TOBO LA PANYA (07)

SEHEMU YA SABA


ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: “mungu wangu, nini hiki nakiona” hapo inspector anajikuta anatazama pembeni kwa haraka, kukwepesha macho yake, huku anaachia ile nguo ambayo inarudi mahari pake. Endelea………

Ama kwa hakika, lilikuwa ni tukio la kutisha, maana aliweza kushuhudia vipande vya viungo vya binadamu, sambamba na kiwili wili chenye kichwa, vilivyo katwa katwa bila huruma ya aina yoyote.

Yule Insp anamgeukia yule askari mwenye cheo cha koplo, “kagueni mwili tuone kama kuna kitu chochote tunaweza kukipata, ilikumtambua marehemu, wacha mimi ningee na huyu mzee” alisema Insp, akimweleza yule askari mwenye cheo cha koplo.

“ndiyo afande” alisema yule koplo, kisha akamwita askari mmoja, na kuanza kukagua mwili wa marehemu, huku Insp wakike akimgeukia yule mzee alie mpokea.

“naitwa Insp Aisha Amry, toka makao makuu ya jeshi la polis mkoa wa Ruvuma, kitengo cha CID, ningependa kufahamu machache kuhusu tukio ili” alisema yule askari wakike, alie jitambulisha kwa jina la Aisha, ambae alipendeza kwa salre zake za kazi, ambazo zilimkaa vyema, hii ni sababu ya umbo lake zuri.

“bila shaka mheshimiwa, nipo na watu walio weza kuona kwa mala ya kwanza na kutoa taarifa pale ofisini kwetu” alisema yule mzee wamakamo, “samahani mzee unaweza kujitambulisha kidogo” alisema Insp Aisha, huku anatoa kijitabu chake cha kunakili, pamoja na karimu ya wino.

“mimi naitwa Michael Ndunguru, ni mwenyekiti wa mtaa wa msamala” alijitambulisha mzee wa makamo, “ok!, mwenyekiti, hao wengine wapo wapi?” anauliza Insp Aisha Amry, na wale vijana wanaitwa na kuanza kuhojiwa, wakieleza kuwa wakati wanafanya shughuri zao pembeni ya mtu, mala wakaona viungo vya binadamu vinaelee kwenye maji.

Baada ya mahojiano, huku tayari ukaguzi wa mwili wa marehemu ukiwa umekamilika, Insp Aisha alipewa taarifa ya uchunguzi na yule koplo, “afande, inaonekana wazi marehemu alikatwa kwa msumeno, ila pia tume bahatika kukuta kitambulisho kwenye mfuko wa suruali yake, anaitwa Loyce Komba, ni mfanyakazi wa kampuni Tino trans” alisema yule koplo.

Taarifa inamshtua kidogo Insp, “mh!, Tino Nyondo tena” alisema Insp Aisha kwa sauti ya kunong’ona, kabla ya kuamuli mwili wa marehemu na viungo vyake, vipakizwe kwenye gari na safari ya mjini kuanza mala moja.***

Naaaaaaaam!, tukirudi chuo cha ualimu, ambako kagiza kausoni kalishaanza kutanda, watu wengi walionekana wakitoka nje ya geti, huku mlinzi akiwasimamia, kwamaana aliitaji kufunga geti, iliashilia kuwa, muda wa wasio wanafunzi kuwepo mle ndani ulishaisha.

Pia tunamwona mwanadada mrembo Anastansia, akiwa amesimama mita kadhaa toka lilipo lango la kuingilia pale chuoni, macho yakiwa langoni, huku mala kwa mala anatazama saa yake ya mkononi, ambayo ilikuwa inasoma saa kumi na mbili kasoro dakika sita.

Anastania anaonekana wazi kukata tamaa, ya kijana mpole kuwai kabla geti alijafungwa, maana kwa taratibu za chuo, geti likishafungwa hakuna mtu kuingia wala kutoka, labda kwa kibari mahalumu, kwahakika angelala na njaa, maana asingweza kula chakula cha chuo.

Naaaaaam!, dakika zimebakia nne, Nancy amesha kata tamaa, anainua uso kutazana getini kama alivyoita kuwa ni mala ya mwisho, bado amwoni mtu, “sijuwi kwanini nilimwambia aende yule kijana, yupo taratibu san…” anawaza Nancy, ambae kabla ajaondoa macho getini, anamwona kijana mmpole akiingia kwa haraka langoni, huku amebeba mfuko mkubwa wakaratasi ya kaki.

“we ebu kuja hapa, kwanini wenzako wanatoka wewe unaingia” alipiga kelele mlinzi, huku anapiga hatua kumfwata kijana mpole, ambae akusimama, aliingia ndani kwa haraka, na kutazama kushoto na kulia, mpaka alipo mwona Anastansia, ambae pia alikuwa anatembea kumfwata kijana mdogo.

“samahani mlinzi, nilimtuma mimi” alisema Anastansia, huku anamfikia kijana mpole, wakati huo mlinzi nae alikuwa amesha mfikia kijana mdogo, “aya kabidhi haraka uondoke bwana” anasema mlinzi, aliewasimamia Anastansia na huyu kijana mdogo.

Mlinzi anamtazama Nancy, binti mrembo na mwenye kutoka familia yenye uwezo mkubwa kifedha, ambae kila siku uwa anamwona akipita hapa getini, kwenda kwa masister kuchukuwa chakula.

Chakula ambacho uninunua kwa gharama kubwa, ambayo kwa mlo mmoja ingefaa kula siku tatu hadi nne kwa yeye na familia yake, lakini binti anatumia kwa mlo mmoja, anaumia roho sababu kama siyo tembele lililopo uwani pale nyumbani kwake, na maindi ya liyo stawi na kukomaa vyema nje ya nyumba yake, basi familia ingelala njaa, maana hkuwa ata na shilingi moja.

“asante sana dogo” anasema Anastansia, huku anapokea mfuko wake, na kijana mdogo anaanza kuondoka, “subiri kidogo” anasema Anastansia, huku anaingiza mkono kwenye mfuko wa koti la baridi (jacket) alilovaa, na kuibuka noti ya elfu moja, ambayo alitaka kumpatia dogo, kama asante.

Lakini aikuwa bahati kwa kijana huyu mpole, “twende bwana, muda wako umiisha” alisema yule mlinzi, kwa sauti yenye hasira na jazba, huku anamvuta kwanguvu kijana pole, na kumsukimia getini.

Kijana mpole anayumba kidogo, ikibakia nusu ajigonge kwenye nguzo ya chuma ya geti, Anastansia alisha fumba macho, akiamini kuwa kijana anaenda kujigonga kwenye geti.

Kijana anasimama kwa sekunde kadhaa akimtazama yule mlinzi, kwa macho tulivu yenye tafakari, “we mlinzi, kwani huyu dogo amekukosea nini?” aliuliza Nancy kwa sauti ya ukali, iliyo onyesha kutokupendezwa na kitendo kile.

Nancy anamsogelea kijana mpole, “pole mdogo wangu, chukuwa hii” alisema Nancy akimpatia dogo ile noti ya elfu moja, wakati huo ikiitwa tenga, au kitabu, huku mlinzi akiwatazama kwa macho yaliyo jaa chuki ya hali ya juu, ungesema kuna kosa kubwa walilifanya mbele yake.

Lakini kijana mpole, apokei ile noti, ila anatazama kushoto na kulia, anawaona watu wamesimama wanawatazama, kijana mdogo anamgeukia Nancy, “asante sana, naomba uniwekee” alisema kijana mdogo, kisha akaanza kutembea kutoka nje, wakati huo kengere za kanisa la matogoro zilikuwa zina anza kusikika, sambamba na filimbi, ya kushusha bendera.

Anastansia anamtazama kijana, mdogo kwamacho ya huruma, ambae anapotelea nje, kisha anamtazama mlinzi, “umeona akichukuwa hii fedha atafaidi sana?” aliuliza Anastansia kwa sauti yenye hasira, kisha anaondoka, kurudi bwenini, akimwacha mlinzi anatazama chini kwa aibu.****

Wakati huo huo, maeneo ya Songea mjini, katikati ya mji, linaonekana gari dogo aina ya Toyota hiace, likiwa lina tembea kwa speed kali, kueleka upande wa magharibi wa mji, likileta usumbufu na kuhatarisha maisha ya watumiaji wengine wa barabara.

Sauti kubwa ya music inasikika toka ndani ya gari, ambalo lilikuwa limetawara mioshi ya bangi na sigara, wanaonekana vijana vijana sita, walio valia kimaridadi, na mavazi ya kiujana, wakati huo wakiitwa mabishow, waliokuwa wameshilikia chupa zao za pombe, huku wengie wakifuta bangi sambamba na pombe.

“Luka hee!, unauhakika Rose atakuwa amesha toka ofisini?” aliuliza mmoja kati ya vijana waliokuwepo ndani ya gari, “nilivuta waya ofisini wakasema amesha toka mapema, wacha tukamtazame nyumbani” alisema mmoja kati ya vijana wale, alie kuwa anaendesha gari ilo.

Safari inaendelea kwa speed hiyo kali mpaka gari linapo fika maeneo ya njia panda ya mshule ya misufini, gari lina punguza mwendo na kuingia upande wakulia bila tahadhari yoyote, kisha dereva anakanyaga mafuta kwafujo kuelekea majengo.

“vipi kama atakuwa na mwanaume mwingine?” anauliza kijana mwingine, swali likimlenga dereva ambae anaitwa Lukas, “yani kama nita mkuta na mjinga mwingine, nae atakiona cha moto, maana yule fara alie kuwa anajivunia kaka amesha mlambisha mchanga” alisema Lukas kwa sauti yenye majivuno na majisifu.

“huyu kama tunamkuta ndani, akuna kulemba, tuna mshugulikia wenyewe, hakuna aja ya kumweleza bro wako” alisema mwingine, kwa sauti yenye kujiamini, “hapo umeongea jambo la msingi, wakati mwingine Brother Tino inabidi atuamini kwamba nasisi tunajiweza” alisema mwingine.

Wakati huo Lukas anasimamisha gari, mbele ya nyumba moja kubwa, kisha anafungua mke wa kwenye dash board, na kutoa bastora, “msiwe na wasi wasi ninamguu wakuku hapa” alisema Luka kisha akaisundika ile bastora kiunoni, na kufungua mlango wa gari. endelea kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa kwa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!