SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? (02)

EP 02
 
alijisemea Wamfue akiwa nje ya nyumba, alinunua shuka la kimasai ambalo ndilo lilimsaidia asipigwe na baridi. Katika siku tatu hizo, alishukuru Mungu mvua haikumnyeshea.
Salome alifika majira ya usiku na kumkuta Wamfue nje ya nyumba akiwa na rafiki yake Mansuli, alimpokea vizuri ambapo Bligita aliposikia tu sauti ya mdogo wake alikurupuka ndani na kwenda kumkumbatia akimsukuma mumewe, alilia kabisa, hakuwahi kuwa na mapenzi ya aina hiyo kwa mdogo wake hapo awali.
Alimshika mkono na kuingia naye ndani, akafunga mlango kitu ambacho Wamfue kilimuacha hoi mno maana alihisi ujio wa Salome ndio mwisho wake wa kulala nje,
“Kaka lakini tuachane na hayo kwanza…huyu ni mdogo wake na mkeo?” alihoji Mansuli
“Ndiyo, kwani vipi,”
“Wa moto! Kaka niunganishe name nipate jiko, angalia lile umbo, mtoto kama anaaka kuwa mwembamba lakini makalio yanamkataa, yaani aina ile ya wanawake ndio unakula mpaka unakombeleza kabisa,”
“Yaani Mansuli akili zako za ajabu sana, badala ya kunisaidia ndugu yako wewe ushaanza kumtamani Salome na umemuona leo tu…”
“Haya sawa, usijali, tutamtumia mdogo wake kumshawishi, usiku huu utaingia ndani,” alipomaliza tu kusema hivyo Salome alifungua mlango kisha akamuita Wamfue,
“Shem Waa! Njoo…”
“Ee bwana ee! Shem Waa, njoo…” Mansuli aliigia sauti ya Salome akijishebedua kama mwanamke tena kwa mapozi hasa na kumfanya Wamfue abaki akicheka tu
“Kaka! Huyu mtoto ni wa moto, kuwa naye makini, kile kipini puani kisikufanye uharibu ndoa maana sisi wanaume ni nguruwe pori tuliochangamka,”
“Nguruwe pori mwenyewe na wenye tamaa wenzako.” Walipoongea hivyo waligawana njia, Wamfue aliingia ndani baada ya siku tatu kupita huku rafiki yake Mansuli akienda nyumbani kwake, alikuwa ni mfanyakazi mwenzake, marafiki wa Wamfue ndio kabisa hawakutakiwa na Bligita hapo ndani hata harufu zao.

Salome alishangazwa na namna Bligita alivyompenda kupitiliza. Alimjali, alimpikia na kutaka kumlisha kabisa, kuna muda Salome alishindwa kujizuia na kucheka, Bligita alilia kwa kuchekwa, “Unanicheka kwasababu nakupenda, sawa tu…” alilalamika hivyo ambapo Salome alipombeleza alihisi raha kweli.
Muda wa kulala ulipofika alimng’ang’ania na kwenda kulala naye chumbani ambapo huwa analala na mumewe. Walipofika huko walijiachia kama wanawake, Salome ndani ya nguo ya ndani tena ya kizungu alivalia na kupanda kitandani, Bligita naye alivalia gauni la kulalia ambapo ndani yake hakuvalia chochote. Walijifunika shuka moja, huku Mwenzangu na mimi Wamfue alikuwa amelala chumba cha wageni alichotakiwa kulala Salome maana walikuwa na vyumba viwili.
Akiwa amevalia pensi yake baada ya kutoka kuoga alipanda kitandani na kumtumia   ujumbe   mke   wake

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!