TOBO LA PANYA (15)

SEHEMU YA KUMI NA TANO

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NNE: Anastansia anajikuta anasimama huku anaachia tabasamu la matumaini, lililomfanya azidi kuwa mzuri na wakuvutia, “kweli mungu mkubwa, kumbe dogo unaishi hapa” anauliza Anastansia, huku anatembea kufwata kile kiti cha uvivu, ambacho toka mwanzo alitamani akae, kutokana na uchovu aliokuwa nao. . . . Endelea….

Alikuwa ni yule kijana mdogo, ambae jioni ya jana alimtuma kwenye bekari ya masister, kwenda kumchukulia chakula, ambae alikuwa anamtazama kwa macho ya mashaka na udadisi, huku amevalia katura ya kaki, na tishert jeusi, chini alivalia kandambili chakavu kiasi, japo nguo azikuwa mpya kiivyo, ila zilikuwa na mwonekano mzuri kiasi.

“ndiyo naishi hapa” anaujibu kijana mdogo, mwenye sura ya upole, kwa sauti yake tulivu, huku macho yake yenye upole yaki endelea kumtazama mwanadada huyu mrembo mwenye kuvutia, “nilikuwa na tembea tu, nikajikuta nimesha potelea huku” alisema Anastansia huku anakaa kwenye kiti, na kuanza kufungua kamba za viatu vyake.

Kijana mdogo anatulia kama vile anatafakari jibu la Nancy, anamtazama mschana huyu mrembo na mzuri kupita maelezo, ambae anavua viatu vyake, na kuacha nyayo za miguu yake mizuri ikiwa wazi, ambayo sasa anakanyagia juu ya viatu vyake.

“dogo naomba maji ya kunywa kwanza” alisema Nancy, huku anajiegemeza kwenye kiti, na kuwa kama amelala, akionyesha wazi kuwa alikuwa amechoka sana.

“sawa” alijibu kijana kwa sauti tulivu, ya upole, huku anaingia ndani kibanda cha udongo, akiwamwacha Anastansia amejikalisha kwenye kiti cha uvivu, anahema kwa uchovu, kichwani akishukuru kwa muumba wake, kwakujikuta amempata mwenyeji anae mfahamu katika nyumba hii, japo moyoni mwake, alijikuta anashikwa na huruma ya hali ya juu sana, kutokana na mazingira duni, ambayo kijana huyu anaishi.

Dakika tano baadae kijana mdogo anatoka nje ya banda la udongo, akiwa na jug la maji kikombe cha cha bati na mkono wakushoto akiwa amebeba kanda mbili mpya.

Kijana mdogo anaweka kandambili chini karibu na miguu ya Nancy, kisha anampatia Anastansia kikombe kitupu cha maji, Anastansia anakipokea, alafu anakinga maji ambayo anawekewa na kijana huyu mpole, ambae yeye anamwita dogo.

Maji yanaingia nusu kikombe, “yanatosha” anasema Nancy, huku anamzuwia dogo asiendelee kuweka maji kwenye kikombe, “sawa” anajibu dogo, huku anasitisha uwekaji wa maji.

Dogo anamtazama mschana huyu, ambae ata unywaji wake wa maji unavutia, mschana ambae licha ya kuonekana amechoka lakini anakunywa maji funda chache, kabla ajaacha kunywa maji, pasipo kufisha ata nusu ya maji yaliyo yanywa.

“asante sana, siwezi kunywa mengi sababu sijala kitu toka asubuhi” anasema Anastansia, huku anavaa kandambili na kuinuka toka kwenye kiti, akiwa na kikombe chake, anasogea pembeni, nakuanza kunawa uso.

Kijana mdogo, anamtazama Anastansia, ambae wakati wakunawa, alikuwa ameinama kidogo, japo alikuwa amefunga jacket kiunoni, lakini bado ungeweza kuona jinsi mschana huyu mrembo, mwenye umbo zuri, alishindwa kuzuwia mwonekano mzuri wa makalio yake.

“yani sikutegemea kama nitamwona mtu ninae mfahamu huku” alisema Anastansia, huku ananyoosha mkono wenye kikombe, kuomba maji mengine, kwa maana yale ya kwanza yalikuwa yameisha.

Kijajana ajibu kitu, zaidi ya kumsogelea anastania na kumwongezea maji, ambayo ananawa tena uso wake, kijana akiwa amesimama pembeni yake, anamtazama mpaka alipo maliza, kishana ampokea kikombe.

