
TOBO LA PANYA (06)

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Alikuwa ni kijana mtulivu na mpole, mwenye makadilio wa umri wa mioaka ishilini, alievalia suruali ya jinsi la blue, iliyo pauka, tishert jeusi lililochakaa kidogo, na raba nyeusi miguuni mwake, ambayo pia ilikuwa imeshaanza kuchakaa, aliekuwa amesimama peke yake, anatazama mchezo wa mpira wakikapu……endelea…..
“ngoja ni mtume huyu dogo” alisema Anastansia, huku anaanza kutembea taratibu, kumfwata kijana huyu, ambae kiukweli akuwa mgeni machoni pake, japo hakuwa amezoweana nae, sababu kijana huyu ambae siyo mwanafunzi, ameanza kumwona toka mwaka jana, kabla ya likizo ya mwezi wakumi nambili, akiwa anakuja kutazama mpira hapa chuoni.
Ni kijana mtulivu, pia naweza kusema ni kijana ambae pekee ndie ambae, auwezi kuona akimtazama kwa matanio, utazama mala moja kisha angeendelea na hamsini zake, ila pia ni kijana ambae licha ya kujitaidi kwa usafi wa nguo na mwili, ila alionekana wazi kutokea katika mazingira duni ya kimaisha.
Anastansia anapiga hatua kadhaa, huku akisindiklizwa na macho ya watu, mpaka alipofika pale alipo simama yule kijana, ambae leo anaamini kuwa ndie msaada wake, anapo mfikia anagusa bega, “ujambo dogo” anasalimia Anastansia, kwa sauti yake nzuri tamu na nyororo, ikiwa katika utulivu na upole.
Kijana mdogo anageuza uso wake tulivu, na kumtazama mtu alie mgusa bega lake, macho yake yanakutana na Anastansia, kijana anaachia tabasamu afifu, Anastansia analiona tabasamu lile, ambalo limekosa uchangamfu.
Nancy anahisi unyonge moyoni mwake, kwa hali ya ukosefu wa amani, uliopo ndani ya kijana huyu, ambae licha ya nguo zake kuonekana safi, lakini zina wonekano wa uchakavu, nae anatabasamu kidogo.
“dogo naomba nikutume hapo bekari kwa masister” anasema Nancy, kwa sauti yake tamu, na tulivu, huku anamtazama kijana huyu, ambae kimwonekano, Anastansia ni mrefu zaidi ya kijana huyu, ambae upole wake umepitiliza, nakuwa unyonge.
Wakati huo kila mmoja alikuwa anawatazama, ni kama walikuwa wanataka kuona au kusikia kilichokuwa kinaongelewa na wawili wale, japo hakuna alie waza mabaya, maana hadhi ya wawili hawa ilikuwa tofauti kabisa.
“sawa” aliitikia kijana huyu mdogo, huku anakubari kwa kichwa, bila kuongeza neno, Anastansia anaanza kutembea kuelekea pembeni ya uwanja, kule ambako alisimama mwanzo, na kijana mpole akimfwata nyuma, huku wakisindikizwa na macho ya kila mmoja pale uwanjani.
“Naomba uende pale kwenye bekari ya masister, ukanichukulie chakula, ukimkuta meneja, mwambie Nancy amenituma, ata kupatia mfuko, mimi utanikuta nakusubiri kwenye lile geti dogo” alisema mwanamke huyu, mrembo ambae sauti yake sawa na nyimbo tamu, isiyo chosha kusikiliza, huku wanaendelea kutembea taratibu, kuelekea upande wamajemho ya utawara, wakiacha kabisa eneo la viwanja vya michezo.
“sawa” alijibu kijana mpole, ambae akuwa ameongea neno jingine zaidi ya “sawa” toka ameanza kuongea na Anastansia, kiasi kwamba Anastansia anakilimoyoni mwake kuwa, huyu dogo ni mpole kuliko yeye, hali ambayo ilimfanya Nance amchukulie huyu kijana kuwa, ni mtu aie athisiliwa kutokana na ugumu wa maisha anayo pitia.
Wanatembea kimya kimya mpaka kwenye makutano ya barabara nne, ile ambayo inatoka kwenye majengo ya utawara, ile inayoenda kwenye mabweni, ile inayoenda langoni, na ile inayoenda madarasani.
“naomba ujitaidi kufanya haraka, utanikuta pale getini nakusubiri” alisisitiza Nancy, wakati kila mmoja anashika njia yake, “sawa” anajibu kijana mpole, huku anaelekea upande wa lango la kutokea, huku Nancy akishika njia ya kueleka bwenini.
Nancy anatembea hatua kadhaa, huku anamtafakari kijana huyu mdogo, ambae ni tofauti kidogo na wanaume wengine, yani licha ya upole na unyonge wake, lakini pia alionekana kuwa katika hali duni ya maisha.
Nancy baada ya kutembea kidogo, anakumbuka jambo, hivyo anageuka na kumtazama kijana huyu, ambae anamwona anaendelea kutembea, bila kutazama nyuma, “tofauti na wanaume wengine” alijisemea Nancy, ambae amezowea kuwa, kila anapopishana na mwanaume, lazima angegeuka kumtazama makalio yake.
Anastansia anatembea kuelekea bwenini, akimwacha kijana wetu anatokomea nje lango la kuingilia chuo, “anatia huruma, sijuwi anaishi na nani huko kwao” alijisemea Nancy, huku anaendelea kutembea peke yake, kusogelea bweni ambalo alikuwa anaishi.*****
Naaaaaaaam!, mida hii ya jioni, kaskazini mwa mji wa Songea, maeneo ya msamala, tunaliona gari aina ya land rover miaka na kumi, mali ya jeshi la polisi, likitembea kwa speed kuelekea upande wa darajani.
Nyuma likiwa na askari wanne walio valia sale za kaki, na kofia nyeusi, wakiwa wamekumbatia silaha zao, kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine, ukiwa umeshikilia bomba.
Mbele ya gari kukiwa na watu wawili, yani dereva wagari ilo, na askari mmoja wa kike, mwenye nyota mbili mabegani mwake, zikimtambulisha mwanamke huyu, kuwa ni afisa wa jeshi la polisi, mwenye cheo cha Insp, ambae kwa mkadilio alikuwa na umri wa miaka 25.
Safari hii inaenda kukoma darajani, ambapo wanakuta kundi kubwa la watu, likishangaa kitu flani ambaco siyo cha kawaida, kilichokuwa kimefunikwa na kanga, huku kanga ikionekana kulowa damu, ni wazi yalikuwa mabaki ya mwili wa mnyama flani.
Sekunde chache baadae tayari gari lilikuwa limesha simama, na askari walikuwa wamesha shuka, wakiongozwa na yule Insp wakike, ambae alisogelea moja kwa moja kwenye kundi la watu.
Insp wakike anapokelewa na mzee mmoja wamakamo, “mheshimiwa afadhari mme fika, maana tulishindwa kufanya lolote, kama tufukie au tufanyeje” alisema yule mwanaume mtu mzima, huku anamwongoza Insp kusogelea kwenye kile kilichofunikwa.
“shikamoo mzee wangu, pole na matatizo” alisema yule Insp wakike, ambae alikuwa anatembea kusogelea kwenye kile kilicho funikwa, akiongozana na askari mwingine mwenye cheo cha koplo.
“marahaba mwanangu, tumesha poa” alisema yule mzee, huku akiongozana na Insp, ambae anaonekana kuingiwa na mashaka kila alipozidi kusogelea kile kilichofunikwa, anafika sehemu ya tukio na kufunua kidogo kile kipande cha kanga.
“mungu wangu, nini hiki nakiona” hapo inspector anajikuta anatazama pembeni kwa haraka, kukwepesha macho yake, huku anaachia ile nguo ambayo inarudi mahari pake. endelea kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

