SHEMEJI UMECHOMEKA KWELI? (11)

EP 11

“Ni wewe tu, kama umempenda mkubalie,”
“Nataka nimkubalie, hana tabia chafu kama zangu?”
“Anazo kidogo ila akikupata atatulia, sio kwa utamu ulionao,” “Shenzi!”
“Na yule Murama mpenzi wako utamuachia nani?”
“Hivyo ee? Ona sasa nilishaanza kumsahau,”
“Kichwa kama kuku…” walitaniana mtu na shemeji yake wakijiachia hapo sebuleni,
Ghafla alikuja Bligita waliyemdhania kuwa alikuwa usingizini. Ni kama alivyolala huo muda mfupi, aliota aking’twa na nyuki maana mdomo ulitangulia mbele akiwa amenuna, kisirani kiliongeza mkataba mpya kwenye moyo wake.
Aliketi hapo sebuleni huku tumbo likitangulia mbele, alichukua rimoti kisha akaweka muziki, akamuinua mumewe na kumtaka acheze muziki tena akatike, alikuwa na huo ujanja Wamfue wa kukataa? Alilijua balaa lake kama angekataa.
Mbavu za Salome ndizo zilipata shida, Wamfue mwenyewe hakujua kucheza muziki, alikata mauno na kuonekana kama katuni. Wakati Salome akiwa anacheka Bligita alilia kwamba asimcheke mumewe, alito amachozi kabisa, alikuwa na hisia za karibu mno Bligita.
“Twende mume wangu, twende chumbani,”
“Sawa.”
Bligita aliyekuja na kisirani sebuleni alisema hivyo kisha alimchukua mumewe, waliongozana mpaka chumbani. Bligita mpaka soga za maisha aliongea na mumewe, jina la mtoto na maandalizi ya vifaa vya kujifungulia pamoja na mtoto wao ajaye.
Huku upande wa Mansuli, alionyesha nia ya dhati ya kumuoa kabisa Salome. Walianzisha mahusiano taratibu ambapo Mansuli ndiye aliyekuwa wa moto sana kwenye mapenzi hayo.
Kabla hata hajamuoa alianza kumwelekeza vitu ambavyo hakuvipenda, kipini puani, vikuku miguuni, kwavile vinavuka na asipovalia hawezi kupatwa na madhara, Mansuli alimuomba aviache, hiyo ikawa ngumu kwa  Salome  maana  alipenda  sana. vikuku na kipini. Vitu vidogo viliwafanya washindwane kabla hata y akufika mbali. Huku upande wa pili Bligita alifanikiwa kujifungua, alikuwa ni mtoto wa kiume. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa wawili hao waliosumbuka kupata mtoto.
Bligita aliporuhusiwa kuja nyumbani, baada ya kutumikia wiki hapo nyumbani akila vyakula vya uzazi, zile tabia zake za awali zilipungua mno. Aliwaomba msamaha Salome na Wamfue, alimpenda sana mume wake, tena sana, kupita maelezo.
Walisameheana zikichukuliwa zilikuwa ni changamoto za ujauzito. Wamfue alimuonyesha video za baadhi ya siku alizokuwa akimfokea na kumfukuza. Wote walibaki wakicheka tu.
Salome kilichoendelea kati yake na shemeji yake hakikuendelea tena, walikubaliana hivyo na Bligita hakujua chochote kilichoendelea, ilibaki kuwa siri baina yao.
Baada ya miezi mitatu, Salome aliondoka huku akipewa kiasi cha laki tano fedha za kitanzania ili imsaidie
  mbele ya safari maana walipomuita walimtoa kwenye kazi aliyokuwa akiingiza kipato, walitumia ubinadamu tu kulipa fadhila.
 

MWISHO

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!