TOBO LA PANYA (25)

SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE: Naaaaaam!, wakati Nancy anasubiri jibu toka kwa kijana mpole, ghafla mbele yao analiona gari Toyota hiace, likiwa linakuja usawa wake, likiwa katika mwendo mkali sana. . ……..Endelea ….

“mamaaaaaa!” Nancy anapiga kelele za uoga, huku amefumba macho, akijuwa fika kuwa, sekunde chache mbele anazolewa na gari lile, na pengine ndiyo mwisho wa uhai wake, au ndio mwanzo wa kuwa na kilema cha kudumu, maana hakuwa na ujanja wakulikwepa lile gari, ambalo muda mfupi uliopita waliliona likija upande huu.

Lakini ile kufumba na kufumbua, Anastansia alishtuka akiwa ameshika mkono kwanguvu na mkono wenye nguvu, na kuvutwa pembeni, akikwama kwenye kifua cha kijana mdogo, huku wakienda kwapamoja pembeni ya barabara, huku upepo mkali wa gari, ukiwapitia pembeni yao, sambamba wingu kubwa la vumbi.

“kum… make nyie, mnaleta ujinga barabarani” ilisikika sauti yakiume ikipaza toka kwenye gari, ambalo sasa lilisikika likipunguza mwendo, na kwenda kusimama mita kama hamsini mbele.

Vumbi bado limetanda, Anastansia yupo kifuani kwa kijana mdogo, anatetemeka kwa uoga, kutokana na ajari iliyo mkosa kosa, bado ajaelewa kijana mdogo amefanyaje, mpaka ameweza kummwokoa, anajisikia amani kuwepo kifuani kwa kijana huyu, na wakati huo huo, anasikia ngurumo ya gari lile, likirudi nyuma, kuja pale walipokuwepo wao.

Anastansia anafumbua macho yake, anaona vumbi limeondoka, lakini pia anaona gari linawasogelea, na kuja kusimama usawa wa pale, walipokuwepo wao, “mungu saidia yasitokee mabaya” Nancy alimsikia kijana mdogo akiongea kwa sauti ya chini, huku anamwachia toka kifuani mwake.

Nancy anamwonea huruma kijana huyu mdogo, anahisi kuwa, anawaogopa wamiliki wa gari lile, na alishamwambia kuwa apendi uchokozi, hivyo Nancy anajivesha ujasiri, nakuligeukia lile gari, “hivi unawezaje juendesha gari kama unatumia barabara oeke yako?” anaongea kwa ukali mwanadada huyu mrembo, huku analisogelea gari.

Lakini Anastansia simama gafla, ni mala tu anapo ona, milango ya gari lile inafunguliwa, kisha wanashuka vijana watano, waliovalia kimaridadi, ambao mikononi mwao, wameshikilia chupa za pombe, na misokoto ya sigara ambazo, mwonekano wake unamtia mashaka, licha ya kwamba, yeye siyo mvutaji, wala ajawai kuwa karibu na wavutaji.

“hooooo!, jamani niliwaambia huyu demu ni mkali kinyama, macho yangu ayaongopi” alisema mmoja kati ya wale wanaume, ambae alishuka toka kwenye seat ya dereva, huku anamsogelea Anastansia.

Anastansia anaona hali ya hatari mbele yake, anapoteza ule ujasiri aliokuwa nao, anaanza kurudi nyuma taratibu, huku kimbilio lake likiwa ni kwa mwanaume wapekee aliekuwa nae pale, ambae ni kijana mdogo, japo alikuwa anajuwa kuwa, kijana huyu mpole, akuwa na uwezo wa kumsaidia ata kwa nukta moja, na pengine angepigwa, na kisha yeye kufanyiwa jambo lolote baya, mbele ya kijana huyu.

“dah!, ebwana eeeee, sijawai kumwona demu mkali kama huyu, hivi wanajifichaga wapi watoto wazuri kama awa” anasema mwingine, huku wengine wakiwa wamesimama ubavuni mwa gari, wanamtazama mwenzao yule dereva, aliekuwa anamfwata Anastansia, ambae sasa alikuwa amemfikia kijana mpole, na kusimama nyuma yake.

“huyu anafaa kuwa na mnyamwezi kama mimi” alisema yule dereva, huku anazidi kumsogelea Anastansia, ambae alikuwa nyuma ya kijana mpole, akitetemeka kwa uoga, maana alijuwa kuwa kwa uzuri aliona nao, lazima angechukuliwa na vijana hao na kwenda kubakwa.

Anastansia anamwona yule kijana ambae alikuwa ameshikilia bangi kwenye mkono wa kushoto, akiwafikia pale walipokuwepo na kunyoosha mkono wake wakulia, kumshika Anastansia, ambae anakwepa kwa kuzunguka upande wa kushoto wa kijana mpole, ambae muda wote alikuwa anamtazama kijana huyu, pasipo kusema neno lolote.

“mrembo acha usumbufu, leo utakuwa na mimi, achana na huyu fala, awezi kukusaidia kwa lolote” alisema yule dereva, huku ananyoosha tena na safari hii alifanikiwa kumshika Anastansia, “niache bwana” anasema Anastansia, kwa sauti ya kupiga kelele, huku anajipapatua mkono wake toka wka kijana huyu, ambae mimi na wewe tunamfahamu kama Lukas, yani mdogo wa Tino Nyondo.

Anastansia anajibanza tena ubavuni kwa kijana mdogo, maana ndio sehemu salama pekee aliyo iona, “Luka vipi tuja tukusaidie tumpakize kwenye gari?” aliuliza kubaga, ambae alikuwa ubavuni mwa gari na wenzake watatu.

“anawezaje kunishinda demu, nampakiza mwenyewe kwenye gari, siwezi kumwacha demu mkali kama huyu” alisema Lukas, huku ananyoosha mkono, kumshika tena Nancy, ambae sasa alisha kata tamaa, na kuona kuwa anachukuliwa na kwenda kubakwa.

Lakini chakushangaza, nasi anamwona kijana mpole anazuwia mkono wa yule kijana dereva, Nancy anamtazama kijana mpole, kwa macho ya mshangao, akitaka kujuwa ujasiri huu ameutoa wapi, “kaka nivyema kama mtaondoka, ilikuepusha matatizo” Anastansia anamsikia yule kijana akiongea kwa sauti ya upole.

Hapo vinasikika vicheko vya dharau, toka kwa wanaume wote watano, “hahahahahahahaaaaaa!” wanacheka wakina Lukas, “mnamsikia huyu fala, ebu pisha kabla sijakupasua” anasema Lukas kwa sauti yenye jazba, kiasi cha kumtisha Anastansia.

Lakini kijana mdogo akuonyesha wasi wasi wowote, “jamani nyie ni vijana wadogo, msitafute matatizo, nivyema mkaondoka zenu kwaajili ya usalama wenu” alisema kijana mpole, kwa sauti ya upole, yenye kutasharisha, ungesema anamshauri mtu mwema, katika hali ya usalama.

“mjinga wewe, unaniwekea usiku” alisema Lukas huku anajipapasa kiunoni na kutoa bastora yake, kisha akaelekeza kichwani kwa kijana mdogo, hii iliwashtua ata wakina kubaga, ambao waliamini kuwa, muda wowote Lukas anasababisha maafa.***

Naaaaaaa!, kule makao makuu ya jeshi la polisi, wakiwa na dakika chache toka wamekaa pale kwe benchi, karibu na maegesho ya magari, mala wakina Insp Aisha na ASP Zamoyoni, wanaliona gari moja la polisi aina ya land rover mia defender, linaingia huku likiwa na askari kadhaa wenye silaha.

Inaoyesha wazi kuwa, wametoka kwenye jukumu flani, la dharula, nao wanahamu ya kufahamu jukumu lililowatoa askari wale, ambao kikawaida walitakiwa wawe wamaesha pumzika majumbani kwao, wanalitazama gari lile ambalo lina simama na askari wanaanza kushuka.

Lakini wakiwa katika matamanio hayo, mala wanamwona askari mmoja mtu mzima, mmoja kati ya wale askari, walioshuka toka kwenye gari, aliekuwa na cheo cha sajent, alikuja upande wao, wakaona lengo lao litafanikiwa.

“habari za jioni afande” anasalimia yule sajent, kwa saluti ya kijeshi, huku anakatiza mbele yao, “salama mzee Komba, vipi mlikuwa na operation gani huko?” anauliza ASP Zamoyoni, ambae kikawaida ni mkubwa kicheo kwa huyo bwana Kombo.

“kuna tukio mto mateka, tumeokota mwili wa mtu mmoja alie uwawa kwa kuchomwa na uma wa kulia chakula shingoni” alijibu sajent Kombo, “mh!, hakuna mshukiwa mlie weza kumpata?” anauliza Insp Aisha kwa sauti yenye udadisi, na masikitiko.

“haa!, Afande, kiukweli inabidi tuifanye kama vile hakuna mshukiwa, maana imebainika kuwa, marehemu ni mfanyakazi wa bwana Tino Nyondo, na tulipotoa taarifa kwa OC FFU, akasema tuandike kuwa marehemu ni mtu asie julikana” anasema sajent Kombo, kwa sauti ya masikitiko. ……..
….
MWISHO SEASON ONE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata