SEHEMU YA 18
Baadaye kidogo
“Kwani ilikuwaje mpaka ukawa umebeba yale makopo yote hujui ndo yalikufanya upate ajali?” alimuuliza rafiki yake mmoja aliyekuwa naye hospitalini pale
“Bro nilikuwa nampelekea, Husna akaweke juisi zake auze” alisema Mandi
“Ahahahah alikuwa anakulipa au?” aliuliza kijana huyo
“Hamna”
“Ahahaahhaa…..unazingua kinoma” Kijana yule alimcheka sana
*
Basi habari zikasambaa kijiweni kote kwamba alikuwa anamsaidia Husna ndipo Husna akaanza kuchambwa na mashoga zake
“Nenda kamsalimie kaka wa watu aliumia kwa sababu yako” alisema shoga ake
“Mi sikumtuma” alisema Husna
“Acha roho mbaya, kamsalimie ukamuone tu” alisema binti mwingine tena
“Niacheni bwana” Husna alikuwa akijaribu kukwepa hilo jukumu
**
Baada ya watu kumshawishi sana, Husna aliamua kuamka mapema asubuhi na alimtembelea Mandi katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam
Alifika mapema sana na alimkuta mandi akiwa amefumba macho anavumilia maumivu makali aliyokuwa akiyapata. Husna alisimama kando ya kitanda na kumtazama huku akimhurumia sana.
Baada ya sekunde takribani 45, Mandi alifungua macho na alipotazama alishangaa kuna mtu kando yake amesimama ikabidi amzingatie
Alipomtazama ni Husna tena machozi yanamlenga lenga
“Husna” alisema Mandi huku akijaribu kuinua uso amtazame
“Mandi….” alisema binti na kujifuta machozi “Umeumia kwa ajili yangu? Sikujua umeumia hivi” alisema Husna na kuketi kando yake akamshika mkono
“Aaah usishike mkono unauma sana” alisema
“Eeh” Binti alishtuka “Huu umevunjika?” aliuliza
“Hapana umetenguka”
“Jamani pole” alisema binti
Basi ilikuwa hivyo walisalimiana na kisha binti aliondoka huku akimhurumia sana.
Kuanzia hapo Husna alihusika kumletea chakula kila mara mpaka mwezi ulipokatika akawa anatakiwa atolewe hospitali
Mandi hakuwa hata na shilingi mia ya kulipa, mbaya zaidi alikuwa anadaiwa,shilingi milioni moja na laki moja, biashara yake ya dagaa ilikuwa imeshakwisha na asingeruhusiwa kutoka hospitali bila kulipia gharama hizo.
Husna alifika siku moja hospitalini
“Naomba unisaidie Husna nahitaji kutoka hapa nikatafaute maisha nimechoka sasa”
“Nikusaidieje?” aliuliza Husna
“Ninadaiwa milioni moja na laki moja natakiwa nilipe waniruhusu na kadri ninavyozidi kukaa hapa ndo gharama zinazidi mara mbili, sasa naomba unisaidie hata kiasi kidogo cha fedha”
“Mandi” Binti aliita kwa utulivu “Mimi hiyo milioni napata wapi? Biashara yangu unaijua, mpaka sasa nina baki ya shilingi laki tatu tu na natakiwa nilipe kodi wiki ijayo nikikupa nitaishije?” aliuliza mtoto wa kike
“Daaaah!” alisema Mandi
Machozi yalianza kumtiririka Mandi kwa kipindi kile, hakuwa na namna yoyote ya kuweza kuondoka pale alitoa maneno ya uchungu akisema hivi
“Kuzaliwa katika nyumba ya masikini kuna matatizo sana, sina hata ndugu mmoja ambaye amenitafuta wala kunisaidia hata kwa shilingi 100, kwanini MUNGU hukuacha nife kabisa? Haya maisha yana raha gani? Nina miaka 30 sina kitu chochote zaidi ya kipande cha godoro na nguo nazovaa, hii yote kwa sababu ya umasikini….” alisema Mandi na kulia sanaaa tu
“Usilie mandi, muombe Mungu”
“Daaah, Mungu gani zaidi ya huyu aliyetuumba? Naumia sana Husna naumia, daaah bora ningepata tatizo lingine, je hili la pesa nyingi hivi nitawezaje?”
Mandi alilia kwa uchungu mpaka Husna akajisikia vibaya
Baada ya Husna kuona vilio vimezidi aliondoka zake na kumuacha Mandi akilia.
Kama utani Husna alishindwa kufanya chochote kwani alikuwa akiyawaza mambo ya Mandi tu, kichwani hakuwa na raha!
“Naumia” alisema binti
*
BAADA YA WIKI MOJA
Hakukuwa na shughuli yoyote iliyokuwa imefanyika kukamilisha iwezo wa kumuwezesha Mandi aondoke pale hospitalini, hakuna juhudi iliyokuwa imefanyika.
Ghafla Mandi akiwa hana hili wala lile, Husna alitokea hospitalini akiwa amebeba Hotpot jioni, alipolifunua hotpot lilijaa pilao pamoja na nyama za kutosha halafu alimpatia
“Kula usiwe na mawazo” alisema Husna kwa uso uliokuwa na tabasamu pana
“Mbona una furaha?” aliuliza Mandi
“Nataka nikufanyie surprise” alisema Binti
“Surprise gani?”
“We kula umalize halafu nikupatie surprise”
“Ok” alisema Mandi
Mandi alifukia ile pilao kisha akanywa maji na kumtazama wote wakatabasamu.
Binti alimshika shavuni kisha akafungua pochi na kutoa kitita cha pesa na kumpatia
“We!” Mandi alishangaa
“Za nini hivi?” aliuliza
“Lipia hapa hospitali itabaki nauli, nenda kwenu kajitibu halafu utanitafuta” binti alisema huku alimuandikia namba ya simu kwenye kikaratasi na kumkabidhi
“Umezipata wapi pesa hizi?” aliuliza Mandi ila binti alinyanyua pochi yake na kuondoka akiwa analia
JE ITAKUWAJE? USIKOSE MWENDELEZO WA KUMBUKUMBU HII! KWENYE SEHEMU INAYOFUATA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU