TOBO LA PANYA (19)

SEHEMU YA KUMI NA TISA

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE: “Mahundi, kama mkuu wa upelelezi, umeishia wapi mpaka sasa katika kumtafuta SA-26” anasema mkurugenzi Haule, au baba Eric, kwa wanao mfahamu, huku anamkazia mwanaume mmoja kijana, karibu yake upande wake wa kulia . . . . . . . . Endelea….

Hapo mwanaume kijana mwenye makalio wa miaka 30, anajikooza kidogo, kisha anaanza kueleza, “mkuu, tumefwatilia kwa ukaribu matukio na kumbu kumbu za SA-26, tumegundua kuwa, ni mtu asie tabilika kama tunavyozania, au kama maelezo toka makao makuu yanavyosema” alisema yule mwanaume kijana.

Wote mle ndani wanatega masikio, kusikiliza maelezo ya mkuu wa upelelezi na uchunguzi wa SA mkoa wa Ruvuma, “nivigumu kumpata SA-26, kwa kukadilia maisha yake ya sasa” alisema bwana Mahundi, ambae akuishia hapo.

“kwanza kabisa hakuna kumbu kumbu ya picha yake ata moja, wala jarida lake, sehemu yoyote, pili hakuna hakuna mtu aliewai kumtabiri, wala kumkadilia ata fanya nini au atakuwaje dakika tano zijazo” anasema mpelelezi Mahundi.

Hapo nikama Mahundi akuweleweka vizuri, maana wajumbe wote wanatazamana, kabla mzee Haule ajaomba ufafanuzi, “bwana Mahundi, ebu fafanua hapo, unamaanisha nini unaposema kumkadilia tabia zake, kwa dakika tano zijazo” alisema mzee Haule,.

“mfano, siku ambayo alikutana kwa mala ya kwanza na mkurugenzi Kingumwile, kipindi ambacho SA-26 akiwa darasa la, wakati ambao kulikuwa na seku seku kubwa la hukumu ya kesi ya meno ya tembo, ambayo ilikuwa inausisha vigogo watatu wa hapa Songea” anasimulia Mahundi.

“mkurugenzi Kingumwile, alikuwa ndie shahidi muhimu katika kesi hiyo, na ndio wakati ambao, watuhumiwa walikuwa wanapambana kupoteza ushahidi wakesi yao, kituambacho Kingumwile mwenyewe alikuwa anakijuwa, na kuanza kuishi kwa tahadhari”

“lakini siku moja, kingumwile, akiwa kwenye gari lake binafsi, mida ya jioni anatoka kazini, akiwa anakatiza kwenye barabara ya makambi, kuelekea mabatini, ambako yeye alikuwa anakaa”

“mala akaona waona kikundi cha watoto sita wakiume, wanafunzi ambao umri wao ni miaka kati ya 12 mpaka 15, ambao walikuwa wanamshambulia mtoto mwenzao wa kiume, mwenye umri kati ya miaka 13 au 14”

“ni eneo ambalo halikuwa na makazi ya watu, hivyo bwana Kingumwile akaona kuwa yeye ndie msaada pekee kwa mtoto yule, ambae alionekana kuwa mnyonge sana”

“lakini ile shukuka tu, wale watoto wengine wakakimbia, na kutokomea vivhakani, wakimwacha yule mnyonge akiwa amejiinamia, kwa unyonge, japo kunakituambacho kilimshangaza sana bwana Kingumwile, kwamaana licha ya kipigo ambacho, wale watoto walikuwa wamemshushia mwenzao, lakini hakuonyesha dalili ya kwamba alikuwa analia”

“aya mtoto nzuri, nenda nyumbani haraka, wasije kukukuta tena wale wakorofi” alisema bwana Kingumwile, ambae wakati huo huo ndipo alipogudua kuwa, gurudumu moja la gari lake, limepata pancha, na linakaribia kumaliza upope kabisa.

“kwakuwa bwana kingumwile, alikuwa na tairi la akiba, akaona itakuwa vyema akibadiri kabisa tairi, lakini kabla ajafanikiwa kufungua ata mlango wa gari lake, ili afungue buti, akashtuka inakuja pikipiki moja kubwa kwa speed kali sana, na kusimama karibu yagari lake, ikiwa na vijana wawili wenye miili iliyooshiba kwa mazoezi.

Mwanzo Kingumwile akuwa na wasi wasi, juu ya ujio wa vijana wale wawili, lakini alishtuka baada ya kumwona mmoja kati ya vijana wale, anashka toka kwenye pikipiki, na kutoa kisu vikubwa sana, chenye kung’aa kwa makali yake, hapo mkurugenzi Kingumwile, akajuwa tayari mwisho wake umefika.

“Sali sala zako za mwisho, uende ukatoe ushidi kaburini” ilisikika sauti nzito isiyo na huruma ya kijana alieshuka toka kwenye pikipiki, ambae anamkaba mzee Kingumwile, akimkanda miza kwenye gari lake mwenyewe, mzee kingumwile akumwona tena yule mtoto nyonge, akujuwa ametoweka vipi, anawaza kama wale watoto walikuwa ndani ya mpango huu, lakini anakosa jibu.

Hakika jambo ili lilikuja kwa ghafla sana, wakati ambao Kingumwile hakuwa na uwezo wakujitetea, maana bastora ilikuwa ndani ya gari, hapa hakuwa na kitu chochote, ambacho angeweza kutumia kama silaha, “hoya maliza kazi tuondoke zetu” alisisitiza mmoja wao, yani alie bakia juu ya pikipiki, iliyo kuwa inaunguruma.

Hapo mzee kingumwile, katika hali ya kukata tamaa anamwona yule kijana anavuta kisu kwanguvu, tayari kukikandamiza kwenye tumbo lake, nae anatoa macho ya hofu na uoga, tayari kuyapokea maumivu yatakayo mjia.

Lakini ghafla anashtuka anamwona yule kijana mdogo, anaibuka kwa ghafla huku akipeleka mkono wake kwenye uso wa yule jamaa mwenye kisu, “mamaaaa na jicho languuuu” yule jamaa anapiga ukelele wa maumivu, huku anaachia kisu ambacho kinaanguka chini, na yeye kupeleka mkono usoni, sambamba na damu nyingi usawa wa jicho.

Kingumwile akiwa katika hali ya kushangaa, anaona kipande cha karamu ya risasi, yani penseri, ikiwa inaning’ia kwenye jicho la kulia la huyu jamaa, wakati huo huo, yule jamaa, alie bakia kwenye pikipiki anashuka kwa haraka, akiiacha pikipiki inajibwaga chini.

Hapo kingumwile anakumbuka inabidi afanye jambo, kwa haraka, maana niwazi huyu jamaa anakuja kumaliza lile aliloshindwa mwenzie, lakini kwa akili ya haraka, asingweze kuchukuwa bastora na kufyetua huyu jamaa, na kiukweli akuwa vizuri kwenye sanaa ya mapigano.

Lakini wakati anajiuliza afanyeje, anamwona yule mtoto mdogo wa miaka 14, akiinama kwa haraka na kuzowa mchanga, ambao aliurushwa kwa haraka usoni kwa yule jamaa alie ruka toka kwenye pikipiki.

Ambae ni wazi akutarajia tukio ilo, maana mchanga unamfika usoni, macho yana jaa mchanga na kumfanya apate upofu wa muda, maana ata Kingumwile alimwona yule jamaa wapili anapeleka mikono usoni, na kupapasa macho yake.

“we mtoto ni shetani mkubwa” alisema kwa sauti iliyo jaa hasira kali, jamaa alie tobolewa jicho moja, huku anamsogelea mtoto mdogo, akionyesha wazi anaenda kumnyonga.

Lakini aikuwa hivyo, maana bwana Kingumwile alishuhudia kitu ambacho akutegemea kukiona kwa wakati huo, yani ile jamaa anamfikia tu yule mtoto, nyonge, kingumwile alimwona yule mtoto, akiinama chini na kuokota kile kisu, ambapo ile kuinuka, aliinuka nacho amekitanguliza juu, nacho kikaenda kujikita kwenye koo, la yule jamaa ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata