewe na wala hana mtoto wa kucheza naye
“Mungu kwanini mimi?” alijiuliza Husna

Sadiki aliamua kusogea mlangoni mwa shemeji yake akamkuta shemeji ameketi ameshika tama anaendelea kulia kwa kwikwi

“Shem kuna tatizo gani?” Sadiki aliongea huku akiingia ndani ya chumba cha kaka yake

Husna aliendelea kukaa kimya ikabidi Sadiki amfuate hadi pale kitandani alipoketi
“Shem mbona unalia, kuna shida gani?” alimuuliza

“Shem please kalale”

Sadiki aliamua kumshika shem lakini shemeji alimsukuma “Niachie” alisema

Sadiki aligundua kwamba shemeji ana hasira naye, aliketi kando yake na kumuongelesha
“Samahani, huenda ikawa mimi ndo nimekukera shemeji, nisamehe Sana

Husna alinyanyua uso akamgeukia sadiki akamtazama, ndani kulikuwa na mwanga hafifu wa taa ya sola ndogo.

Sadiki alipomtazama aligundua shemeji yake amelia sana machozi yalikuwa machoni na mashavuni.

“Unalia nini?” alimuuliza

“Naumia kwa ajili yako Shem” aliamua kujiweka wazi hisia zake

“Kivipi?” Sadiki aliuliza lakini Husna alirudisha kichwa chini anajishika shika vidole vyake

JE ITAKUWAJE? USIKOSE SEHEMU YA 13

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!