
SEHEMU YA THELATHINI NA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA SITA: Baada ya kumaliza kuongea na na simu ile, na kukata simu, kingumwile anapiga namba nyingine na kuweka mkonga sikioni, anasikilizia simu inaita kwa sekunde kadhaa, lakini aikupokelewa inakatika, nae anapiga namba nyingine, nayo inaanza kuita mara moja. ……Endelea ….
Yaaaaap!, ASP Ayoub Mzee na Insp Aisha wanaingia kwenye lango la kuu la hospital ya mkoa, wakiwa ndani ya gari lao, aina ya Toyota crester, na kwenda kusimama mbele ya jengo la utawara, pembeni ya magari matatu, mawili ya kiwa ni Toyota land cruiser na moja likiwa ni range rover, tena yakiwa yana unguruma, ikionyesha kuwa mida wowote yanaweza kuanza safari.
“tayari moto umewaka, jamaa yupo huko ndani” alisema ASP Ayoub Mzee, huku anashuka toka kwenye gari, bila kuzima engine ya gari, “wanawezaje kumpata muuwaji ingawa ata sisi wenyewe atujamwona” anauliza Aisha huku na yeye anafungua mlango na kushuka toka kwenye gari.
“unazani awawajuwi maadui zao, lazima watakuwa wanajuwa waanzie wapi…..” anasema ASP Ayoub Mzee, huku anaanza kutembea kwa haraka, kuingia kwenye jengo la utawara la hospital, Aisha akumfwata nyuma, lakini wakati huo huo, ASP Ayoub Mzee anasitisha maongezi, huku anatumbua macho mbele yao.
“hoooo! matatizo” alisema Ayoub Mzee, kwa sauti ya chini, Aisha anatazama mbele, na kuona kundi la wanaume zaidi ya kumi, waliokuwa wanakuja mbele yao, mmoja wao akiwa anasaidiwa kutembea, kwamaana ya kwamba alikuwa mgonjwa tena wa viungo vya mwili.
“inamaana huyu mzee ndio Nyondo mwenyewe”? anauliza Aisha, kwa sauti ya chini, yenye tahadhari, lakini kutokana na ukaribu waliokuwa nao na wale watu, ASP Ayoub Mzee anashindwa kujibu, swali la Insp Aisha.
“sikia Mbwilo, nenda na vijana watatu huko chuo, mkaniletee huyo mwanamke, yeye ndie atakae nieleza huyo mpuuzi anapatikanaje” Aisha na Ayoub Mzee waliweza kunasa, maongezi ya wakina Nyondo, wakati wanapishana.
“boss nakuhakikishia huyo mpuuzi namleta kwako usiku huu” alisema mmoja kati ya wanaume wale, kwa sauti ya kujiamini, na pasipo kuonyesha kama wanawajari wakina Aisha na Ayoub Mzee, “kumbuka kuwa, namtaka akiwa hai, nataka nimtoe roho mimi mwenyewe” wakina Ayoub Mzee waliweza kumsikia mzee Nyondo, akiongea kwa sauti yenye hasira kali sana.
Safari ya wakina Insp Aisha, inaishia mbele ya jengo la kulazia wagonjwa, ambako wanashindwa kujuwa elekee wapi, “hivi afande, umesikia alichosema yule mzee?,” anauliza Aisha huku wanageuka na kutazama walikotoka, ambako kwa pamoja wanaweza kuwaona wale wanaume walioongozana na mzee Nyondo, wakiingia kwenye magari yao.
“wanaenda chuo cha walimu kumfwata mwanamke” anajibu ASP Ayoub Mzee, kwa sauti ya chini, kama anajiongelea peke yake, ni mwanamke gani huyo unazani?” anauliza Insp Aisha, huku anamtazama ASP Ayoub Mzee, ambae pia alimtazama Aisha, kwa sekunde kadhaa, kama vile wote walikuwa wanatafakari kitu ambacho wamesha kipatia jibu.
“ni yule mwanamke, aliekuwa na yule kijana mpole” wote walitoa jibu kwa pamoja, kisha bila kujiuliza mala mbili, wakaanza kutembea kwa haraka kuelekea upande wa nje, yani walikotoka, ambako sasa magari matatu, yalisikika na kuonekana ya kiondoka zake.
“ikiwezekana tuvuruge wasiweze kumteka, huyu binti, uazani watamfanya nini wakimpata” alisema Aisha, ambae alionekana wazi kuingiwa na moyo wa imani zidi ya mwanamke mwenzie, “ni wakatili sana awa jamaa, wanaweza kumzuru sana yule mwanamke” alisisitiza ASP Ayoub Mzee, huku wanaongeza mwendo kuwai nje ya jengo.
Wawili awa wanatembea kwa haraka, mpaka nje, ambako kabla awajagusa milango wa gari lao, “afande Mzee, mnaitwa na afande Zamoyoni pale kwenye gari” ilisikika sauti ya mwanaume toka upande wao kushoto.
Nao wanageuka, kutazama kule waliko ambiwa kuna gari, wanaliona gari aina ya land rover defeder rangi nyeupe, lenye namba za kiraia, ambalo wanalilifahamu mala moja, kuwa linatumiwa na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai, wa mkoa wa Ruvuma, yani RCO, ambae ni bwana Zamoyoni Mpeta.
“dah! tayari kimeo kimeingilia kati” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti ya chini, yenye kukata tamaa, “inamaana alikuwepo hapa na huyu mzee mshenzi?” anauliza Insp Aisha, huku wote wanaanza kutembea kulifwata gari la mkuu wao, wakitengo cha upelelezi.****
Naaaaam! sasa tupo mtaa wa mabatini, mita chache toka kilipo chuo cha ulimu, kwa upande wa kusini, na kaskazini ukipakana na kambi la jeshi la polisi, mashariki kuna shule ya msingi mahenge, ambayo pia kaskazini inapakana na mtaa mkubwa wa seed farm A.
Sisi tuna elekea upande wa magharibi wa mtaa huu wa mabatini ya matogoro, upande ambao, mtaa huu umepakana na mtaa wa mahenge, huku mitaa hii miwili ikipakanishwa na bonde dogo, ambalo utililisha maji kwamisimu yote ya mwaka.
Kando kando ya bonde linalo pakanisha mabatini na mahenge, tuna weza kuona nyumba kadhaa za kifahari, ambazo pia zimejengwa kwa kuachiana nafasi kubwa sana, huku kila nyumba, ikiwa na eneo lenye ukubwa wa nusu hekari.
Sisi tunaenda moja kwa moja, kwenye nyumba ya mwisho ya upande wakulia, kabla ya kijingia kchembamba, kinacho tumiwa na watembeao kwa miguu, kuvukia upande wapili, yani mtaa wa mahenge.
Huko tunaingia kwenye jumba la kifahari la mzee Johnson, ambae alistaafu ghafla serikalini, huku maisha yake yakibadirika ghafla, toka kwenye hali ya kati, na kuwa ya kifahari kiasi, wengi wakihisi kuwa ni sababu ya fedha alizo lipwa kwa kustaafu kwake, japo wengine walisema kuwa fedha ya kustaafu isingekizi mafanikio yale ya mzee Johnson.
Nje ya nyumba hii kubwa ya kifahari, upande wa mbele, palionekana magari mawili ya kifahari, moja likiwa ni zusuk pajero, na BMW, yote yakiwa mapya kabisa, tofauti na gari mbili zilizo kuwepo ubavu wa kushoto wa nyumba hii, ambayo ni Toyota hilux na land rover mia na kumi.
Ndani ya nyumba hii ya kifahari, ilikuwa na watu wanne tu, yani mzee Johnson mwenyewe, mke wake, na waschana wawili, ambao ni wafanyakazi wandani, kwamaana hapakuwa na ndugu wala mtoto wa familia hii, aliekuwa anaishi hapa.
Mida hii, mzee Johnson na mke wake, yani wazee wenye nyumba hii, walikuwa sebuleni, wanasiliza kipindi cha michezo cha redio ya taifa, ikiwa ni maandalizi ya kusikiliza taarifa ya habari, toka kituo icho cha redio, wakati huo, mschana moja wakzi akiwa anaandaa chakula kwenye meza kubwa ya chakula.
“baba Hance, naona kama kama vile, leo Hance amechelewa kupitia hapa nyumbani, au hakuwa na ratiba hiyo” alisema mke wa mzee Johnson, kwa saui yenye wasi wasi mwingi, huku anamtazama mume wake, ambae anamwona anainua mkono wake wa kushoto, na kuitazama saa yake mkononi, nae akionyesha wasi wasi usoni mwake.
“saa mbili kasoro tano, siyo kawaida yak…..” kabla mzee Johnson ajamaliza kusema alichokuwa anasema, mala wakasikia sauti ya mschana wakazi, upande wa mlango wa jikoni, uwa tunaita uwani. ……Endelea …. kufwatilia mkasa huu wa #TOBO_LA_PANYA, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU