
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA TATU: Huyo ni mkulugenzi wa idara ya uchunguzi na usalama wa siri wa nchi, mkoa wa Ruvuma, ambae kwa wanao mfahamu, huyu ndie mzee Haule, mala nyingi ujiita James bond, (soma kiapo cha damu, mrembo kipofu na mwalimu anataka)…ENDELEA……
“ndiyo mkulugenzi, itatekelezwa kwa usalama wa taifa letu” walisema wale watu wote mle ndani, huku wakimtazama mkulugenzi haule, au baba Eric, au James bond.****
Naaaaaaam!, miezi miwili na week mbili baadae, saa sita usiku, ndani ya mji huu wa Songea ambao ulikuwa kimya, giza zito lilikuwa limetanda, manyunyu ya mvua yalikuwa yanatililika toka angani na kutuwa ardhini, yakijaza maji kwenye sakafu ya dunia, nakutengeneza vidimbwi vidogo vidogo.
Upande wa kaskazini wa mji huu wa songea, hapo tuna zungumzia maeneo ya msamala, barabara kuu, ambako usiku huu hapakuwa na pilika ya aina yoyote ya kibanadamu, ambayo ilionekana wazi, hapakuwa na gari wala boda boda iliyoonekana ikipita barabarani.
Lakini katika utulivu huo huo, tuna yaona magari matatu, mawili yakiwa ni toyota land cruiser na moja likiwa ni range rover, yote yakiwa na rangi nyeus, yakiwa yana tililika kwa speed kali, katika barabara kuu iendayo mikoa ya Iringa na Mbeya, likitokea upande wa mjini kuelekea upande wa daraja la mto luhuhila.
Dakika chache baadae magari yana simama mita chache toja darajani, kisha wanashuka vijana wanne wenye mmili iliyo jengeka kimazoezi, toka kwenye magari mawili aina toyota land cruiser, baadhi yao wakiwa na bastora mikononi mwao, huku mmoja akiwa na mikono mitupu.
Lakini kwenye gari aina ya range rover wakishuka watu wawili tu, kijana mmoja alie jengeka mwili kimazoezi, alieshikilia mwamvuri akimkinga mvua mwanaume mtu mzima, mwenye mkadilio wa miaka 48, alie valia suit nyeusi, mkononi akiwa ameshikilia bakora moja nzuri ya kutembelea, yenye mng’ao wa dhahabu.
Kijana asie na bastora anazunguka nyuma ya gari moja kati ya toyota mbili, anafungua buti, ambako anaonekana mtu mmoja alie tapakaa damu mwili mzima, na uso ulio chakaa kwa kipigo, kiasi cha macho yake kushindwa kuonekana, kutokana na kuvimba kwa kipigo.
Yule jamaa anamvuta kwa nguvu na kusababisha yule alie chakaa, aanguke chini, kama furushi lisilo na thamani, kisha anaanza kumvuta kumsogeza mbele ya mwanaume mtu mzima alie valia suit nyeusi.
“hivi wewe ulikuja kuomba kazi kwaajili ya shida zako, au kutongoza wanawake wasio kuhusu?” anasema yule mwanaume mtu mzima, huku anaingiza mkono wake wa kushoto ndani ya mfuko wa ndani wa koti la suit, na kutoa kikasha chenye sigara.
Ni kama vile yule jamaa alie chakazwa kwa kipigo, anatamani kusema kitu, lakini anashindwa kutokana na hali ya maumivu aliyokuwa nayo, “yani unawaona mwanawake anapendeza, alafu wewe unatongoza, unazani amejipendezesha mwenyewe yule mwanamke?” anauliza mwanaume mtu mzima, huku anaweka sigara mdomoni.
Hapo kijana mmoja anamsogelea mzee huyu kwa haraka, huku anatoa kibiriti mfukoni, na kumsaidia kuwasha sigara yake, “jibu wewe, boss anakuuliza alafu unaleta kiburi” alisema kijana mmoja, huku anamzibua teke mwanaume huyu, aliekuwa amelala chini, pasipo kuweza kujisaidia mwenyewe, akishiwa ata kutoa sauti ya kuugulia maumivu.
Mwanaume mtu mzima anavuta mkupuo mmoja wa sigara yake, kisha ana utoa moshi mwingi, kwa kutumia pua na mdomo wake, kisha anawatazama vijana wake, “Jomo, naona huyu fala analeta kiburi, ebu angalia chakufanya ilikuweza kusafisha uchafu huu” alisema mwanaume mtu mzima.
“ndiyo kuu” anasema yule kijana alie mleta huyu jamaa alie chakazwa, huku haraka sana, anazunguka nyuma ya gari la pili, ambapo dakika chache anarudi akiwa ameshikilia msumeno wa nyororo, unao tumia mafuta petrol, kwa jina la kigeni, unaitwa Chain Saw.
Anaiwasha ile mashine ya kukatia mbao, ambayo inawaka mala moja, na kumsogelea yule jamaa, ambae ni wazi kabisa siyo alikuwa amepigwa sana hapo mwanzo, maana alishindwa ata kutamka neno, ata alipojaribu kuinua mkono, alishindwa.
Katika hali ya uchungu mkubwa sana, anashuhudia msumeno wa nyororo, ukigusa kwenye goti lake, na kuanza kuchimba nyama za goti, na kupasua mfupa, hukichimba kwanguvu na kurusha damu na vipande vya nyama na mfupa.
Hapo licha ya kushindwa kutoa ata kelele za kujitetea, lakini safari hii alijikuta anapiga kelele za uchungu mkubwa sana, “mamaaaaaaaa” alipiga kelele mwanaume huyu, ambae unaweza ukashindwa kutambua kama ni mtu mzima au kijana.
Kelele za uchungu anazo zitoa mwanaume huyu, licha ya kutia huruma, lakini kwa hakika upande wa watu hawa, wenye roho ngumu, ilikuwa ni furaha na kichekesho, maana walionekana wakianza kucheka kwa furaha.
Kazi aikusimama mpaka mguu ulipo tenganishwa, na kuamia mguu mwingine, kisha mkono, yani mpaka walipo hakikisha wamemtenganisha sehemu zote za mwili, na huyu jamaa kukata roho, katika maumivu makali….. duh!, hii nizaidi ya hatari, ebu tusubiri mengo juu ya awa watu wenye roho ngumu. endelea kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa kwa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU