TOBO LA PANYA (11)

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI: Rose anafungua mlango na kuingia ndani ya ile ofisini, ambako anamkuta mama mmoja mtu mzima, alie tulia kwenye kiti chake kalamu ikiwa mkononi mwake, na kijitabu kidogo kikiwa mezani, “afadhari Rose umefika, nazani utanieleza imekuwaje kuhusu Aloyce, maana boss ameagiza afutwe kazi” alisema yule mama mtu mzima, huku anaweka kalamu mezani. . Endelea….

Rose ana inamisha kichwa chini, usowake ukiwa umejawa na udhuni ya wazi kabisa, hali ambayo inamshtua mwanamama huyu, ambae bila shaka ndie meneja wahii kampuni, ambae anapo mtazama vizuri mschana huyu, ambaae alipishana na Aloyce siku chache kuajiliwa hapa Tino Nyondo Trans, anaona machozi usoni mwake.

“Rose vipi, mbona unalia, kuna tatizo?” aliuliza mama mtu mzima, huku anamtazama Rose kwa macho ya mshangao, tahadhari na huruma, “Aloyce amepotea” alijibu Rose huku anajizuwia kuangua kilio.

Mama mtu mzima, anashtuka kidogo, anatazama pembeni, pengine anahisi kilicho mtokea kijana huyu, “amepoteaje?” anauliza kwa mshangao mama mtumzima, lakini ukizingatia vyema sauti yake, unagundua kuwa, mshangao ulikuwa bandia.

“sija mwona Aloyce, toka juzi usiku, Lukas anasema ……, haa!!! mama inauma sana” anasema Rose safari hii, akishindwa kujizuwia nakuanza kuangua kilio cha kwikwi, mama mtu mzima anashusha pumzi ndefu, akionyesha wazi amesha fahamu anachomaanisha Rose.

“nyamaza kwanza Rose, unielezee vizuri” anasema mama mtumzima, kwa sauti ya kubembeleza, “mama sina cha kukueleza, mimi nimekuja kutoa taarifa naacha kazi, siwezi kuendelea na kufanya kazi hapa” alisema Rose, japo alikuwa bado katika kilio cha kwikwi, lakini alionyesha kuwa na machungu ya hali ya juu.

Mama mtu mzima anainamisha uso wake mezani, anatulia kwa sekunde kadhaa, kabla ajainua tena na kumtazama Rose, “sikia Rose, siwezi kukulazimisha uendelee kufanya kazi hapa, ila nakushauri ufikilie kwanza, kabla ujachukuwa uamuzi, wa kuacha kazi” alisema mama mtu mzima, kwa sauti tulivu.

“mama najuwa kuwa hii kazi ni muhimu kwangu, lakini kwa iki walicho mfanyia Aloyce, siwezi kubakia hapa ata kwa siku moja, kama inashindikana kunipa stahiki zangu, basi nitazisamehe” alisema Rose, kisha akageuka na kuanza kutembea kuelekea nje ya ofisi.

Rose anafunga mlango wa ofisi, huku mama mtu mzima akibakia ametoa macho ya mshangao, Rose anatembea huku anafuta machozi kwa kitambaa chake cha mkononi, akujari watu aliopishana nao, na wala akujisumbua kusalimia na nao.

“we Rose inamaana unioni?” sauti nzito ya kiume inasemesha Rose, ambae anaitambua mala moja kuwa ni sauti ya boss wake mkubwa, yani mmiliki wa hii kampuni, kwamaana ya kwamba, huyu alikuwa ni bwana Augustino Nyondo.

Rose anasimama na kumtazama mzee huyu, alie ongozana na kijana mmoja alie jengeka kimisuri, Rose anajikuta amejawa na chuki ya hali ya juu juu ya mzee huyu, ambae ni mkatili na mwenye roho ngumu.

“samahani boss nilikuwa mbali kimazo, shikamoo” alisalimia Rose, kwa sauti yenye dalili ya kilio, huku mwana dada Rose, akijitaidi kuficha hasira na chuki aliyokuwa nayo, juu ya mzee huyu.

“kwahiyo hapa ofisini kwangu, ndiyo sehemu ya kuleta hayo mawazo yako?” anauliza mzee Tino Nyondo, pasipo kujibu au kuitikia ile salamu ya Rose, huku sauti ikiwa ya ukali yenye kukalipia.

Kitu ambacho Rose anaona kuwa hii ni dharau na kejeri ya hali ya juu, maana alimini kuwa, mzee huyu anafahamu na anausika moja kwamoja na kile kilicho mtokea Aloyce, hivyo nivyema akijiondoa sehemu hii kwa amani kabisa.

“samahani baba, najisikia vibaya naenda kupumzika” alisema Rose, huku anaanza kutembea kuelekea mapokezi, ambako kulikuwa na mlango wa kutokea nje.

Mzee Nyondo, anamtazama Rose kwa macho ya mshangao, mpaka anapotoweka usawa wamacho yake, kisha anaachia tabasamu la uchungu, maana kitendo cha Rose kuamua kuondoka akimwacha yeye amesimama, mzee Nyondo alitafsiri kuwa ni dharau na kiburi cha hali ya juu.

“binti mpuuzi sana, atanijuwa mimi ni nani” alisema mzee Nyondo kwa sauti yenye hasira kali sana, huku anageuka na kuuelekea mlango wakuingilia ofisini kwa meneja.

Wakati huo huo Hidaya alie ona tukio lile, alimuwai Rose ambae alikuwa anaelekea nje ya jengo la ofisi hii kubwa, lakini anapopiga hatua chache anamwona Rose akiwa anaufikia mlango wakutokea nje.****

Mida hii pia kule makao mkuu ya jeshi, kwenye kolido la ghorofa ya pili, wanaonekana askari wengi wakipishana katika pilika zao za kazi, wakiwa katika mavazi tofauti ya kazi na pia wapo walio vaa nguo za kiraia.

Mida hii pia ASP Ayoub Mzee pamoja na Insp Aisha, walikuwa wanatembea kwenye kolido ilo, wakizifwata ngazi za kushukia chini, safari ikiwa ni kwenda kupata chai, tayari Insp Aisha Amary, alikuwa amesha maliza kumsimulia ASP Ayoub Mzee, kile walicho kiona kule msamala, kwenye mto luhuhila, pia alimweleza kile alichoelezwa baada ya kuongea na RCO.

Lakini wakati wanakatiza usawa wa ofisi ya RCO, yani mkuu wao wakitengo, mala mlango wa ofisi hiyo ukafunguliwa na akaibuka mwanaume mtu mzima, alie valia nguo nadhifu za kiraia.

Japo hapo wote wawili wanasimama, ASP Ayoub Mzee anabana mikono yake usawa wa pindo ya suruali yake, kama vile ambavyo Insp Aisha anafanya, “shikamoo afande” anasalimia ASP Ayoub Mzee.

“marahaba amjambo, tena afadhari nime waona wote kwa pamoja” alisema yule mwanaume mtu mzima, ambae kwamajina anaitwa Zamoyoni Mpeta, ndie RCO wa mkoa wa Ruvuma, akiwa na cheo cha SP.

Hapo kila mmoja wao, akahisi nini kinataka kuongelewa na mkuu wao wakitengo, ambae sasa alikuwa anatembea kuelekea nje, nao wakimfwata, “Ayoub, kaa na Insp Amary, mwelekeze kuhusu baadhi ya mambo ambayo atakiwi kuyavalia njuga” alisema RCO Zamoyoni, huku wanaendelea kutembea kuelekea kwenye ngazi. . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!