TOBO LA PANYA (18)

SEHEMU YA KUMI NA NANE

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA SABA: Lakini lakini basi, kabla matairi ya gari la ASP Mzee ayagusa barabara, akajikuta anakanyaga blake za ghafla, na kusimamisha gari, kisha wakatazama upande wakushoto, ambako ulisikika mvumo wa gari, lililokuwa linakuja kwa speed kali sana. . . . . . . Endelea….

Kufumba na kufumbua, wakaliona gari aina ya Toyota Hiace linakatiza kwa speed mbele yao, huku vijana wakipiga mbinja (miluzi) kwa ushabiki, gari lile ambalo wanalitambua kuwa ni gari la kijana Lukas, yani mdogo wa Tino Nyondo, linaenda linaenda kupunguza mwendo mita mia moja mbele, kisha bila tahadhari yoyote, lina ingia barabara kuu iendayo mikoani, likisulika kusababisha ajari kwa mwendesha baskeli mmoja.

Baada ya hapo gari linaogeza mwendo, na kupotelea upande wa kushoto wa ofisi za mkoa, “kazi hipo” anasema Aisha, huku ASP Mzee anaondoa gari bila kuongea neno lolote, “lakini hipo siku kitamtokea kitu huyu bwana mdogo, ata hao anao wategemea awatoweza kumsaidia” anasema Insp Aisha, kwa sauti iliyoonyesha wazi kuwa alimchukia kijana huyo.

“naombea siku hiyo nisiwe kazini, na wala wasiniusishe” anasema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti yenye kuonyesha chuki ya wazi, “tofauti na mimi, mwenzio natamani nishuhudie tukio” alisema Insp Aisha, ambae pia alionyesha chuki ya wazi.

“usiombe kabisa Aisha, utaingia kwenye kibarua kizito sana siku hiyo” alisema ASP Mzee, akionyesha msisitizo kwa swala ilo, “kivipi, kwani mimi ndie namtuma afanye ujinga wake” aliuliza Insp Aisha, akionekana kujijaza chuki zaidi.

“nakumbuka tukio moja, ambalo niliwai kulishuhudia la huyu kijana” alisema ASP Mzee, na kuanza kusimulia mkasa ambao, ulitokea mbele yake, na kusababisha ajisikie vibaya toka siku hiyo.**

Turudi seed farm B, ambako sasa Dogo anaweka mayai kwenye sinia, kisha anaingia ndani, ambako akai ata dakika mbili, anatoka na kiti kama kile alichokalia Nancy, anakaa na kuanza maandalizi ya mapishi, “hivi dogo unaishi na nani hapa?” anauliza Anastansia, ambae anamtazama dogo, aliekuwa anaanza kuandaa mapishi yake.

“peke yangu” alijibu dogo kwa sauti tulivu huku anaendelea kuandaa mayai kwaajili ya kuyakaanga, “mh!, unawezaje kaa hapa we mwenyewe, kwani uogopi?” anauliza Anastansia kwa sauti yenye mshtuko, huku akijikuta anazidi kuingiwa na huruma juu ya kijana huyu.

“hapana siogopi” anajibu kijana huyu, kwa sauti tulivu, wakati huo alikuwa anaendelea na maandalizi ya kukata vitunguu na kuweka kikaango jikoni, “inaweza kuwa unatania, inamaana uogopi kukaa hapa, kwani wazazi wako wapo wapi?” anauliza Anastansia, huku anamtazama kijana mdogo.

“wapo kwa babu kijijini” anajibu kijana mdogo, huku anamimina mayai kwenye kikaango, na inatokea ukelele flani wenye kutia njaa, na sekunde chache baadae inasikika harufu tamu, zinazo ingia kwenye pua za mwana dada Anastansia, na kumletea hamu ya kula.

Jibu la kijana huyu mdogo, linazidi kumfanya Nancy amwonee huruma, kwamaana anahisi kuwa kijana mdogo, amelazimika kukaa hapa kwaajili ya ugumu wa maisha, “kwahiyo ukipata sehemu ya kufanya kazi ndogo ndogo, na kujiingizia ela, unaweza kuhama hapa?” anauliza Anastansia, kwa sauti ya upole yenye wingi wa huruma.

“hapana siwezi kuhama hapa” anajibu kijana mdogo, kwa sauti ile ile ya upole, inamshangaza wazi wazi mwanadada Nancy, “he!, kwanini sasa?” anauliza kwa sauti yenye mshangao wawazi kabisa.

“sitaki kukaa na watu wengu, ni wachokozi sana” anajibu kijana mpole, huku anaendelea kukaanga yai, ambalo lilikuwa lina nukia vyema, na kuleta hamu ya kula, kiasi kwamba, ata yale maswali ya Anastansia, kama ataweza kula, yalisha ondoka kichwani mwake, na kubakia anaona anacheleweshewa kula.

“sijakuelewa dogo, unamaana gani watu ni wachokozi, inamaana unaogopa uchokozi?” anauliza Anastansia, ambae muda wote macho yake yalikuwa kwa kijana huyu, ambae ukiachilia kuwa mpole kwa vitendo na uongeaji, pia alikuwa na sura tulivu ya upole.

“hapana siogopi uchokozi, ila naepuka wachokozi, uwa siwezi kuwa vumulia” alisema kijana mdogo, kwa sauti ile ile, yani kama vile hataki kuongea, wakati huo kijana huyu, alikuwa anamalizia kukaanga yai na kuliweka kwenye kisaani kidogo.

“sijakuelewa kwakweli” alisema Anastansia, huku anamtazama kijana yule, ambae mala zote uwa amtazami usoni, ambae sasa alikuwa anamkabidhi saani ya yenye mayai, “karibu upunguze njaa kidogo” alisema kijana mdogo, huku anampatia saani Anastansia.

Anastansia anapokea saani yenye mayai, “asante, dogo, unajuwa kupika” anasema Anastansia, huku anakinga mkono wa kulia, kunawa maji aliyokuwa ananawishwa na kijana mdogo, alietumia lile jug.

“dogo ajajibu chochote, anasogelea kichanja na kuchukuwa chupa ya chai, anamimina chai kwenye kikombe, na kumpatia Anastansia, ambae anakipokea kikombe na ma kunywa funda moja, kisha anaweka kikombe chini.

“asante sana dogo, lakini ujanifafanulia, kwanini unakwepa wachokozi, au wanakuonea sana?” anauliza Anastansia, kwa sauti yenye ushawishi, huku anamtazama kijana mdogo, ambae mpaka sasa hakuwa amemjuwa jina.

Kwa mala ya kwanza, kijana mdogo anamtazama Anastansia usoni kabisa, lakini kwa macho tulivu ya upole, kiasi cha Anastansia kuhisi utofauti, kwamaana kijana huyu, siyo tu kuwa mpole na mtulivu, pia alikuwa na sura nzuri ya kuvutia.

Dogo anamtazama Anastansia kwa sekunde kadhaa, kama vile anawaza jibu la kumpatia, “nivyema ukaacha ipite, maana nivigumu kuelewa juu ya ili, na wala usitamani kuona kwa macho” alisema kijana mdogo, kabla ajaingia ndani na kumwacha Anastansia akishangaa pale nje, huku anaendelea kunywa chai kwa mayai.****

Naaaaaaaaaam!, twende mtaa wa Songea club, kwenye jumba kubwa mita mia nne toka barabara kuu iendayo Iringa, ambapo leo licha ya kuwa na magari matano mbele yake, lakini pia nje palikuwa na wanawake wawili na mwanaume mmoja, wote walikuwa wamevalia nguo za kawaida kabisa, nguo ambazo ni kawaida kwa mtu alie amua kushinda nyumbani.

Ukiachilia watu wale watatu walio kaa kibaradhani, wanaongea na kucheka kwa furaha, lakini pia Ijumaa ya leo, nje ya nyumba hii, kama ilivyo siku zote, palikuwa na nguo zilizokuwa zimeanikwa kwenye kamba, upande kulia wa nyumba.

Wakati huo huo ndani ya jumba ili kubwa, ungekuta vijana zaidi ya saba, wakike kwa wakiume, waliokuwa sebuleni wanaongea ili na lile, huku wanatazama video za mpira wakikakupu wa MBA, yani #Mbogo_Land Baskert Ball Asociation, hao tunafahamu kuwa ni madereva na wanao usika na magari ya nje, pamoja na wfanyakazi wengine wa shirika ili la siri, linalo angazia usalama wa nchi.

Jikoni nako, palikuwa na wanawake wawili, waliokuwa wanaendelea na upishi, ambao tuna wafahamu kuwa, ndio waangalizi wa mwisho wa usalama, wa ofisi hii kuu ya siri, ya mkurugenzi wa usalama wa nchi, mkoa wa Ruvuma.

Huko ndani ya ofisi sasa, palikuwa na watu watano, walio zunguka meza kubwa, mmoja wao akiwa ni mama mtu mzima, na ndie mwanamke pekee, huku mkurugenzi bwana Haule, akiwa mbele yao.

“ni miezi miwili sasa hakuna dalili za kumpata SA-26” alisema mkulugenzi Haule, ambae leo alionekana wazi kuwa katika utulivu mkubwa sana, “makao makuu hawatuelewi kabisa, ni muhimu huyu mtu apatikane, maana sababu ya yeye kuacha kazi aijawalidhisha wakuu” alisema Haule, akionyesha kusikitishwa kwake.

“inawezekana vipi miezi miwili tushindwe kumpata mtu mmoja, ikiwa tumesha wai kufanikisha mipango mingi ya kiusalama” alisema Haule, alisema mzee Haule, kwa sauti yenye kukemea, ikuionekana wazi kuwa, hakulizishwa na utendaji wa watu wake.

Kinapita kimya kifupi, kama vile kuna tafakari inapita, kwenye kila kichwa cha mtu mle ndani, mkurugenzi Haule, au James bond, anaofunua jarida lililopo mbele yake, juu yameza, anasoma mawili matatu, kisha anainua uso wake na kumtazama mwanaume mmoja kijana, aliekuwa upande wake wa kulia.

“Mahundi, kama mkuu wa upelelezi, umeishia wapi mpaka sasa katika kumtafuta SA-26” anasema mkurugenzi Haule, au baba Eric, kwa wanao mfahamu, huku anamkazia mwanaume mmoja kijana, karibu yake upande wake wa kulia . . . . . . . . Endelea…. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!