SHEM MI NATAKA (19)

SEHEMU YA 19

TULIISHIA HAPA
Binti alimshika shavuni kisha akafungua pochi na kutoa kitita cha pesa na kumpatia

“We!” Mandi alishangaa

“Za nini hivi?” aliuliza

“Lipia hapa hospitali itabaki nauli, nenda kwenu kajitibu halafu utanitafuta” binti alisema huku alimuandikia namba ya simu kwenye kikaratasi na kumkabidhi

“Umezipata wapi pesa hizi?” aliuliza Mandi ila binti alinyanyua pochi yake na kuondoka akiwa analia

ENDELEA NA KUMBUKUMBU
Mandi hakuamini alizihesabu zile pesa zilikuwa shilingi milioni moja na laki mbili na elfu hamsini (1250000) taslimu.

Aliruka kitandani maana mguu ulikuwa,umeshapona japo alichechemea kwa mbali, alifurahi sana bila kujua zimepatikana vipi

**
Kesho yake Mandi alitoka hospitali huku akimshukuru sana Husna.


Ilipita kipindi cha siku tatu Mandi hakupata taarifa ya wapi Husna alipo, ndipo akapata wasiwasi kwamba binti amepata matatizo

“Naomba simu nimpigie” aliniambia Vidax ambaye pia alikuwa kando yake kwa kipindi hicho

“Poa”

Mandi aliandika namba ya Husna kwenye simu ya Vidax Rasi halafu akampigia na alipokea binti

“Hallo nani?”

“Mi Mandi uko wapi mbona hauji kunitazama?”

“Mandiiiii…..niko Tanga nyumbani”

“Tanga??? Umeondoka lini na kuna nini?” aliuliza Mandi


“Nimekuja kupumzika, naamini umeshatoka hospitalini”

“Nimeshatoka nashukuru sana sana sana rafiki yangu”

“Hayaa” Husna alisema na kukata simu yake


Siku tatu tena zilipita ndipo Mandi akapata taarifa kuhusu pesa alizopewa na na Husna

Ilikuwa ni baada ya binti kuona mateso anayopitia Mandi na hana hata mtu yeyote wa kumsaidia, Husna alihangaika kule na huku kutafuta pesa ya kumtibu rafiki yake aliyeumia kwa ajili yake.

Husna aliona haina haja ya kuwa na vitu ambavyo havitengenezi uhai ndipo akaamua kuuza mashine yake ya kutengeneza juisi ya miwa pamoja na siku kitanda na godoro akapata shili milioni na laki 1, alipojumlisha ile laki tatu aliyokuwa ameweka kwa ajili ya kodi ilifika Tsh 1,400,000/=

Alitoa laki moja na nusu halafu milioni na laki mbili na nusu alimpa Mandi

Siku 1 moja baadaye binti alisafiri na kwenda kwao huku akiiua biashara yake kabisa

Huwezi amini baada ya Mandi kupata taarifa hii alilia sana, tena hakuamini. Alimtumia ujumbe
“Kwanini umefanya haya kwa ajili yangu Husna?”

Husna akajibu “Nimefanya hivi kwa sababu tu niliona changamoto unazopitia, hata sasa najua huna kazi, naomba urudi kwenu halafu Baada ya muda nitawasiliana na wewe”

Mandi hakuamini, na alitii bila shuruti,
Baada ya siku moja alirudi Singida kwao.

*
Baada tu ya kupona kabisa Husna alimuita Mandi Tanga kwenda kufanya uvuvi na Mandi alipofika tu alimkuta binti akiishi katika nyumba ile ambayo haina umeme bila kulipia.

Kitendo cha kuishi pamoja kikazaa mapenzi ndipo mandi akamfua binti usiku mmoka na kumkumbatia

“Mandi unataka kufanya nini?” Alisema Husna akiwa amekumbtiwa wamesimama katikati ya chumba

“Kwa wema wote uliowahi kunitendea nimejikuta nakupenda sana Husna, ninajua unalijua hili na natamani iwe hivyo, naomba tuwe wapenzi” alisema Mandi

“Wewe!!!” Binti aliita kwa mshtuko akimtazama usoni “Kweli?”

“Ndio, nakupenda sana” alisema Mandi mara binti akaanza kulia


“Usinipende Mandi, mi nina matatizo”

“Matatizo gani?”


“Mandi mi siwezi kuzaa, hata ukinioa sitoweza kukuzalia mtoto” alisema binti lakini mandi hakuwaza kabisa


“Hilo tu? Nakuahidi nitakuwa na wewe hivyo hivyo duniani tunapita”

“Kweli Mandi?” aliuliza binti

“Ndio”

“Kweli?” aliuliza tena

“Ndio”

“Please Mandi usinisaliti, pia nakupenda”

Mandi hakujibu chochote alilifungua gauni la binti na kulitiririsha mgongoni ndipo likadondoka chini na kubaki na nguo ya ndani pamoja na shanga zilizojaa kiunoni.

Mandi alizitazama shanga hakuwahi kuziona kabla, hakuhangaika nazo, alimbeba binti na kumrusha kwenye godoro akamvua nguo iliyobaki akaanza kumtandika.

Baada ya kutandikana ndipo binti akawa anamfundisha namna ya kuchezea shanga, ghafla bin voo Mandi akazikata zote baada ya kuzivuta kwa nguvu sana


*
Kumbukumbu hiyo iliishia pale mandi alipofuta machozi na kumuita mkewe huku bado akiwa ameshika shanga mkononi

“Husnaaa mke wangu” alisema

“Abeee” aliitika

“Njoo mara moja”

Husna alisonya kidogo na kumtazama Sadiki aliyekuwa ameketi wanaonyeshana ishara. Aliondoka na kuingia chumbani ambapo alimkuta mumewe akiwa ameshikilia shanga iliyokatwa mkononi

Husna alishtuka sana baada ya kuona mumewe akiwa na shanga, akahisi ameshtukiwa mchezo wake na Diki

“Mume wangu kuna nini?” aliuliza binti

Mandi hakujibu chochote la, alipiga magoti chini taratibu na kuanza kuongea
“Mke wangu naomba unisamehe nimekukosea mara nyingi sana, nimeshindwa kukuthamini lakini nina uhakika tumetoka mbali sana naomba unisamehe nakuahidi kuirudisha furaha yako tena” alisema

“Nini tena?” aliuliza binti kwa uoga hakumuelewa kumbe mwenzake amekumbuka mengi sana

“Nisamehe mimi” alisema kwa uchungu

“Nimekusamehe inuka basi?” alisema Husna

Mandi aliinuka na kumtazama mkewe amejawa na uoga kupitiliza lakini Mandi kwa mara ya kwanza alimvamia mkewe na kumnasa ulimi akaanza kuunyonya

Ilichukua dakika mbili kuamini lile tukio, ndipo Husna akarudi nyuma na kumtazama “Ni wewe kweli?” alimuuliza

“Ndiyo mke wangu”

“Haya twende ukale”
*
Kesho yake Sadiki alienda kwenye interview ya pili
****

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!