
SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MOJA: Anastansia akiwa amezama kwenye mawazo ya kipuuzi, huku anachuma zambarau, mala anashtuka kuona kijana mdogo ameachilia tawi, nalo likapanda juu, na kuchomoka mikononi mwa Anastansia, nikama kijana mpole alishtukia kile ambacho, Anastansia alikuwa anakitazama kwake. . ……..Endelea ….
“mbona umeachilia” anauliza Nancy huku anamtazama kijana mdogo, “uwezi kumaliza zote, zinakela kwenye meno” anasema kijana mdogo, huku anaweka vyema sehemu zake za mbele, ambazo zilikuwa katika hali mbaya ya matamanio.
Sasa ni kama walikuwa wanaoneana aibu, japo Nancy alikuwa anatabasamu mala kwa mala, kila alipokumbuka tukio la msimamo wa dudu ya kijana mdogo, ambae mpaka sasa akuwaikutabasamu ata kwa bahati mbaya.
Lakini hali ya kuoneana aibu inaisha muda mfupi baadae, pale waliporudi mbele ya kijumba cha udongo, na kuanza kusaidian kukujipikilisha chakula cha mchana, wakiwa wamechinja kukummoja, na kuanza kumwandaa kama mboga ya kulia ugari, ambao waliupika muda mfupi baadae.
Ama hakika kila dakika zilivyoenda ndivyo walivyo zidi kuzoweana na kila mmoja kumfahamu mwenzie, kwamaana kijana mdogo, alimfahamu Nancy kama mwanamke mzuri zaidi ya vile alivyokuwa anamwona, hakuw na majivuno, ila alikuwa ni kutoka katika maisha mzuri na familia bora.
Huku Nancy yeye akigundua kuwa kijana huyu mdogo, siyo mwongeaji, ila ni kijana mkarimu sana, ambae mwenye upendo kwake, ila ni mwanaume kama wanaume timamu, kama wanaume wengine.
Lakini kilicho msumbua akili ni namna ya kumfanya kijana huyu awe mwenye furaha, maana alionekana wazi kuwa mnyonge na mwenye kukosa furaha na amani ya maisha.***
Naaaaam, saa 11 kasoro za jioni, ndani ya ofisi ya mkulugenzi wa TSA, kikao bado kinaendelea, mkulugenzi Haule anaendelea kupokea maelezo toka kwa afisa upelelezi, wa mkoa, ambae alijaribu kueleza ugumu wa kumpata SA-26.
“kwamujibu wa taarifa za kiuchunguzi, ni kwamba, SA-26, ni mtu ambae licha ya kutokuwa na rafiki wakaribu, pia ni mtu ambae uwezi kumtabiria kile ambacho anataka kukifanya muda mfupi ujao, pia ni mtu ambae akuwai kuonekana na katika starehe ya aina yoyote” alieleza mpelelezi Mahundi
Mahundi akuishia hapo, akaendelea kufafanua, “taasisi ilijaribu kumwekea mitego kadhaa, ili kumfahamu zaidi wakara wao, ikiwa ni kumtega kwa starehe na burudani mbali mbali, lakini ilishindika, na mbaya zaidi, ata walipo jaribu kumtega kwa kumsakizia wakala wakike, ili awenae kimapenzi, lakini pia ilishindikana” alisema Mahundi.
“kitu cha kushangaza zaidi, alipoondoka kwenye taasisi, na file lake likatoweka moja kwa moja, hivyo hapajabakia kumbu kumbu yoyote ya mtu huyo, ambae makao makuu waitaji afe ili kulinda siri, na uwezekano wa kuto kutumiwa na maadui wa serikali yetu” alisema mpelelezi Mahundi.
Akiwa bado ajamaliza kuongea, bwana Mahundi akaendelea kueleza, “lakini taarifa toka kwa mchunguzi wa siri ambae nime mweka, ambae anaangaika usiku na mchana, kumtafuta SA-26, mpaka sasa wamesha wafwatilia vijana wanne, lakini bado majibu yanakuja siyo mawakala na hawajawai kuwa mawakala wa SA” alimaliza Mahundi.
Hapo kila mmoja mle ndani akashusha pumzi ndefu, “mliwai kudodosa sababu ya SA-26 kuachana na mawakala wa siri?” aliuliza mama mtu mzima, “hakuna anaefahamu, wapo wanaosema alichukizwa na kitendo cha kukamatwa na polisi, wengine wanahisi ameshawishiwa na mashirika binafsi ya kijasusi” alisema mpelelezi Mahundi.
Hapo kinapita kimya kifupi, kila mmoja akitafakari jibu la mpelelezi Mahundi, “lakini taalifa za mwanzo zilisema huyo bwana, akuna alie wai kumtabilia anachokusudia kufanya, sindio?,” aliuliza mkulugenzi Haule, huku anamtazama Mahundi.
“ndiyo mkulugenzi, hakuna aliewai kutabiri japo kwa dakika tatu mbele SA-26, atafanya nini” alieleza Mahundi, nahapo mkulugenzi Haule akaachia tabasamu lenye mlengo wa masikitiko.
“kwahiyo tukubaliane jambo hapa” anasema Haule, na kuwafanya wajumbe watege masikio yao kumsikiliza kwa umakini, huku macho yao yakielekea kwa mkulugenzi Haule.
“mpaka sasa hakuna ukweli wowote, kwenye vitu tulivyo hisi kwa SA-26, kuanzia sababu za kuacha kazi, wala maisha yake ya sasa, hivyo ni wazi tunatakiwa kuongea juhudi na umakini mkubwa, katika msako huu” alisema Haule kwa sauti yenye msisitizo.
Kila mmoja anatikisa kichwa juu chini, kukubaliana na mkulugenzi, kwamba anachosema niukweli mtupu, hapo mkulugenzi anamtazama mkuu wa kitengo cha utendaji kimapigano, “abdulkareem na wewe inabidi ujipange, nazani umesikia jinsi ambavyo kijana anauwezo wa kupambana” alisema Haule, huku wenzake wakiendelea kumsikiliza.
“sitarajii kusikia kifo au madhara yoyote kwa wakala, zaidi natarajia kumwona SA-26 akifikishwa hapa mzima” alisema mkulugenzi Haule, “ndiyo mkulugenzi, maagizo yako ni kipaumbele kwetu” alijibu mkulugenzi wa kikundi cha mapigano.
“basi watu waendelee na msako, naitaji taarifa za mala kwa mala” alisema mkulugenzi akiwa na maana ya kufunga kikao, maana baada ya kutamka hayo kila mmoja akainuka na kuelekea nje ya chumba iki, ambacho kinatumika kama ofisi ya mkulugenzi, wakimwacha yeye mwenyewe mkulugenzi.
Ambae anamaliza kuweka sawa mambo yake, kisha anatoka ofisini, ambapo anamkuta dereva wake ndani ya gari, aina ya Toyota land cruiser, “twende zwet nyumbani, nimemiss vituko vya wakina Eric” alisema mzee Haule, na dereva akaondoa gari kuifwata barabara kuu iendayo mikoa ya iringa na Mbeya.
Dakika nne baadae anakuwa tayari amesha ifikia barabara hiyo, na kukata kona kushoto, akishika upande wa mjini, ambako anatembea mita kama mia nne kisha anakata kona kushoto, kushika barabara iendayo mikoa ya kusini, yani Lindi na Mtwara.
“mkuu hivi Eric amepata nafisi ya kidato cha tano?” anauliza dereva, “hapa amepata huko Songea boys, na Eva pia amepata Songea girls, ila naofia sana” alisema mzee Haule.
“unaofia nini mkuu, wewe ni James Bond bwana” alisema dereva, akimalizia kwa kicheko, “mh!, hiyo aiitaji elimu ya upelelezi daraja la kwanza, unazani itakuwaje akimpachika mimba binti wawatu, akiwa kidato cha tano au sita?” aliuliza mzee Haule.
Na kabla dereva ajatoa jibu, Haule akaeleza wasi wasi wake mwingine, “vipi ile tabia yake ya kupigana mala kwa mala, atavumulia uchokozi wa wanafunzi wenzake?” anauliza tana bwana Haule, na hapo dereva anacheka kidogo.
“mkuu hapo inabidi tusubiri matokeo tu…” kabla ajamalizia kuongea vizuri dereva, ambae alikuwa anaendesha gari kuvuka eneo la Angon arms, mala ghafla mita chache mbele yao, wakaliona gari aina ya Toyota hiace likiingia barabarani, kutokea upande wa kulia wa barabara, kwenye mchepuko wa barabara itokayo shule ya waschana ya Songea na mtaa wa mateka.
“kum.. make, awa washenzi nini” anang’aka mzee Haule, wakati dereva anatumia ufundi wake kulikwepa lile gari, na kubakia kidogo waingie kwenye mtaro wa pembeni ya barabara.
Mpaka wanakaa sawa, nakulitazama lile gari, wanalio tayari limesha shika mwendo kuelekea upande waliokuwa wanaelekea wao, “dah!, kumbe kuna watu wanaishi kwa amani kiasi hiki” anasema mzee Haule, huku dereva anaensha gari taratibu kulirudisha barabarani.
“mpuuzi sana huyu dogo, anajiamini kwaajili ya kaka yake” alisema dereva wa mzee Haule, ambae kwa majina anaitwa Jacob, “kumbe unamfahamu huyu mjinga” anauliza mzee Haule, kwa sauti yenye shahuku.
“huyu ni mdogo wake Augustino Nyondo, anaitwa Lukas Nyondo, anasifa ya fujo na matukio ya ajabu, na watu wanamwogopa sababu ya kumwogopa kaka yake, maana inasemekana, unaweza kusamehewa na Tino Nyondo kwa kosa lolote, lakini siyo kosa la kugusa mdogo wake huyo” anafafanua Jacob. . ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU