
TOBO LA PANYA (24)

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU: Jacob anatazama na kumwona kijana mmoja mdogo, mpole mwenye sura ya kinyonge, alie valia suruali ya jinsi iliyo pauka kwa uchakavu, na tishert jeusi lenye kupoteza upya wake, alie ongozana na mschana mmoja mzuri wakutamanisha, alie valia turck na tishert. . ……..Endelea ….
Shida aikuwa kwa kijana mdogo, ambae mzee Haule, alikuwa anamwona mala kwa mala katika barabara hii, na kuhisi pengine analinda shamba la mtu fulni huko mbele ya mtaa wao, siku zote alionekana kuwa mnyonge na mwenye utulivu uliopitiliza.
“duh!, nilizania watoto wazuri wameisha” Jacob nae anatoa macho kwa mshangao, wote walimtazama mwanamke mrembo alie ongozana na kijana huyu, “pengine nimtoto wa mmiliki wa eneo analo Linda yule bwana mdogo, maana anaishi kule kwetu kwambele zaidi” anasema mzee Haule, wakati wanapishana na watu wale.
“sijuwi atakuwa mtoto wanani huyu?” anauliza Jacob, “sizani kama nitakuwa na mfahamu baba yake, ila omba asikutane na waharifu kama wakina Eric” alisema mzee Haule huku wanazidi kutokomea upande wa seed farm.***
Naaaaaaaam!, Insp Aisha Amary mida hii, akiwa amevalia suruali yake nyeusi ya kitambaa chepesi, shat la blue na jacket la baridi, alikuwa anatembea taratibu, kuingia makao makuu ya jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma, huku kichwani mwake anawaza juu ya maisha yake ya mausiano, maana licha ya kuwa na umri wa miaka 27, lakini akuwana ata rafiki wa kiume.
Siyo kwamba hapakuwa na wanaume wanao mfwata na kumtongoza, la asha, Insp Aisha alikuwa anatongozwa na wanaume wengi sana, asa ukizingatia walikuwa wanajuwa fika kuwa hakuwa na mwanaume.
Shinda nikamba, wengi walio mtongoza, walikuwa katika mausiano, yani kama siyo mchumba, basi mume wa mtu, kitu ambacho yeye akukubaliana nacho, maana mpango wake kwa sasa ampate mwanaume mwaminifu, ili aowane nae.
Ukiachilia kutamani kuolewa, kutokana na umri kuzidi kusonga mbele, akiwa ajapata mtoto ata moja, pia mwanadada huyu, alikuwa na wakati mgumu sana, wakupandana na hamu ya dudu.
Maana kuna wakati ambao, alikuwa anashikwa na hamu kali sana, kiasi cha kufanya kila analoweza ili kupunguza kiu yake, kitendo ambacho alikuwa anakichukia kila anapomaliza kukitenda.
Wakati Insp Aisha alievalia viatu vyeusi vya ngozi, vyema nyayo msawazisho, akiwa kwenye mawazo, huku anaingia kwenye lango la makao makuu ya polisi, mala Insp Aisha anashtuliwa na ngurumo ya gari toka nyuma yake, anasogea pembeni kidogo, kupisha gari ilo.
Lakini anashangaa gari linasimama pembeni yake, anageuka kulitazama, analiona gari la ASP Zamoyoni, “ungeniambia kama unakuja mwenyewe, ujuwe ndio natoka nyumbani kwako sasa hivi” alisema ASP Zamoyoni kwa sauti yenye lawama.
“lakini hukuniambia kama utakuja kunifwata” alisema Insp Aisha, ambae alikuwa amesimama karibu na gari, aya basi twende kwenye uwanja waparade tukamalizane nao, tujuwe tuna ishije usiku waleo” alisema ASP Zamoyoni Mpeta, huku anaondoa gari na kwenda kuweka kwenye maegesho.***
Yaaaaaaap!, sasa twende matogoro njia panda ya barabara ya mahilo na ile ambayo inaelekea kwa mkwawa, ni mtaa ambao umepoa kidogo, ni kutokana na kuwa hapakuwa na nyumba nyingi wala duka la biashara.
Wanaonekana watu wachache wakiwa kwenye nyumba zao, wanaendelea na shughuri zao, kasoro kwenye nyumba moja kubwa kiasi, ambayo inaonekana hipo kimya kabisa, pasipo dalili ya kuwepo mtu ndani yake.
Dakika chache baadae, tunaliona gari aina ya Toyota Hiace, likuja kwa speed kali na kusimama nje ya nyumba ile tulivu, pasipo kujaei mauwa yakupandwa waliyo kanyaga.
Hapo mlango mkubwa wagari ili, na ule wambele wa dereva inafunguliwa, kisha wanashuka vijana watano, walio shikilia chupa zao za pombe na misokoto ya bangi, ikiwa inamikononi na modomoni mwao inafuka moshi.
“Tiba uba uhakika ndio hapa, mbona kama hakuna mtu?” anauliza Kubaga, kwa sauti yenye mashaka, “ndio hapa bwana, ila nazani mama yake ajatoka shuleni yeye ni mwalimu wa shule ya mahilo” alisema Tibasana.
“hapa hakuna dalili ya uwepo wa mtu yoyote” anasema Lukas ambae anaonekana kuwa na mashaka flani, “ila nikuambie kitu kubaga, huyu demu atakuwa ameenda bombambili, kwa rafiki yake Hidaya, twende kwa shemeji kule ofisini atakuelekeza kwa Hidaya” alisema Lukas huku anarudi kwenye gari.
“anabahati yeye na mama yake mdogo, leo ningemla huyo mmama” anasema Tibasana, huku wanarudi kwenye gari na gari linaondoka kwaspeed kurudi lilikotoka.***
Huko makao makuu ya jeshi la polisi, Insp Aisha Amary na ASP Zamoyoni, wanaonekana wakiwa wanatembea taratibu kutoka kwenye uwanja waparade, ilionyesha kuwa parade fupi ya maandalizi ya zamu ya usiku, ilikuwa imesha malizika.
“nazani tuvute muda kidogo, twende nyumbani kwangu tukale” anasema ASP Zamoyoni, huku wanasogea kwnye maegesho ya magari, “kuna chakula gazi cha kuzidi kunacho kufanya unipeleke kwako usiku huu” anauliza Insp Aisha kwa utani.
“wifi yako amepika pilau, umesahau asubuhi tumenunua viungo pale sokoni” anakumbusha ASP Zamoyoni, “hooo!, hapo umeniwezea, tena inabidi twende mapema aswaaa” anasema Insp Aisha kwa sauti iliyojaa utani, wanakaa kwenye benchi dogo, karibu na maegesho ya magari.
“basi tuzuge kidogo, gari la doria likiondoka tu, twenzetu” alisema ASP saa nne hakuna lolote, naenda zangu kulala” alisema Aisha, “poa, mimi nitakupeleka tu, alafu nitakuja kukaa mpaka saa sita” alisema ASP Zamoyoni.***
Naaaaaaaam!, kijana mwanadada Anastansia, akiwa anatembea taratibu sambamba na kijana mpole, wanatembae kimya kimya, hadithi zilikuwa zimesha koma, kila mmoja anawaza la kwake moyoni.
Anastansia anawaza kuhusu kijana huyu mpole, anamatamani kutengeneza urafiki zaidi, maana licha ya kuwa kijana huyu siyo muongeaji, lakini amejikuta anapenda kuwa nae, “nitakuwa nakuja kwako, mala kwa mala” anasema Anastansia, huku anacheka kidogo, “karibu” alijibu kijana mpole,.
Wanatembea tena mita kadhaa wakiwa kimya, sasa walikuwa wanaacha mtaa wa seed farm A, na kuingia eneo lenye mingomba mingi sana na bwawa la maji taka, “pia ukiwa unaitaji kitu chochote, usiogope kuniambia, sawa dogo?” anasema Anastansia huku anamtazama kijana mdogo.
Kijana mdogo anamtazama Anastansia kwamacho ya kumtathmini, “unamaanisha chochote?” anauliza kijana mdogo, kwa sauti tulivu yenye kumaanisha.
Anastansia anashtuka kidogo, anahisi pengine maelezo yake yalikosewa katika utoaji, “siyo chochote, ni kile ninachoweza kukupatia” alisema Anastansia, huku wanaendelea kutembea taratibu, kwenye eneo tulivu, lenye kichaka cha migomba mingi sana.
“sawa” anajibu kijana mdogo, ambae anaonekana akitazama mbele, kusikiliza ngurumo ya gari iliyokuwa inasikika kwa fujo ikitokea mbele, Anastansia anamtazama kijana mdogo, “sasa wewe ulizania nimekuambia ukitaka nini?” anauliza Anastansia huku anacheka kwa aibu, hakika ajawai kuzungumza jambo lenye mlengo kama huu, kwa miaka miangi sana.
Lakini kijana mdogo ajibu kitu, zaidi anaendelea kusikiliza sauti ya ngurumo ya gari, ambalo liliashiria kuwa linakuja kwa fujo sana, maana sasa lilioanza kuonekana vumbi kwa mbali, nivugumu kuliona gari, maana mbele kulikuwa na kona.
Anastansia anatazama kule anakotazama kijana mpole, nae anaona vumbi, lakini anaona hakuna sababu ya kushangaa, maana niwazi kuna gari linakuja, anamtazama tena kijana mdogo, “lakini dogo ujaniambia unaitwa nani” alisema Anastansia safari hii akimgusa bega kijana huyu, ambae kwa haraka alikuwa amemzidi kidogo kimo.
Naaaaaam!, wakati Nancy anasubiri jibu toka kwa kijana mpole, ghafla mbele yao analiona gari Toyota hiace, likiwa linakuja usawa wake, likiwa katika mwendo mkali sana. . ……..Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

