TOBO LA PANYA (20)

SEHEMU YA ISHIRINI


ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TISA: Lakini aikuwa hivyo, maana bwana Kingumwile alishuhudia kitu ambacho akutegemea kukiona kwa wakati huo, yani ile jamaa anamfikia tu yule mtoto, nyonge, kingumwile alimwona yule mtoto, akiinama chini na kuokota kile kisu, ambapo ile kuinuka, aliinuka nacho amekitanguliza juu, nacho kikaenda kujikita kwenye koo, la yule jamaa ……..Endelea ….

Bwana kingumwile akatoa macho ya mshangao, anamwona mtoto mdogo anachomoa kisu kwa nguvu, na kwenda kwa yule ambae alikuwa anapapasa macho yake kuondoa mchanga, akimwacha huyu mwingine, amesimama kama sanamamu, na mikono yake ikiwa shingoni, damu nyingi zina mvuja.

Kingumwile anamwona kijana mdogo, anakandamiza kisu kwenye eneo la chembe ya moyo, ya yule kipofu wa muda, na kuchomoa, kisha anarudia mala kadhaa, kama alikuwa anachoma kwenye mgomba au kitu chochote cha mdhaha.

Baada ya kuchoma mala kadhaa, kijana ambae adi shati lake, lilikuwa limelowa damu, akaacha kisu chini na kutaka kuondoka, “usindoke kijana, unaitaji nguo mpya, uwezi kwenda nyumbani namna hiyo” alisema kingumwile, ambae ndie mtu pekee anae fahamu jina la harisi la SA-26.

“licha ya kuwa huo ndio mwanzo wa Kingumwile, kumwajiri kijana huyo na yeye kumlea kama kijana wake, lakini ata yeye akuweza kumwelewa kijana huyu, kuwa ni mtu wa aina gani, asa linapokuja swala maisha yake au maamuzi yake” alieleza mpelelezi Mahundi.***

Saa sita mchana, nyumbani kwa tajiri Tino Nyondo, tunamwona bwna Augustino Nyondo mwenyewe, akiwa sebuleni, anapata chakula cha mchana, huku, huku mfanyakazi mmoja akiwa amesimama pembeni yake.

Bwana Nyondo anaonekana mwenye hasira na chuki za wazi kabisa, maana licha ya kukunja sura kwa hasira, pia alikuwa anasonya kila dakika, “mschana masikini kabisa, anawezaje kunidharau mimi” anajisemea Nyondo.

Wakati huo huo unasikika mlio wasimu ya mezani, iliyokuwepo mita chache toka kwenye kochi alilokaa, yule mfanya kazi ana chukuwa mkonga wa simu wenye waya inayo vutika, na kumpatia boss wake.

“niwekee maji kwenye grass” anasema Tino Nyondo huku anaweka uma pembeni, na kupojea mkonga wa simu, kisha anaweka simu sikioni, na kusikilizia kidogo, kuangalia mazingira ya mtu anae piga simu.

Nyondo anagundua kuwa ni mazingira tulivu, pengine ni ofisini, “Tino Nyondo ndiyo hapa, nani mwenzangu” anasema Nyondo, kwa sauti tulivu na kavu, “ni SP Zamoyoni hapa, RCO” ilijitambulisha sauti toka upande wapili wa simu.

“hallow bwana Zamoyoni, habari za leo” alisalimia Nyondo, kwa sauti tulivu, huku uso wake ukionyesha wazi, kuto kuipenda ile simu, sijuwi kwa nini, “salama bwana Nyondo, ila kunajambo naitaji tuongee kidogo” ilisikika sauti ya kiume toka upande wapili wa simu, “nakusikiliza bwana Zamoyoni” anasema Nyondo huku anamtazama mfanya kazi wake aliekuwa anamimina maji kwenye grass.

“bwana Nyondo, nikweli tunakuheshimu na kukupa uzito katika mkoa huu, lakini naomba uwaeleze vijana wako, wawe makini wanapo fanya majukumu yao, maana jana tumeokota mwili ambao unaushaidi wa kuwa vijana wako wanausika moja kwamoja” ilisikika sauti upande wapili wasimu.

Nikama swala lile linamkela Zamoyoni, “unazungumzia mwili hupi, maaana toka juma nne, wamesha fanya kazi tano, kama hizo?” aliuliza Nyondo kwa sauti ya taratibu, yenye dharau nyingi, huku anamtazama mfanyakazi wake ambae sasa alikuwa anamaliza kuweka maji kwenye grass.

“ni kule msamala kwenye daraja la mto luhila” ilisikika sauti ya upande wapili wa simu, na wakati huo mfanyakazi yule wakiume, ambae alikuwa amesha maliza kumimina maji, sasa alikuwa anainua grass, na kuisogeza karibu na bwana Tino Nyondo.

“nani anasimamia ilo swala?” aliuliza Nyondo kwa sauti ile ile ya taratibu, “ni bahati tu lipo chini yangu, na nimesha lizibiti…” hakika bwana Zamoyoni hakupewa nafasi ya kumaliza kuongea.

“Zamoyoni, acha ujinga, sasa unanieleza ili iweje” safari hii Nyondo alipaza sauti, huku anagonga ngumi kwenye meza, na wakati huo huo, kwa bahati mbaya, yule mfanyakazi wakiume, alikuwa anaweka maji mezani, na kusababisha grass ipinduke na maji yanatawanyika hovyo, na mengine yanafika kwenye suruali ya bwana Nyondo.

Ambae anainuka ghafla, kuepusha maji yasiingie ndani zaidi, japo alikuwa amesha chelewa, maana aliusikia ubaridi mpaka kwenye chup, na kengere zake na hasiri, “samahani boss, aikuwa kusudio lang…..” alisema yule mfanya kazi huku anakusanya mikono usawa wakifua chake, akiashiria anautaka msamaha.

Lakini akupewa nafasi ya kusikilizwa maana bwana Nyondo aliinya uma aliokuwa anautumia kulia chakula, na kuukita shingoni kwa mfanya kazi wake huyu, kisha akamwacha anayumba kama mlevi, na kujibwaga chini, huku damu zina mchuruzika shingoni mwake.

“bwana Nyondo, sinamaana mbaya, ila ni tahadhari tu” maongezi kwenye simu yalikuwa yanaendelea, “tahadhari ya nini Zamoyoni, kuna kitu cha kunitisha mimi, au tanakiwa kaa kama konokono pale wajinga wanapo gusa pumbu zangu?” alisema kwa ukali bwana Nyondo, ambae akujisumbua ata kumtazama yule mfanya kazi aliekuwa anatapa tapa, kwa kurusha mikono na miguu, ikiwa ni angaiko la kukata roho.

Nyomdo akusubiri kauri yoyote, toka upande wapili wa simu, baada yake anakata simu, kwakuiweka sehemu yake, na kuanza kutembea kutoka nje, anatazama kwenye maegesho ya magari, waona vijana wake wakiwa wamesimama wanaongea na kucheka.

“Kichondo, waambie vijana wawili wakatoe mzoga sebuleni kwangu, kisha pasafishwe haraka” alisema Nyondo, huku anatazama mbele na gari aina ya Toyota hiace lililokuwa lina shusha vijana watano, Lukas akiwa mmoja wao.

Lukas anatembea kumfwata kaka yake, huku rafiki zake wakina Kubaga, wakiwa wamesimama nje ya Toyota Hiace, wanamtazama rafiki yao, “mnaweza kuniambia Rose yupo wapi?” aliuliza Tino Nyondo, huku anarudi ndani.

“amejifanya kukimbilia kwa mama yake mdogo, huko Matogoro” anajibu Lukas ambae alikuwa anamfwata nyuma kaka yake, huku vijana wawili wanaingia ndani, kwenda kutoa mwili wa mfanyakazi.

“kwahiyo hapa mnafanya nini, ikiwa bado amjampata huyo mwanamke?” anauliza Nyondo, huku anasimama na kumtazama mdogo wake, “ata tukienda wkwa mama yake mdogo, bado atakuwa ajafika, tuna vizia baadae kidogo tuka mdabue” alisema Lukas, huku wanashushidia vijana wawili, wakiwa wameubeba mwili wa mfanya kazi, wakiutoa nje.

Hapo Augustino Nyondo anatulia kwa sekunde kadhaa, kama anawaza jambo flani, kisha anamtazama mdogo wake, “hapo kidoooogoo, unaelekea kuwa kama ninavyotaka” anasema Tino Nyondo, huku anamgusa bega mdogo wake.

“kaka utakubari tu mziki wangu, ngoja nikaluletee yule demu” alisema Lukas kwa majigambo, “ok!, hakikisha jioni unampata Rose” alisema Nyondo kwa sauti ya msisitizo, kisha akaelekea chumbani kwake, kubadiri nguo, huku Lukas nae akirudi nje, kuungaa nawenzake, ambao walikuwa wanavuta bangi na kunywa pombe.***

Naaaaaam! saa saba za mchana, kule seed farm, nje ya kijumba cha udongo, ambako bado tunamwona mwanadada Nancy akiwa pale, na mwenyeji wake, yani kijana mpole, ambae anakila mwonekano wa kusema ni mnyonge.

Sasa wawili awa, walikuwa upande wa nyuma wa kichuguu kikubwa, kilichungana na kibanda cha udongo, Nancy alie valia kandambili, alikuwa anakagua na kutazama mazingira yanayozunguka eneo lile.

“kwahiyo dogo unaishi peke yako?” aliuliza Anastansia ambae ninaposema ni mschana mzuri, elewa kuwa ni mzuri aswaa, “ndiyo” anajibu kijana mdogo, kwa sauti tulivu ya upole.

Kinapita kimya kifupi, wanapita kwenye mabanda ya kuku na mbuzi, wanaelekea upande ambao unashamba la mihogo, na maindi, wanatazama huku nikama vile kila mmoja alikuwa anawaza la kwake kichwani.

Maana kijana mdogo alikuwa anamtazama Anastansia kwa macho ya wizi, akijaribu kuusadifu uzuri umbo la mschana huyu, ambalo licjhakukutana na maumbo mazuri ya wanwake, lakini hakuwai kumwona mwanamke alie barikiwa kila kitu kama huyu.

Lakini wakati huo huo, Anastansia ambae akuwai kuwaza ududu ata siku moja, anajikuta katika hali ambayo akuwai kuiwaza ata sikumoja, “mh!, hivi akama ningekuwa kama mwanaume sinaweza ata kukalazimishe kanifanye, alafu nakakataza kutangaza” anawaza Anastansia, ambae anajikuta anaishia kutabasamu kwa ujinga alio uwaza. ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata