TOBO LA PANYA (40)

SEHEMU YA AROBAINI

ILIPOISHIA SEHEMU YA THELATHINI NA TISA: Lakini kabla Nancy ajaona nini kinatokea baada ya watu wale kumfikia mlinzi, mara ghafla anashtuka akiwa ameshikwa mkono, na mtu toka nyuma yake, kitendo ambacho kilimshtua vibaya sana, halimanusla aanguke kwa kihoro, anageuka kumtazama alie mshika mkono……Endelea ….

“Farida jamani, umenishtua sana” anasema Anastansia, huku anashusha pumzi nzito ya kujitoa kwenye hofu, “Nancy, hapa chuoni siyo salama kwako, unatakiwa kuondoka haraka sana” alisema mwanadada Farida, ambae ni mwanachuo mwenzie na Nancy, huku anamwongoza Anastansia kutoka sehemu ile ya bomba, kuelekea upande wa barabara kupitia kwenye uzio wa miti mifupi.

“unanipeleka wapi Farida, kwanini hapa chuo siyo salama kwangu?” anauliza Nancy, kwa sauti yenye hofu kubwa, huku anamshangaa Farida, kwa macho yenye viulizo, “mtu mlie muuwa kaka yake ni mtu hatari sana, lazima atokaa kimya, atakutafuta mpaka akupate” alisema Farida, ambae mpaka sasa tunamtambua kuwa, ni mwanafunzi wa hapa chuoni.

Inamshtua sana Anastansia, ambae anasimama na kujaribu kujipapatua mkono wake toka kwa Farida, na kufanikiwa, “we ninani, na umejuwaje hayo yote au ni polisi?” anauliza Anastansia, huku anapiga hatua mbili nyuma.

“acha maswali Nancy, ebu tazama kule getini” alisema Farida akionyesha mkono, upande wageti dogo, ambako pia Anastansia alitazama, ambako anawaona watu wawili walioshuka kwenye gari wanabishana na mlinzi wa getini, kabla ya kuanza kumshushia kipigo.

“mbona wanampiga mlinzi?” analiza Anastansia, huku macho yamemtoka kwa uoga, “hao wanakutafwata wewe, ni lazima uondoke mahali hapa” alisema Farida huku anaushika mkono wa Anastansia, na kuanza kutembea, kuifwata fensi ya niti ya chuo iki, safari hii, Anastansia alifwata bila ubishi.*****

Naaaaaam!, tukiwa hapa hapa maeneo ya chuo cha uhalimu, mita chache toka geti dogo la kuingilia pale chuoni, tuna mwanaume mmoja mtu mzima, alie valie mavazi chakavu, huku akiwa anakokota kipando chake cha baiskeri, iliyobebeshwa furushi lililojaa vyema, japo aikuonekana kumpa shida, sababu kwa ujazo ule, ilipaswa kuwa ni mzigo wa kilo zaidi ya hamsini.

ikionyesha wazi kabisa, alikuwa amechelewa sana, toka katika shuguri zake za shamba, ambayo muda wa mwisho kabisa ni saa kumi na mbili za jioni, ambae sasa alikuwa amesimama anatazama upande wa geti dogo, ambako vijana wanne, walikuwa wanamaliza kushusha kichapo kwa mlinzi, ambae wali hakikisha amelalachini hoi bin tahabani.

Kisha wanaonekana vijana ale wanne anaingia ndani ya gari, na kuondoa gari kwa mwendo mkali sana, kuingia ndani ya eneo la chuo, ikionekana wazi kuwa hapakuwa na usalama huko ndani.

Nikweli hapa kuwa na usalama ata kidogo, maana gari linaenda kusimama mbele ya jengo kubwa lililoandikwa UKUMBI WA MAHAKULI, ambako palikuwa na watu wachache, waliokuwa wanapata maitajio madogo madogo.

Na wakati huo, wanafunzi wawili waliokuwa wamesha maliza kupata maitajio yao, waliongozana kutoka nje ya ukimbi, wakiongea na kimahaba na kucheka kwa pamoja, vicheko vyenye furaha tele, ni wazi walikuwa wanamausiano ya kimapenzi.

Lakini ile wanauvuka mlango wa ukimbi, wanakutana na wakina Mbwilo, waliokuwa wanaingia ukumbini, “we binti, tueleze Anastansia Anthony, yupo wapi” alisema Mbwilo, huku anamshika mkono yule mwanamke, na kumvuta kwake kwanguvu.

Kilikuwa ni kitendo cha ghafla chenye kushangaza na kushtusha, kilicho pelekea yule kijana kutafsiri kuwa ni dharau kubwa sana kwake, “hoya bro ebu acha dharau” alisema, yule kijana, huku anapiga hatua kumsogelea Mbwilo, huku amekunja sura kwa hasira.

Lakini bahati aikuwa upande wake, maana kabla ata ajamfikia Mbwilo, tayari alishtuka akiwa amesha pigwa teke la kufua na kujibwaga chini, ile anajiandaa kuinuka, tayari ngumi mbili zilisha tuwa usoni mwake, “tulia we boya, nitakuuwa mimi” alisema mwanaume mwenye misuri, uku akisitisha kipigo usoni kwa kijana yule.

Kuona hivyo yule mwanamke, ambae alikuwa ameshikwa na Mbwilo, akajuwa ya kuwa, akifanya mchezo, basi kibaya zaidi kita mkuta yeye na mpenzi wake, wakati huo mle ndani ya ukumbi wa chakula, palikuwa kimya kabisa, kila mmoja akiwa ameshikwa na uoga mkubwa.

“Nancy alikuwa bwenini, anajiandaa kwenda kuoga, bado ajaenda darasani” alisema yule mwanamke, huku anatetemeka kwa uoga, “bweni lipi, ebu eleza haraka” alisema Mbwilo, kwa sauti yenye vitisho.

“lile pale la tatu, nime mwona sasa hivi” alisema yule mwanamke, akiona kuwa kueleza hivyo ndiyo unafuu wake, au kunusulika kwake, “hoya, atuna muda wakupote, twendeni tuka mchukuwe huyo demu, maana boss anamsubiri” alisema Mbwilo, huku anamwachia yule mwanamke kwa kumsukuma, nae anaenda kujibwaga juu ya mwanaume wake.

Wote mle ndani wanaona wale vijana wanne, wakiondoka na kuelekea upande wa mabweni, wakililenga bweni waliloonyweshwa na yule mwanamke, huyu kila mmoja alishikwa na mwaswali, nini kinaenda kumpata mwanamke mrembo mwenye kujiheshimu, huku akiwa na kumbu kumbu ya masaa machache yaliyopita, baada ya kusikika mlipuko wa risasi, na ujio wa askari wajeshi la polisi.**

Naaaaaaaam!, wakati huo huo, upande wapili, gari dogo aina ya Toyota crester, lilionekana likitimua vumbi kwa speed kali sana, kukatiza mtaa wa mabatini, na kuelekea upande wa chuo cha ualimu na uongozi wa jamii, huku wakilipita gari dogo jeusi, ambalo hawakuangaika kulitambua ni la aina gani.

Gari linatimua vumbi, mpaka linapo fika kwenye eneo la vwanja wa michezo, vya wazi, huku ndani kukiwa na Insp Aisha Amary na ASP Ayoub Mzee, “afande, ni vyema kama ukipunguza mwendo, ili tujuwe kinachiendelea, maana awa jamaa tayari wapo hapa” alisema Insp Aisha, akimweleza afande wake Ayoub Mzee. Endelea kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata