SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? (10)

EP 10

kuliko wanaume, haimaanishi kuwa wote wanaolia huhisi raha, wengine huwaaminisha wanaume wao kuwa wanawamudu.
Salome alikwenda kulala chumbani kwa dada yake huku Wamfue akilala chumba cha wageni. Mchezo huo uliendelea ambapo Salome ule muda mfupi aliopanga kukaa hapo kwa dada yake aliongeza. Alionja tabu alizokuwa akizipata shemeji yake hivyo alimuonea huruma, mbali na hivyo alipewa onyo na dada yake kuwa angethubutu kuondoka na yeye angejiua, ilibidi kusubiri mpaka wakati wa kujifungua.
Vituko hakuishiwa Bligita, kuna siku akiamka asubuhi, basi huwaomba msamaha Salome na Wamfue mpaka machozi, hizo zilikuwa ni siku ambazo na yeye Wamfue alionyesha umwamba, alijifanya kutomsamehe japo kosa halikuwepo, Bligita machozi hayakukauka. Kuna siku alikusanya viatu mpaka vya majirani kisa akanusa tu.
Kwa siku ambazo hucharuka basi tabu kubwa humpata Wamfue, Salome alikuwa katika sehemu salama, kitu chochote kikienda tofauti basi Wamfue ndio  alisababisha  kwa  jinsi  Bligita alivyokuwa akiwaza.
Siku moja asubuhi aliamka na wazo la uke wenza. Alimuambia Wamfue atafute mke mwenzake, anataka wawe wawili kwake, mwanzoni Wamfue alichukulia kawaida ila aliporudi nyumbani siku hiyo alioagizwa bila mwanamke alilala nje mpaka asubuhi maana alifunga mlango na funguo aliondoka nayo.
Wamfue ilibidi kumuomba mfanyakazi mwenziye aigize kama ndio mke wake, si akaenda naye nyumbani kwa kutegemea ataruhusiwa kulala ndani. huyo mfanyakazi mwenzake na Wamfue alitimuliwa akichapwa bakora za mgongoni mpaka aibu,
“Kumbe wewe ndio unachepuka na mume wangu, eti unajiamini kabisa kuja nyumbani kwangu na kujitambulisha ni mke Mwenzangu, una kichaa ee?” aligeuza kibao siku hiyo Bligita na likaonekana kosa lilikuwa ni la Wamfue.
Kwa kutumia ujanja Salome alichomoa ufunguo mmoja wa mlango huo wa kuingilia ndani, alipoufunga basi yeye baadaye alimfungulia na kulala kwenye chumba cha wageni. Tabu ya kulala nje hata akifungiwa iliisha kwa mtindo huo.
Ujauzito ulikua, miezi saba ulikimbilia, kwa miezi waliyovumilia, safari ilibaki umbali mfupi ili mateso yaishe. Wamfue kuna baadhi ya vitu alivichukua kama ukumbusho na kuvihifadhi kwenye simu ili siku hali hiyo itakapoisha amuonyeshe mkewe jinsi alivyokuwa akimtesa.
Mchana mmoja siku ya jumapili, Bligita akiwa amelala, Salome alikuwa na Wamfue sebuleni,
“Rafiki yako ananitongoza, nimkubalie?”
“Rafiki yangu nani?” “Mansuli,”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!