EP 01
Ungelikuwa wewe ungewezakweli? Kwa hayo aliyoyafanya Bligita nakuuliza tena ungeweza? Ilikuwa ni ngumu, swali hilo ni kwa wanaume wote. Basi ungana na mimi ili nikujaze taarifa na mwishowe unipe majibu yako kama ungeweza au lah!Mimba! Lingeweza kuongeleka kama ni suala jepesi mno kupatikana kama ungekuwa ukisiliza taarifa ya wanafunzi wengi walioacha shule kwasababu ya mimba. Amini nakuambia kwa wengine ilikuwa ni kazi, bila Mungu kusimama kati basi hata hizo ndoa zisingekuwepo kabisa, zingesambaratika au kutoweka kwa amani kutokana na masimango au kuchepuka.
Wamfue Kilacha, alikuwa ni mmoja kati ya wanandoa na mkewe Bligita waliopitia changamoto hiyo ya kuchelewa kupata mtoto. Iliwachukua takribani miaka kumi ndipo tumbo la Bligita lilipobeba ujauzito, hakika ilikuwa ni furaha kubwa kwa Wamfue aliyetamani kutangaza dunia nzima ju ya ujio wa mwanaye mpya, eti kuna watu wanachagua watoto! Unachagua aina ya mtoto? Pengine ni kwasababu una uwezo na matarajio ya kuwapata wengindio maana.
Wamfue alikuwa tayari kumfanyia chochote mkewe kwa jinsi alivyo na furaha. Kazi zake, akili yake, vyote vilikwenda vizuri kutokana na furaha aliyokuwa nayo ya kuja kuitwa baba miezi kadhaa mbeleni.
Ooh! Mimba, huja na changamoto nyingi sana, kila mmoja na aina yake. Bligita alianza kuwa na tabia ambazo hakuwahi kuzionyesha hapo awali kwa mumewe. Wamfue alipevuka na kutambua hizo ni changamoto za Mimba hivyo hakukasirika wala kumbeza mkewe.
“Namtaka mdogo wangu, naomba uniletee mdogo wangu sasa hivi…” lilikuwa ni agizo alilolitoa Bligita, ungeweza kudhani alitania, mpaka machozi aliyatoa,
“Nakuletea mke wangu ila tambua yuko mkoa mwingine…”
“Namtaka, nisikuone hapa nyumbani kama hujaja naye…toka! Mpuuzi mmoja wewe!”
“Sawa.” Alijibu kwa upole Wamfue na kutoka nje, ndio alikuwa akielekea kazini muda huo na alilala sebuleni usiku wake, Bligita hakumtaka kabisa kitandani.
Basi alianza kuongea na mdogo wa Biligita ambaye ni shemeji yake, huyo aliitwa Salome. Ilikuwa ni ngumu kwasababu alikuwa akifanya biashara pamoja na rafiki yake tena mkoa mwingine. Alimbembeleza mpaka Salome alianza kumuonea huruma shemeji yake, basi walipanga angekuja baada ya kuweka mambo yake sawa.
Siku tatu mfululizo Wamfue alilala nje ya nyumba yake, ndani mkewe alikuwa akilia tu akimtaka mdogo wake, alitishia mpaka kujiua kama mdogo wake asipokuja. Ilibidi Wamfue amuombe jirani yake mama Tuche, huyo alifunguliwa mlango na Bligita na alikuwa akimuangalia kwa karibu maana sio kwa vitisho vile. “Mungu, nitavumilia kwa kila jambo, nilikuomba kwa muda mrefu na umenipa, siwezi kukuomba kingine tena zaidi ya kukushukuru kwa yote, ninakuhakikishia kuwa nayafurahia, kwenye filamu, sitakuangusha, nitaimudu vizuri haya matukio uliyonipangia na mke wangu.” Moyoni
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU