
SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA: Wakati huo Lukas anasimamisha gari, mbele ya nyumba moja kubwa, kisha anafungua mke wa kwenye dash board, na kutoa bastora, “msiwe na wasi wasi ninamguu wakuku hapa” alisema Luka kisha akaisundika ile bastora kiunoni, na kufungua mlango wa gari. endelea
Wote wanashuka toka kwenye gari, Lukas anatembea kuingia ndani ya jengo ili kubwa, huku wenzake wakibakia nje ya gari na pombe zao mikononi.
Lukas anaingia ndani na kukutana na kolido ndefu, yenye milngo kadhaa pande zote, kwa maana ya vyumba vya wapangaji, sasa unawaona wapangaji wa kike, ambao walionekana wakiwa wamekaa nnje ya vyumba vyao, wakiendelea na shughuri mbali mbali, za mapishi, na maongezi ya hapa na pale.
Lakini wote wasitisha story, na kumtazama Lukas aliekuwa anatembea kukatiza kolidoni, huku anachupa ya pombe mkononi mwake, pasipo kutoa salamu ata kwa mtu mmoja.***
Yap! Insp Aisha sasa yupo ofisini, anamaliza kuandika taarifa ya tukio la kuokotwa kwa mwili wa marehemu Loyce Komba, ulio katwa vipande pande, nakutupwa mto luhila A.
Baada ya kumaliza kuandika tukio lile, sasa Insp Aisha Amry ana sogelea kwenye meza yam le staff room, na kuinua mkonga wa simu, kwamaana ndiyo simu zilizokuwepo wakati huo.
Anabofya namba kadhaa, kisha anaiweka mkonga sikioni, na kusikilizia sekunde kadhaa, kisha simu inaanza kuita, nayo inata mala chache, kabla aijapokelewa.
“hallow, nyumbani kwa RCO Zamoyoni, nani mwenzangu” ilikuwa ni sauti ya mama mtu mzima, “mimi Aisha Amry, shikamoo mama” alisalimia Insp Aisha, kwanamna ambayo ilionyesha wazi kuwa, alikuwa na uhakika kuwa mama huyo anamfahamu.
“hooo!, dada Aisha habari za masiku, naona umetususa siku hizi” alisikika mama mtu mzima toka upande wapili wasimu, “majukumu mama, vipi mzee yupo, maana kuna taarifa inabidi aipate” alisema Aisha, ambae amefahamiana na mama huyu, kutokana na kufanya kazi na mume wa mama huyu, katika kitengo kimoja.
“yupo, ngoja nimwite” alisema mama mtu mzima, na zikapita dakika mbili, kabla mkonga aujashika, “Insp Aisha, kunanini usiku huu?” ilikuwa ni sauti nzito yenye mikwaluzo, “afande kuna tukio la mauwaji lime ripotiwa jioni hii” alisema Insp Aisha.
“natikiwa kufanya nini sasa, kwani aikufaa uniambie kesho, au ilo ni tukio la kwanza kutokea hapa Songea?” aliuliza mwanaume mtu mzima, kwa sauti iliyo onyesha kuchukizwa.
“samahani afande, ni kwamba marehemu ni mfanya kazi wa kampuni ya Tino Nyondo, hii imekuwa inajirudia sana” alieleza Insp Aisha kwa sauti tulivu yenye tahadhari kubwa.
Lakini hii inamshtua kidogo mwanaume mtu mzima, ambae ni RCO wa mkoa wa Ruvuma, “unasema ni mfanyakazi wa Nyondo?” aliuliza kwa mshtuko RCO Zamoyoni, “ndiyo afande, ili ni tukio la tatu la mauwaji, ndani ya miezi minne, ambalo lina mhusu Nyondo kwa ukaribu” anasema Insp Aisha.
Hapo kinafwata kimya kifupi, ni kama RCO upande wapili wa simu alikuwa anajaribu kutafakari jambo lile, maana baada ya sekunde kadhaa, sauti ya kiume ya upande wapili ikasikika, “sikia Aisha, ebu funika ilo jambo, fanya kama vile, huyo mtu ajulikani alikotokea” alisema RCO Zamoyoni, kwa sauti ya kutahadharisha.
Maelekezo ambayo Insp Aisha aliyatarajia, maana imeshatokea mala kadhaa, kuzuiliwa kufwatilia kesi ambayo inamhusu bwana Augustino Nyondo, “ndiyo afande” alisema Insp Aisha, ambae tayari alikuwa amesha andika taarifa ya tukio, kwenye kitabu cha taarifa.
“hakikisha taarifa aziendi popote” alisema RCO Zamoyoni, kabla ya kukata simu, “inakela kwakweli, huyu mtu wata mlinda mpaka lini” alijisemea Insp Aisha, baada ya kuweka mkono wa simu mahari pake, kisha akafwata kitabu cha taarifa za matukio, na kuachana kurasa nzima, ya kitabu kile, ambacho alikweka kwenye mfuko wa suruali yake.