“dogo naweza kula muindi mmoja?” anauliza Anastansia, huku anarudi kwenye kiti, “ndiyo” anajibu yule kijana mpole, huku anaweka jug na kikombe juu ya kigogo, kisha akaelekea ndani ya nyumba ya udongo.

Anastania anachukuwa muindi mmoja, ambao ulikuwa tayari, anakaa kwenye kiti na kuanza kuula taratibu, huku akipambana na moto ulio kuwa kati muindi ule, kichwani mwake akijaribu kutafakari maisha ya kijana huyu mdogo, “sijuwi anaishi na nani hapa” anajiuliza Anastansia, huku anatafuna punje za maindi taratibu.****

Naaaam!, sasa twendeni mfaranyaki, ambako tunamwona Hidaya akiwa anashuka toka kwenye pikipi ndogo ya kukodi, nje ya jengo kubwa lenye kupangishwa, jengo ambalo anaishi mwanadada Rose.

Hidaya analipa tsh 500, kisha anaanza kutembea kuingia ndani ya jengo ilo, ambapo kolidoni anakuta shughuri zamapishi zinaendelea, Hidaya anasalimia huku anawavuka wanawake wenzake, ambao licha ya kuwa wanamfahamu, lakini walikuwa wanamtazama kwa macho flani ya tahadhari na huruma.

Hidaya anahisi ni kwanini anatazamwa vile na wale wanawake, ni sababu ya kile kilicho mtokea Rose jana, lakini yeye anapotea, zaidi anaendelea kutembea huku akiwasalimia wanawake wale, mpaka anapoufikia mlango wa chumba cha Rose, ambako anakariboshwa na sauti ya music.

Hidaya anagonga mala ya kwanza, hapati jibu lolote, anagonga mala ya pili, hapati jibu lolote, Hidaya akugonga mala ya tatu, baada yake anashika kitasa na kukinyonga, lakini mlango haufunguki.

“ata kuwa amefunga kwa ndani, mwite akusikie sauti, awezi kukufungulia kama ajakujuwa” alisema mwanamke mmoja aliekuwa karibu yake, Hidaya anatabasamu kidogo, “Rose ni mimi Hidaya nifungulie mlango” alisema Hidaya kwa sauti ya juu.

Hapo kinapita kimya cha muda mfupi, kabla ya mlango kufunguliwa, na Hidaya anakutana uso kwa uso na Rose, ambae uso wake unaonekana wazi kuwa alikuwa amelia kwa muda mrefu sana.

Maana ukiachilia kuwa yalikuwa mekundu, pia nikama yalikuwa yamevimba, huku alama za machozi zikionekana wazi kabisa usoni mwake, “karibu” anasema Rose kwa sauti ya chini, huku anaachia mlango na kurudi kikifwata kitanda, akiwa amevalia nguo zile zile alizokuja nazo kule ofisini.

Hidaya anafunga mlango, kisha anamfwata Rose, ambae sasa alikuwa anapanda kitandani, “Hidaya usiache mlango bila kufunga na funguo” anasema Rose, kwa sauti ya chini yenye uzuni na unyonge wa hali ya juu, huku anajiweka sawa juu ya kitanda.

“sikia Rose, hapa siyo pakukaa sana inabidi uondoke haraka, wanataka kuja kukuteka” alisema Hidaya huku anarusi kwenye mlango na kuufunga kwa komeo la ndani.

Rose anainuka ghafla toka kitandani, akionyesha uso wawasi, “wapo wapi?” anauliza Rose, huku anafwata viatu vyake na kuvi vaa, “sijuwi wapo watakuwa wapi, ila inuka haraka, chukuwa vitu vya muhimu tuondoke” anasema Hidaya, huku anaanza kumsaidia Rose kuchukuwa baadhi ya vitu, na kuweka kwenye begi lake dogo.

“jamani hawa watu sijuwi nime wakosea nini, inabidi niende kujificha kwa mama mdogo kule matogoro” anasema Rose akionekana mwenye wasi wasi mkubwa sana.

“kwa mama mdogo hapakufai Rose, ni bora ukajifiche bombambili, pale napoishi, kwa mama yako mdogo lazima wataenda kukuangalia” alisema Hidaya, huku wanaendelea kuweka baadhi ya vitu kwenye begi. . . . . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!