
TOBO LA PANYA (14)

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU: Anatastania anatamani afikie kwenye kiti na kujikalisha, kwajinsi alivyokuwa amechoka, lakini anajitaidi kuwa mwenye subira, maana bado hajamfahamu mwenyeji wake ni nani, kama atakuwa mwanaume au mwanamke, mzee au kijana. . . Endelea….
Na vipi roho yake, au tabia zake, anaweza kuwa mkarimu au mchoyo, mchangamfu au mpole, mwenye tamaa au mstaarabu, kwakifupi hakujuwa atapokelewaje na mwenyeji wa makazi yale, ambae ni wazi anaonekana kuwa anakaa muda, kama mlinzi wa eneo, maana palionekana kuwa na alama za mairi ya gari, ambalo lilikuwa linakuja mala kwa mala.
Anastansia anatamani kusogelea kibanda na kubisha hodi, kwenye mlango chakavu ulio tengenezwa kwa vipande vya miti ya mianzi, ambao ulikuwa umefunguliwa nusu, huku ndani kukonekana giza nene, kwakifupi hapa kuwa na tofauti kubwa na kibanda cha mganga wakienyeji.
Inampa wakati mgumu Anastansia, ambae ana anasita kuusogelea mlango wa ile nyumba ya udongo, licha ya kuona dalili zote za kuwepo wa mtu ndani yake, lakini mwokeno na utulivu wa sehemu ile inamtisha mwanadada huyu mrembo kupita maelezo.***
Nyumbani kwa bwana Nyondo nako, mambo yalikuwa mtimbwiliko, maana upande wanyuma ya nyumba hii kubwa, wanaonekana vijana sita, wakiwa pamoja na Lukas, ni wale ambao alikuwa nao jana, katika safari ya kwenda kumbaka Rose.
Wakiwa wamekaa kwenye viti vyao, wakizunguka meza moja kubwa yambao, ambayo juu yake, ilitapakaa mabakuri ya supu, ambayo walikuwa wanayafakamia, pamoja na misokoto ya bangi, iliyokuwa inawasubiri wamalize kula.
“kwahiyo demu akuleta ubishi ata kidogo?” aliuliza mmoja kati ya wale vijana, “anaanzaje kuleta ubishi mbele yangu, wakati anajuwa kilicho mtokea yule mpuuzi wake” aliongea Lukas kwa majisifu, huku wanaendelea kukula maja na mbawa za kuku.
“tatizo Ngurai anajifanya kama amjuwi Lukas, yani demu alete kiburi mala mbili” anasema kijana mwingine kati ya wale, na wakati huo huo anaibuka Augustino Nyondo, yani kaka wa Lukas.
“dogo nataka sasa hivi, mkamlete yule mala ya wako, amenikela sana, nataka nimshikishe adabu” anasema Tino Nyondo, huku anasimama pembeni ya meza ya vijana wale, na kuokota msokoto mmoja wa bangi.
“Malaya gani unamzungumzia kaka?” aliuliza Lukas kwa mshangao, huku anamtazama kaka yake, aliekuwa anawasha ile sigara bwege, “kale ka Rose, leo ameniletea dharau kubwa sana, nataka ukeshe nae kuanzia leo, mpaka utakapo niambia umemchoka, tumuulie mbali” alisema Tino Nyondo huku anaendelea kuvuta bangi.
“hapo bro umesema, tena kalinikela sana jana, mimi nakula mzigo yeye analia lia tu, kisa anamlilia yule fala wake” alisema Lukas akionekana mwenye furaha kubwa sana, zilizo tokana na taarifa aliyo ipata toka kwa kaka yake.
Tino Nyondo anavuta mikupuo kadhaa kwa kuisikilizia, kisha anawatazama wale vijana waliokuwa pamoja na Lukas, “Migenda, hakikisha mnamleta yule mwanamke, pia mambo mengine madogo madogo, hakikisheni mnayamaliza huko huko, siyo mpaka yanifikie mimi” alisema Nyondo, huku anampatia mmoja kati wale vijana kile kipisi cha bangi.
“kaka ilo halina shida, tuliongea toka jana, kwamba sasa hivi, na sisi tukiona ujinga mbele yetu tunaufagia kabisa” alisema yule alie itwa Migenda, kwa sauti ya majisifu, “nakukubari sana Migenda na vijana wako, na hii ndiyo kazi yenu ya majaribio” alisema Nyondo, huku anaanza kuondoka kurudi alikotoka, akiacha vijana wakilipuka kwa shangwe.
“hoya ebu tumalizeni kula kisha tuanze safari, huku tuna gonga mitungi” alisema Lukas kwa shangwe lisilo la kawaida, “na kweli inabidi tumalize mapema, siunajuwa leo week end ndiyo inaanza” alisema mwingine, kwasauti iliyojaa shangwe.***
Insp Aisha Amary na ASP Ayoub Mzee, sasa walikuwa wanatoka nje ya kantini hii, iliyopo pembeni ya jengo kuu la makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma.
Sasa walikuwa wamesha maliza kupata chai, “Aisha unakazi yoyote ofisini?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, “kazi gani tena, wakati kazi yenyewe nazuiliwa” alijibu Aisha kwa sauti ya kukata tamaa, basi twende zetu mjini kunakitu nataka kufwata” alisema ASP Ayoub Mzee.
“lakini siwezi kwenda kwa miguu, siunaona nipo na sale” anasema Aisha na wote wanacheka kidogo, maana unapozungumzia sale kwa Aisha, kuna mambo mawili, kwanza sivyema kutembea na sale za kazi, pasipo kuwa na jukumu, pili vali alilovaa leo la suruali na koti lake, viliushika mwili wa mwanadada huyu, kiasi cha kufanya naungo tamanishi ya mwili wa Aisha kuonekana vyema.
“we shida yako nini, tutaenda na gari langu” alisema ASP Ayoub Mzee, huku wanaanza kutembea kuelekea kwenye maegesho ya magari, “alafu wakati mwingine Aisha wewe ni CID, uwe unavaa nguo za kiraia” anasema Ayoub Mzee na wote wanacheka, “nimekuelewa afande” anajibu Aisha, na wakati huo walikuwa wamesha lifikia gari dogo aina ya Toyota crester.***
Naaaaaaam! sasa turudi seed farm, ambako tuna mkuta mwanadada Anastansia, akiwa anatazama kile kibanda kwa sekunde kadhaa, kisha kama alie ingiwa na uoga anageuka na kuanza kuondoka zake.
“karibu, mbona uondoka” Anastansia anashtuliwa na sauti ambayo siyo ngeni masikioni mwake, iliyo tokea nyuma yake, nae anageuka na kutazama alikotoka, anamwona mkaribishaji, ambae alikuwa anatoka nje ya kibanda kile.
Anastansia anajikuta anasimama huku anaachia tabasamu la matumaini, lililomfanya azidi kuwa mzuri na wakuvutia, “kweli mungu mkubwa, kumbe dogo unaishi hapa” anauliza Anastansia, huku anatembea kufwata kile kiti cha uvivu, ambacho toka mwanzo alitamani akae, kutokana na uchovu aliokuwa nao . . . . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