“wacha nikapumzike nyumbani, nimehoshwa na huu upuuzi” alijisemea Insp Aisha, huku anachukuwa mkoba wake wakike, na kuiweka kwapani kisha akaanaanza kutembea kuelekea nje ya ofisi.***
Naaaam!, kule majengo, ndani ya nyumba kubwa ya wapangaji, kwenye chumba kimoja, chenye ukubwa wa wastani, kilicho pambwa na vitu vizuri vya kisasa, chumba ambacho ukiingia tu unajuwa kuwa ni chumba cha mtoto wakike.
Chumba ambacho licha ya kuwa na makochi mawili tu, lakini kilikuwa na kitanda kizuri, meza ndogo iliyo jaa vidoze vya kila aina, yenye kioo cha kujitazamia, kabati dogo la nguo, pembeni ya kabati la vyombo, TV ndogo ya inch, 14, yenye deki ya mikanda mikubwa, sambamba na redio cassate nzuri ya dable deck, iliyokuwa inatoa sauti ya taratibu ya music.
Lakini mle ndani juu ya kitanda, alikuwa amejilaza mwanamke mmoja aliekuwa amevalia upande mmoja tu wakanga, alieonekana kujawa na mawazo mengi sana, kiasi kwamba, usingeweza kuzani kama anasikia sauti ya music toka kwenye ilr redio yake.
“ata kama kuna kitu nimemkosea, lakini asingeweza kuacha kuja kazini” anajisemea mwanadada huyu, ambae anaitwa Rose, “lakini alisema angekuja jana usiku, mbona ajaja, na amepotea moja kwa moja, nyumbani kwake hayupo” anaendelea kuwaza Rose, ambae alikuwa anamuwa mtu muhimu kwake.
Rose alikuwa anawaza juu ya Aloyce Komba, ambae mpenzi wake wa tangu utotoni, kwamaana walicheza pamoja tangu wakiwa watoto, mpaka walipoamua kuanzisha mausiano miezi michache iliyopita.
Kiukweli Rose alitokea kumpenda sana Aloyce, mwanaume ambae siyo tu kumfahamu toka wakiwa na miaka tisa, ila pia ni mwanaume ambae alionyesha kumpenda na kumjari toka utotoni.
Katika kipindi chote cha maisha yao toka utoto, Aloyce alisimama kama mwanaume kwa Rose, mala kadhaa alisha mpambania toka kwenye uonevu wa watoto wezao, katika hali ya urafiki Aloyce alihakikisha Rose anapata furaha ata kama yeye anapitia wakati mgumu.
Rose ambae baada ya kupata ufahamu na kujuwa jinsi Aloyce anavyo jitoa kwake, walizidisha urafiki mala dufu, huku wakishindwa kuingia katika hatua ya pili ya urafiki, ata urafiki wao ulipokoma, baada ya wazazi wa Aloyce, kuamia iringa wakitokea Songea.
Lakini miezi michache iliyopita, walikutana kwenye ofisi za kampuni ya Tino Trans, na bila kuulizana wakaingia moja kwa moja kwenye mausiano, japo wakati penzi lao likiwa linazidi kushamili na mea misiri ya mgomba kwenye mfereji wa maji.
Siku mbili zilizopita, alikuja Lukas pale ofisin, ambae ni mdogo wa mwisho wa boss Augustino Nyondo, na kumwona Rose, na kumweleza kuwa anamtaka na jioni ya siku ile, atakuja kulala hapa kwake.
“samahani boss, tayari ninamchumba wangu” hivyo ndivyo alivyo jieleza Rose, japo aikusaidia kitu, Lukas alikuja nyumbani kwa Rose mida ya jioni, ambako alimkuta Aloyce akiwa na Rose.
Lukas aliondoka akiwa amechukia sana, ata siku iliyo fuata yani jana, mida ya jioni alifika pale ofisini, alipowaona Rose na Aloyce, alionyesha chuki ya wazi kabisa, “bro unajifanya unajuwa sana kupenda siyo, kaa tayari” maneno hayo aliyatamka wazi wazi kijana Lukas, tena akionyesha chuki ya wazi kabisa.
Wawili awa walishikwa na wasi wasi, huku wakitafakari maneno ya Lukas, ambayo yalikuwa kitisho cha wazi kabisa kwa Aloyce, “Aloyce wala usimfikilie sana huyo mjinga, baadae njoo nyumbani tuongee vizuri” alisema Rose kwa sauti ya kubembeleza, akimwondoa hofu mpenzi wake.
“wala usijari, najuwa tabia za watoto au ndugu za maboss wengi, upenda kutumia vibaya, vyeo vya ndugu au baba zao” alisema Aloyce, akionyesha kupuuzia maneno ya Lukas.
Lakini toka walipo agana jioni ya jana, hawakuonana tena mpaka mida hii, na mbaya zaidi, Aloyce ata kazini leo hakuja, Rose alienda nyumbani kwa Aloyce, lakini kijana huyo akuwepo nyumbani kwake, na taarifa zilieleza kuwa, toka jana akuonekana hapo nyumbani.
“sijuwi atakuwa ameenda wapi, ndio ashindwe ata kuniambia kweli, au amekasirishwa na yale maneno ya Lukas” aliwaza Wakati anawaza hayo, mala akasikia mlango wa chumba chake ukigongwa….. endelea kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU