TOBO LA PANYA (23)

SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI: “huyu ni mdogo wake Augustino Nyondo, anaitwa Lukas Nyondo, anasifa ya fujo na matukio ya ajabu, na watu wanamwogopa sababu ya kumwogopa kaka yake, maana inasemekana, unaweza kusamehewa na Tino Nyondo kwa kosa lolote, lakini siyo kosa la kugusa mdogo wake huyo” anafafanua Jacob. . ……..Endelea ….

“mh!, huo mziki kuuzima kwake, lazima damu nyingi imwagike” anasema Haule kwa sauti yenye kupoa kidogo, huku wanalitazama lile gari ambalo sasa lilikuwa limesha potea machoni mwao, na kubakiza vumbi pekee mbele yao.***

Yaaaap!, mida hii ya saa kumi na moja za jioni, tayari wakina Anastansia na kijana mdogo, walikuwa njiani wanatembea taratibu kutoka seed farm B, kuelekea matogoro, kilipo chuo cha ualimu.

Safari yao ilikuwa na maongezi machche sana, hii ni kutokana na ukimya wa kijana mdogo, lakini vichwani mwao, walikumbukumbu ya wakati mzuri sana waliokuwa nao toka mida ya saa nne za asubuhi mpaka mida hii ya saa kumi na moja.

Hakika walikuwa na wakati mzuri sana, maana ukiachilia wakati ule wakimaliza kuchuma zambarau na kuanza kupika, ila pia walishirikiana kuandaa kuku na kumpika, huku wakimkaanga vizuri kabisa, na baadae kupika ugari, ambao walikula kwapamoja, wakitumia saani moja.

Wakati hayo yanaendelea, wawili hawa ambao wanahistoria tofauti za kimapenzi, na pia wanamwonekano usio fanana kuwa wapenzi, kutokana hadhi zao, lakini kila mmoja alikuwa anamtazama mwenzie kwa kuibia, huku akijaribu kuthminisha kile alicho kithaminisha kwa mwenzie, japo kuna wakati kila mmoja alimshtukia mwenzie, kuwa alikuwa anamtazama kwa macho yasiyo ya kawaida.

Kuna wakati ambao, walijikuta wamegusana sehemu nyeti kwa bahati mbaya, kama vile kifuani makalio ata tumboni, na kujikuta wakisisimkwa miili yao, kwa upande wa kijana mdogo sijafahamu kwanini anakuwa hivi.

Lakini kwa Anastansia, pengine naweza kusema ni kutokana na kuto kushiriki mapenzi kwa muda mrefu, tena alishiriki mala moja tu, na akufurahia tendo lenyewe.

Japo hiyo aikuwa sababu ya yeye kusisimkwa namna ile, maana ni muda mrefu akujihisi kutamani dudu, wala kutamani kuingia kwenye mapenzi, na mwanaume yoyote.

Safari inaendelea, huku kila mmoja wao akitamani wasifike mapema chuoni, maana kufika kwao chuo ndio mwisho wa wao kuwa karibu, na pia wangelazimika kutawanyika, pale muda wa saa 12 utakapofika.

“dogo tupite barabara kubwa tukatokee viwanjani” alishauri Anastansia, wakiwa wamebakiza mita kama mia moja hivi, kuifikia makutano ya barabara iendayo matogoro, kupitia makutano, na hii iendayo mikoa ya kusini.

Japo ilimshangaza kijana mdogo, ambae akuelewa maana ya Anastansia kuchagua barabara ile, ambayo kama wangepita, ingewachukuwa lisaa lizima kufika chuoni, kwa mwendo ambao walikuwa wanatembea, ambapo wangekuta mpira umeisha malizika.

Lakini kwa kuwa na yeye alipenda kuongozana na mschana huyu, anajikuta anaendelea kumfwata, kama mbuzi anae pelekwa malishoni, huku akisikiliza hadithi nyingi za maisha ya kifahari ya mwanamke huyu, aliyo simulia yeye mwenyewe Nancy.

Lakini basi wakiwa wanakaribia kuifikia hiyo barabara kuu ya kuelekea matogoro, ile ambayo inaelekea kwa babu Mchopa, mala ghafla wanaliona gari aina ya Toyota Hiace, maarufu kama dala dala, kwa wakati huo, likipita kwa speed kuelekea kule walikokuwa wanaelekea wao, huku likitimua vumbi vibaya mno.

“mh!, kumbe dala dala zinakimbia namna hii, abiria awaogopi?” aliuliza Anastansia kwa sauti yenye msgangao, huku wakitazama kwenye barabara iendayo matogoro, “siyo la abiria lile” alijibu kijana mdogo kwa sauti tulivu, huku wanaendelea kutembea kusogelea makutano ya barabara.**

Naaaaaam! Tunaliona gari aina ya Toyota Hiace, likiwa linatililika kwa fujo kuelekea upande wa mashariki mwa mji wa Songea, liacha barabara iendayo mikoa ya kusini na kuishika ile iendayo matogoro.

Huku gari ilo likitimua vumbi kwa fujo, ndani yake kukiwa na vijana watano, waliokuwa wanaendelea kutumia vinywaji na vivuto haramu, pasipo kujari kuwa, dereva wao pia, alikuwa anatumia vilevi hivyo, pasipo kujari usumbufu na hatari wanayo isababisha kwa watumiaji wengine wa barabara.

“huyu demu leo atajuta kuzaliwa, kwanza nitakesha nae usiku kucha, alafu ndio namkabidhi kwa bro” alisema Lukas ambae ndie dereva wagari ili, ambae kiukweli, licha ya kusababisha kifo cha mpenzi wa Rose, yani Aloyce, lakini hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke huyo.

“sasa Lukas, sawa tunaenda matogoro, kwani unapafahamu nyumbani kwa huyo mama yake mdogo” aliuliza Kubaga, huku safari inaendelea kwa speed kali, wakati huo barabara hii ilikuwa ya vumbi.

“weweeee!, mimi ndio kidume cha huu mji, dakika chache tu, tuna mnasa huyo mwanamke” alisema Lukas kwa sauti ya majigambo, hapo hapo mwingine akadakia, “napafahamu anapokaa mama yake mdogo, zamani nilikuwa na demu mitaa hiyo, ni pale kwenye njia panda ya kwenda kwa Mkwawa” alisema mwenzao.

“unasema kweli Tiba, basi kazi imekuwa lahisi” alisema Lukas, kwa sauti yenye furaha, “sema Lukas inabindi tumnyakuwe chap kwa haraka, maana tukichelewa tu, raia wanaweza kutujazia nzi” alisema Kubaga, kwa sauti yenye tahadhari.

“nani wakusumbua bwana, ninachamoto hapa” anasema Lukas huku anaonyesha bastora kwenye mkebe wa dash board, na wote wanacheka kwa pamoja, “aina aja ya kutumia chamoto, mtu atakae leta ujinga tunamkamua mpaka ajute” alisema yule alie itwa Tiba, ikiwa ni kifupi cha jina lake, yani Tibasana.

“alafu pale yule mama anaishi peke yake, labda kama ameolewa siku za hivi karibu” alisema tena Tibasana, “tena kama analipa na yeye anaongwa vile vile” alisema kubaga, na wote wacheka, huku safari yao inaendelea, ukiwa nimwendo wa kasi, ulio nusulika kusababisha ajari, kwa watumiaji wengine wa barabara.***

Dakika saba baadae, kwenye barabara ile ile, tunaliona gari aina ya Toyota land cruiser, lenye amba za TZA…….., likimaanisha kuwa ni amba za mtu binafsi, lakini gari ili ndio lile ambalo, anatumia mkulugenzi Haule, kama gari la kazini kwake.

Safari inaendelea huku wanaongea ili na lile, kuhusu Eric mtoto wa mzee Haule, na mpenzi wake Eva mzungu, sasa walikuwa wanayavuka kwenye makutano ya barabara, “Jacob, ebu ona ile kitu” anasema mzee Haule kwa mshtuko, huku anatazama mbele ya barabara, akiwatazama watu wawili, waliokuwa wanakuja taratibu.

Jacob anatazama na kumwona kijana mmoja mdogo, mpole mwenye sura ya kinyonge, alie valia suruali ya jinsi iliyo pauka kwa uchakavu, na tishert jeusi lenye kupoteza upya wake, alie ongozana na mschana mmoja mzuri wakutamanisha, alie valia turck na tishert. . ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!