
TOBO LA PANYA (13)

SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI: “nimekuja wapi huku” anajisemea Anastansia huku ana tazana barabara ambayo bado inampa moyo kuwa, huko mbele kuna makazi ya watu, “lakini mbonah hakuna dalili” anajisemea mwanamke huyu mrembo, huku anainua uso wake kutazama mbele, kule barabara inakoelekea. . Endelea….
“siku nyingine siendi sehemu bila kuuliza” anajisemea nancy huku anatazama mbele, umbari wa mita kama mia moja hivi, kule barabara inakoele, “mh!, mbona pale kama kuna watu” anajisemea Anastansia, ambae anaona anaona moshi unafuka toka usawa wa miti mikubwa miwili, mita chache toka barabarani.
Anastansia anaanza kutemnbea, kuelekea eneo lile, akipanga kwenda kuom,ba maji ya kunywa, maana aliamini kama kuna shughuri za kibinadamu zinaendelea, basi patakuwa na maji ya kunywa.
Anastansia akiwa anaanza kujiuliza maswali juu ya usalama wake, anazidi kusogelea eneo lile, huku anaanza kuona uhasiria wa eneo lile, ambapo analianza kuona kibanda cha udongo, chini ya miti mwili mikubwa hasiri, sambamba na sauti ya music wa taratibu, ulioimbwa kwa rugha ya kigeni.****
Naaaaam!, tukirudi mjini kule ofisini kwa bwana Tino Nyondo, tunaona msafara wa magari matatu unatoka ofisini, na kuelekea upande wa soko kuu, huku range rover likiwa katikati ya Toyota land cruiser.
Nikama mwanadada Hidaya, alikuwa anasubiri magari yale yaondoke, ndipo na yeye atoke nje ya jengo la ofisi, maana mala baada ya magari matatu ya msafara wa bwana Nyondo kutoka.
Hidaya nae akiwa na mkoba wake wa mkononi, akatoka haraka na kuelekea barabarani, ambako alipanda pikipiki ya kukodi, na kuelekea upande wa mfaranyaki., leongo la safari ilikiwa ni kufika nyumbani anakoishi Rose, ili akampatie taarifa ambayo, inaweza kumwokoa toka kwenye kifo na uzalilishaji.
Wakati Hidaya anaelekea mfaranyaki kwa Rose, huku bwana Nyondo pamoja na msafara wake, walikuwa wanakatiza maeneo ya katikati ya mji, kisha msafara unakamata uelekeo wa mateka, kupitia de lax one, na barabara ya Songea girls.
Dakika kumi baadae magari yanaingia ndani ya jengo kubwa sana la kifahari, mtaa wa mateka uindini, ambako kume jaliwa nyumba kubwa za kifahari, zinazo milikiwa na watu wenye uwezo mkubwa wakifedha.
Magari yanaingia ndani ya uzio mkubwa wajumba lile la kifahari, ambapo yanaenda kusimama mbele ya mlango wa kuingilia ndani ya jumba kubwa, huku magari mengine yakienda kusimama upande wakushoto, ambako kuna magari mengine sita ya kifahari, pamoja na Toyota hiace, ambalo uwepo wake unamaanisha kuwa, Lukas alikuwepo hapa nyumbani.
Mala baada ya range rover kusimama, haraka sana mlinzi wa Nyondo anashuka toka kwenye gari, na kufungua mlango, wa mbele upande wa abiria, “Kichondo, nisubili hapa nataka nimpe kazi Lukas ashilikiane na wakina Kubaga, wamlete Rose” alisema Nyondo, huku anashuka toka kwenye gari.
“sawa boss” anaitikia Kichondo, huku anafunga mlango wagari, na wakati boss Nyondo anatembea akiacha mlango wa kuingilia ndani na kuzunguka upande wanyuma ya nyumba, huku Kichondo anatembea kuwafwata wale vijana wengine, walioshuka kwenye magari mengine.
“vipi Kichondo, boss anamaagizo au?” aliuliza mmoja kati ya wale jamaa, ambao idadi yao kwa haraka ukiacha madereva ambao bado walikuwa kwenye magari, wanafikia sita.
“hakuna maagizo yoyote, sema boss anawatuma wakina Kubaga, wahakikishe wanamleta Rose, leo leo” alisema Kichondo, huku anaegemea moja kati ya yale magari.
“Rose ni yupi huyo?” aliuliza yule alie uliza mwanzo, “haaaaaa!, Mbwilo bwana, inamaana umesha msahau yule demu wa yule, fala tulie mkata kata juzi usiku” alisema Kichondo akimweleza yule jamaa, aliemwita Mbwilo, “ok!, tena tulimwona anatoka pale ofisini” alisema yule Mbwilo, ambae kimwonekano ni kama wenzake, alikuwa na mwili ulio jengeka kimisuri, kutokana na mazoezi mazito, pengine ya kunyanyua vitu vizito.
“yah!, kalijifanya kamekasirika, kaka leta zarau kwa boss” alisema Kichondo, ambae ni kama alikuwa amejiunga na wenzake na kuanza kupiga nao story, akimwacha boss mwenyewe aende kule nyuma, ya nyumba.***
Naaaaam!, kule seed farm, tuna mwona Anastania, ambae sasa alikuwa amebakiza mita chache kukifikia kibanda, anaweza kuona vyema eneo lile, ambalo ukiachilia kibanda ambacho kilikuwa chini ya miti mikubwa iliyo fanya kimvuri kizuri, huku nyuma ya kibanda hicho kukiwa na kichuguu kikubwa, chenye kimo cha futi zaidi kumi na urefu wa futi alobaini, upana ukiwa ni futi zipatazo kumi nane.
Pembeni kukiwa na mabanda mawili ya mifugo, ambayo ni mbuzi na kuku, huku kibanda na kichuguu, ambacho kilicho jaliwa na nyasi nyingi na miti midogo mdogo, vikiwa zimezungukwa na shamba dogo lenye mazao mchanganyiko, maindi ambayo yalikuwa yamebeba maindi vyema, karanga na mboga mboga.
Anastansia amwoni mtu yoyote pale nje, ila kwa macho ya kiuchunguzi, anagundua kuwa mwenyeji hayupo mbali, kutokana na dalili alizo ziona pale nje, kwamaana, aliona kuna jiko la kuni likiwa linafuka moshi, chini ya mti, huku juu ya jiko ilo pakiwa na redio ndogopalikuwa na maindi manne yaliyokuwa yanaendelea kuiva taratibu, kwamaana yalikuwa yana chomwa, yaliyo mtaamanisha, maana alikuwa na muda mrefu aja pata radha yake.
Pembeni ya jiko pale chini ya mti, palikuwa na kiti cha cha kipekee, kiti ambacho wengi ukiita kiti cha uvivu, ni kiti kilicho tengenezwa kwa miti, huku kikalio chake kikiwa ni kitambaa kigumu sana, kuku walikuwa wanazagaa mbele ya eneo lile, huku sauti za mbuzi zikisikika toka kwenye banda, pembeni ya ile nyumba ya udongo, lililo ezekwa kwanyasi.
Anatastania anatamani afikie kwenye kiti na kujikalisha, kwajinsi alivyokuwa amechoka, lakini anajitaidi kuwa mwenye subira, maana bado hajamfahamu mwenyeji wake ni nani, kama atakuwa mwanaume au mwanamke, mzee au kijana. . . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

