SEHEMU YA 21
TULIPOISHIA
Husna alizidiwa akaamua kwenda hospitalini ili kujua kinachomsibu ni nini, alipofika alipimwa vizuri ila kuna taarifa iliyomshtua sana.
“Unasemaje Dokta????” aliuliza binti
ENDELEA NAYO
“Ndivyo ilivyo hivyo madam” Daktari alisema
“Pima tena, haiwezi ikawa kweli” alisema binti
“Mh haya”
Husna alichukua mkojo akampa daktari mwingine tena na kwenda kupimwa, huwezi amini hakuamini kile alichosikia, kwa mara ya kwanza baada ya binti kusota kwa muda mrefu sana aligundua kwamba ana ujauzito wa mwezi mmoja kasoro
“Eeh?” alisema binti
“Una mimba?”
“Doctor!!! Mi mbona niliambiwa sina uwezo wa kushika mimba?” alimuuliza
“Nani alikuambia” aliuliza doctor
“Babu yangu” binti alisema huku machozi yakimlenga lenga
“Ni daktari?”
“Hapana, ni mzee wa mitishamba”
“Ahahaha, alikudanganya, anyway sifahamu ila ndio hivyo”
“Asante doctor”
Husna hakuamini aliondoka hospitali na kufika nyumbani ila sasa hakuwa na kitu chochote cha kula pale nyumbani.
Alichukua simu yake na kumpigia mzee aliyekuwa amempa ile nyumba aliyokuwa akiishi
“Shikamoo mzee Banga” alisalimia
“Marahaba habari yako”
“Salama, samahani”
“Bila samahani”
“Nataka kurudi nyumbani sasa, hivyo nimekupigia ili nikutaarifu hilo”
“Lini?”
“Leo leo”
“Sawa….nitakuja”
“Nashukuru”
Husna alikata simu haamini kile alichokuwa amekisikia hospitalini, ni miaka mingi sana amesofa bila kufanikiwa kupata mimba, alilia kilio cha furaha lakini pia moyoni alijua kabisa Sadiki ndo amehusika pale
“Asante sana Sadiki ninajua hii ni ya kwako, ulijua kunipatia” alijisemea huku akifuta machozi.
Alimtumia ujumbe
“SHEM NIMESHAACHANA NA KAKA YAKO, ALIENDA KUISHI NA MWANAMKE MWINGINE AMBAYE ANA MTOTO NAYE, NINASHUKURU SANA SHEMEJI YANGU KWA KUNISAIDIA MIMI UMENIPA MIMBA, NAKUAHIDI SITOITOA, SITOKUDAI CHOCHOTE NA NITAMLINDA MTOTO WAKO, ASANTE UMENITOA AIBU NA NIKUTAKIE MAISHA MEMA, MIMI HUSNA” alituma binti
Sadiki aliitazama message hakuamini akajikuta anashangaa
“Kivipi? Mbona alisema hashiki mimba? Ananitania” alisema na kumpigia
“Hallo” Husna alisema baada ya kupokea
“Hallo, mbona sikuelewi?”
“Siamini shemeji, nimeenda hospitali nina mimba ya wiki tatu, najua hii ni ya kwako, nashukuru sana”
“Uko serious?”
“Kabisa”
“Sawa, sasa ilikuwaje broo hakukupa mimba kipindi chote hicho??”
“Mi sijui tatizo”
“Ok kila la kheri, na hongera kwako” Sadiki alisema na kukata simu
Alibaki na mawazo afanyeje? Ni kweli alifurahia penzi la Husna ila haitafaa kuwa naye kama mke maana atakuwa amempora kaka yake
Pia aliwaza “Broo hajampa mimba mkewe kwanini? Au hana uwezo wa kumzalisha mwanamke? Hivyo basi kama ndivyo basi hata yule mtoto aliyezaa na mwanamke mwingine anaweza akawa sio wa kwake”
*
Baadaye Mzee Banga alifika kwa Husna na alikabidhiwa nyumba, Husna alipakia vitu vyake na kurudi kwao Kabuku kwa wazazi ili akailelee mimba yake, kwa raha.
Alifika salama
*
Kesho yake, Sadiki hana hili wala lile, akapokea taarifa kutoka A & B Company Limited, kwamba amepata kazi na anatakiwa afike ofisini tarehe 15 mwezi wa kwanza ili kuanza internship kwa siku kumi na tano na tarehe 1 mwezi wa pili ataanza kazi rasmi kwa mshahara wa shilingi laki 7 na elfu 50.
Alibaki njiapanda, akamtafuta kaka yake lakini hakupatikana. Aliamua kumpigia Chiku ampokee, na ikawa hivyo
Alipata pa kukaa mpaka atakapojiweza kiuchumi ila sasa imebidi awe na Chiku kimapenzi kwani hakuwa na chaguo lingine.
JE UNGEMSHAURI NINI SADIKI?
JE UNGEMSHAURI NINI HUSNA?
JE UNGEMSHAURI NINI MANDI?
MWISHO WA HADITHI
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU