TOBO LA PANYA (36)

SEHEMU YA THELATHINI NA SITA

ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA TANO: Lakini katika hali isyo ya kawaida, kumbu kumbu zote za SA-26, zikatoweka, kuanzia taarifa zake, mpaka picha na maelezo binafsi ya kijana huyu, ambazo zilitunzwa kwenye computer za makao makuu ya TSA, haikujulikana ninani alie futa kumbu kumbu izo. ……Endelea ….

Hapakuwa na namna, zaidi ya kutumia kumbu kumbu chache, toka kwa mashuhuda wa karibu wa SA-26, kwaajili ya kumtafuta kijana huyu, ambae baada ya kukosekana jijini dar es salaam, wakaona kuwa sehemu pekee ya kumpata, inaweza kuwa ni mkoani Ruvuma, katika mji wa Songea, huku wakitabiri kuwa ata kuwa anaishi maisha ya kifahari, pamoja na wazazi wake, ambao waliamini kuwa wanaishi Songea vijijini. ***

Saa moja na dakika kumi na nane, eneo la hospital ya mkoa wa Ruvuma, magari matatu, yanaingia kwa fujo na kusimama nje ya jengo la utawara, leo gari aina range rover, lililokuwa katikati, milango miwili yote inafunguliwa kwa pamoja, kama ilivyokuwa kwa magari mengine mawili aina ya land cruiser.

Watu wote wanashuka toka kwenye magari, nakuacha madereva peke yake, leo ata Tino Nyondo Nyondo alie shuka kwenye range rover, akusubiri kufunguliwa mlango, alifungua mwenyewe na kushuka, kisha akaanza kutembea kuelekea ndani, ya jengo la utawara, akiongozana na vijana wake saba.

Bwana Nyondo anatembea kwa haraka mpaka mapokezi, ambako anakuta pana watu wachache sana, akiwapo na muuguzi katika dirisha la huduma, “niambie vijana wangu wako wapi na wamepatwa na nini” alisema Tino Nyondo, huku anasimama mbele ya dirisha la huduma.

Muuguzi wa kike, anamtazama Nyondo, huku anajiuliza, ni vijana gani, anazungumzia, “samahani hao vijana kama ni wagonjwa, nipatie majina yao, niwatazame kwenye kitabu” alisema yule mwanamke, huku anamtazama Nyondo, ambae kiukweli licha ya umaarufu wake, lakini aikuwa lahisi kumwona mala kwa mala na kumfahamu.

“kwahiyo wewe ujuwi wagonjwa wanao letwa hapa, mpaka mimi ningaike…” alisema Nyondo kwa hasira, huku anajipapasa kiunoni, na kuigusa bastora yake, kila mtu akajuwa kuwa yule binti hakuwa na bahati.

Lakini kabla ajaichomoa bastora, ilisikika sauti yakiume toka upande wa majengo yenye ward za wagonjwa, na vyumba vya matibabu, “mheshimiwa, karibu sana, pia pole kwa tatizo ili”.

Nyondo na vijana wake wote, wanageuka na kutazama upande ilikotokea sauti, ambako wanamwona RCO Zamoyoni, akiwa anakuja upande wao, akitokea kwenye chumba cha kulaza wagonjwa wa mivunjiko, kwamaana walio pata ajari mbali mbali.

“yupo wapi Luka?” anauliza Tino Nyondo, huku anatembea kumfwata Zamoyoni, ambae wanakutana katikati, Zamoyoni anashusha pumzi nzito, anainamisha kichwa chini kwa masikitiko, huku anaonyesha chumba cha alichotokea yeye.

Tino Nyondo aongea neno jingine, anaanza kutembea kwa haraka, kuelekea kwenye kile chumba, alichoonyeshwa Zamoyoni, akifwatiwa na vijana wake, huku Zamoyoni akiwa amesimama pale pale, akiwatazama watu awa, “kazi hipo” anajisemea Zamoyoni, huku aanza kutembea taratibu kuelekea nje ya eneo la utawara.

Nyondo na vijana wake wanaingia ndani ya chumba kile ambacho, wanakuta kuna vitanda nane, chumba kizima, huku vitanda vitano vikiwa vime laliwa na watu, kimoja kati yake kikiwa kimelaliwa na mtu alie funikwa mwili mzima, huku vijana wengine wakiwa wamefungwa bandage ngumu, kwenye sehemu mbali mbali za miili yako.

Nyondo akiwa mwenye hofu kuu, anatazama kitanda kimoja baada ya kingine, akitazama kama anaweza kumwona mdogo wake Luka, lakini akumwona Lukas miongoni mwao.

Tino Nyondo anatazama kitanda cha pembeni, alicho lalia mtu aliefunikwa mwili mzima, kisha anaanza kutembea kwa haraka, kukifwata kitanda kile, huku mapigo yake ya moyo yakizidi kwenda mbio, ata alipofikia kitanda, Tino Nyondo akafunua lile shuka.

Alicho kutana nacho kilimfanya simame kwa sekunde kadhaa, akikodoa macho ya kuto kuamini, huku kichwa chake kikianza kuwa kizito, ikimsababishia kuanza kuyumba kama mtu alie kunywa pombe nyingi.

Nyondo anajaribu kujishika kwenye kitanda cha jirani, lakini anashindwa kukifikia kutokana na umbali wa sehemu kilipo kitanda, nakuanza kuelekea chini, lakini Kichondo anawai na kumdaka kabla ajafika chini.

“niache we mpuuzi” anasema Nyondo, huku anajiweka sawa na kushikilia kichwa chake, ambacho sasa alianza kuhisi maumivu kwambali, “ni mshenzi gani huyu mwenye jeuri ya kumuuwa mdogo wangu” alisema Tino Nyondo, kwa sauti iliyo ambatana na kilio cha wazi kabisa, kilio kilichobeba machungu.

Hakuna alie mjibu, zaidi kila mmoja alitabiri hatari inayo fwata, kwa mtu alie fanya kitendo hicho, “nauliza nani huyu alie fanya hivi?” aliuliza Nyondo, huku anasogelea kitanda cha jirani, na kutoa kigemeo cha drip, alafu anainua juu na kuishusha kwenye kitana alicho lalia Adam Mwakaleja.

Ile antenna inashuka sawia kwenye mguu wa Mwakaleja, ulio filigiwa bandeji, na kumfanya Mwakaleja aachie yowe kali la kilio, “mamaaaaaaa!” akionyesha wazi kuwa alisikia maumivu makali.

Aikusadia kitu, “nauliza mlikuwa wapi wakati Lukas anauwawa” alisema Nyondo kwa sauti ya ukali, huku anashusha mvua ya kipigo kwa Mwakaleja, “boss, naomba utusikileze kidogo, huyu jamaa ni hatari sana” alisema Kubaga, ambae alikuwa amelala kwenye kitanda cha tatu kutoka alipolala Mwakaleja.

Tino Nyondo Nyondo anasitisha kipigo, na kumtazama Kubaga, “ni nani huyu mjinga, anae diliki kufanya hivi, pasipo kuniogopa ata kidogo?” aliuliza Nyondo, ambae alionekana kuwa na hasira na uchungu mwingi sana.

“kiukweli boss, ata sisi hatumjuwi, ila alikuwa na mwanamke mmoja hivi wa pale chuo cha ualimu” alieleza Kubaga, kwa sauti iliyo jaa tahadhari, “mwanamke gani huyo, namtaka sasa hivi, akaonyeshe huyo mpuuzi anakoishi” alisema Nyondo, kwa sauti ile ile yenye hasira.

“nilisha wai kumwona mara kadhaa, ni mzuri sana, nikimwona siwezi kumsahau” alisema Kubaga, “pasipo kujari hali yako, utaondoka na wakina Mbwilo, hakuna kurudi mpaka huyo mshenzi amepatikana” alisema Nyondo, huku kisha akamtazama Mbwilo.

“namtaka huyu mshenzi, usiku huu, tena akiwa mzima, nataka nimkate kipande moja baada ya kingine, kisha na mzika kwenye kaburi atakalo zikiwa Lukas” alisema Nyondo, kabla ajaanza kutembea kutoka nje ya jengo lile.****

Wakati huo huo mbezi dar es salaam, nyumbani kwa bwana Kingumwile, mkulugenzi wa TSA, kanda ya mashariki, ambae alikuwa sebuleni kwake, pamoja na familia yake, mke na watoto wakitazama vipindi vya habari mbali mbali, kwenye television.

Huku bwana kingumwile, akiwa amesimama kwenye kona moja ya sebule ile kubwa, ameshikilia mkonga wasimu sikioni mwake, “sikiliza kwa umakini, fanya kila unachoweza, kuhakikisha huyo mwanamke anakuwa salama, na usalama wake hupo mikononi mwa Panya, ni hatari sana endapo huyo mwanamke atapatikana na hao watu au TSA, lazima ataeleza kuhusu Panya” hayo ni baadhi ya maneno ya Kingumwile, ambae aliongea kwa sauti ya chini.

Baada ya kumaliza kuongea na na simu ile, na kukata simu, kingumwile anapiga namba nyingine na kuweka mkonga sikioni, anasikilizia simu inaita kwa sekunde kadhaa, lakini aikupokelewa inakatika, nae anapiga namba nyingine, nayo inaanza kuita mara moja. ……Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata