TOBO LA PANYA (42)

SEHEMU YA AROBAINI NA MBILI

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA MOJA: Wote wanatazama upande unakotokea ngurumo ya gari, wanaliona gari dogo rangi ya maziwa, aina ya Toyota crester, lililokuja karibu yao na kusimama karibu yao, “aya Nancy, ingia ndani ya gari, sasa hupo salama” anasema Farida huku anafungua mlango wa gari upande wa seat za nyuma. Endelea……..

Nancy ambae anaonekana kama analifahamu gari ili, wala kujiuliza mara mbili, juu ya nani yupo ndani ya gari, yeye akaingia ndani ya gari nakukaa seat ya nyuma, kisha akatazama seat za mbele, na kujikuta anatoa acho kwa mshangao.

Anastansia anawaona atu wawili ambao akutegemea kuwakuta ndani ta gari, watu ambao masaa machachache yaliyopita, walimuuliza kuhusu kumwona kijana alie fanya mauwaji, ni wazi kabisa awa ni polisi, ambao nao walikuwa wanamtazama kwa macho yenye tabasamu la ushindi.

Kwa haraka sana Anastansia anajaribu kufungua mlango, lakini tayari mlango ulisha wekewa lock, Anastansia anatazama nje ya gari, anamwona Farida anatokomea kwenye uzio wa miti, na kupotelea ndani ya eneo la chuo.

“nivyema ukawa mtulivu bibie, ili ujibu maswali yetu, kisha tukuachie, kwa amani” alisema Insp Aisha, kwasauti ya chini, huku anaachia tabasamu la kejeli, mpaka hapo tayari Nancy alijuwa amesha fikikia ukingoni, maana alijuwa fika kuwa awa wawili ni polisi, sasa je, inawezekana Farida nae akawa polisi.

Anastansia anatazama nje kupitia kioo cha gari ambacho kilikuwa kimepandishwa mpaka juu, anamwona Farida anatokomea kuingia kwenye uzio wa miti, ulio zunguka cho iki kikubwa na maarufu, Anastansia anaonashindwa kupiga kelele, maana alihisi kuwa Farida alifanya vile makusudi.

Anastansia anawatazama wakina Insp Aisha, “lakini siyo mimi, ni yule mkaka ndie alie muuwa yule mwanaume” alisema Nancy kwa sauti yenye wasi wasi mwingi, kiasi cha kuwfanya wakina Insp Aisha watazame kwa macho yenye mshangao, “inamaana huyu ndie mwanamke anae tafutwa na wale jamaa….” ASP Ayoub Mzee, akufanikiwa kumalizia sentensi yake.

Maana kabla ajamaliza kuongea, wote watatu, walishtuka wakimulika na mwanga mkali wa taa za gari mbele yao, lililokuwa lina kuja kwa kasi na kusimama mbele ya gari lao.

“Aisha tumekwisha” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti ya kunong’ona, iliyosikika wazi wazi mle ndani ya gari, huku wakijipapasa kwenye vungu za seat walizo kalia, ili kutoa bastora zao, kuwa wai wale jamaa kabla awajashuka toka kwenye gari lao.

Lakini tayari walikuwa wamesha chelewa, maana walishtuka vitasa vya milango ya gari lao, ina funguliwa na watu toka nje, bahati ni kwamba, walisha ilock, kwandani, na vioo vilikuwa vimepandishwa juu.

Wanapo tazama pembeni, ya mlango yote ya mbele, wanawaona vijana wawili, katika milango ya mbele yani ule wa dereva na wa abiria, huku wameshika bastora mikononi mwao, “ondoa gari afande, awa watu siyo wazuri ata kidog….” Alisema Insp Aisha.

Nikama wazo ilo tayari lilikuwa kichwani kwa ASP Ayoub Mzee, maana wakati huo huo, alikuwa tayari amesha tupia gia ya nyuma, na kukanya mafuta kwanguvu, kulifanya gari liondoke kwa speed, kurudi nyuma.

Wakati huo mwana dada Anastansia, akiwa amezidiwa kwa hofu na wasi wasi, anaomba huyu dereva, mwanaume mtu mzima, ambae ni polisi afanikiwe kuwakimbia awajamaa, ambao wanaonekana kuwa ni hatari.

Lakini basi, gari ili dogo aina ya Toyota crester, linafanikiwa kurudi mita kama kumi tu, kabla awajamwona mmoja kati ya vijana waliokuwa wamesimama mbele yao, akiinua bastora yake na kuelekeza lilipo gari, kisha ikafwata sauti ya mlipuko wa lisasi mbili mfululizo, moja ikigoga kioo cha mbele usawa wa dereva, na ya pili ikigonga tairi la mbele, upande wa kulia, yani wa dereva.

“acha ujinga Nzala, ujuwi kama huyo mwanamke yupo humo ndani, utamuuwa kabla ajatueleza huyo mpuuzi yupo wapi” alisema Mbwilo, ambae alikuwa anashuka toka kwenye gari, huku wanalishuhudia gari dogo, likikosa mwelekeo, na kuingia kwenye uzio wa miti mifupi, inayozunguka eneo la chuo.

Tayari ndani ya gari, kila mmoja alikuwa katika hali ya uoga na kuchanganyikiwa, hofu imewatawara, wanawaona wale vijana ambao sasa walikuwa wanne, wanalisogelea gari lao.

Insp Aisha na ASP Ayoub Mzee wanaangaika kufungua mikanda ya viti vyao, ili angalau wajaribu kujiokoa, huku wakimsahau abiria wao, ambae kwa asilimia mia moja, anawategemea wao kumwokoa.

Milipuko ya risasi inasambaa eneo lote la chuo na mitaa ya jirani, kama vile matogoro shuleni kanisani kwamtutuma, mabatini na kimoro, kwamaana hiyo basi, mwana dada Farida ambae alikuwa mita mita kama mia moja, toka barabarani, anaweza kusikia vyema mlipuko ule.

Farida anasimama na kutazama alikotoka, anaona mwanga wamagari mawili, ambao unaashilia kuwa, tofauti na gari alilo liacha mwanzo, sasa kuna gari jingine, na tayari mapigano yameanza.

Hivyo kwa haraka sana, anainhua gauni lake, na kuikamata bastora pajani, mwake, aliyokuwa ameibana kwenye kwenye kifuko chake, katika bukta ndogo ya kubana misuri.

Kisha ana kimbia kurudi alikotoka, akiwa mwenye tahadhari kubwa sana, anatumia sekunde chache kuufikia uzio wa miti, na kutazama upande wa nje, yani kule barabarani.

Naaaaaaam! Farida anashikwa na mshtuko mkubwa sana na kubaini kosa alilolifanya, mala baada ya kuona vijana wanne waliolizinguka lile gari dogo, wakiwaamulu watu watatu watoke nje ya gari lile.

Licha ya kumfahamu Anastansia, ambae alikuwa amevaa vazi la bafuni, lakini pia aliweza kuwa tambua askari wawili wa jeshi la polisi ambao ni Insp Aisha Amary na ASP Ayoub Mzee.

Huyu mwanamke, anaitwa Farida, ambae ni SA-54, toka ya kitengo cha mawakala wa siri wa usalama wa nchi na majukumu ya siri, kanda ya dar es salaam, ambae amejiunga na chuo iki miezi mitatu iliyopita, ikiwa ni kwaajili yale jukumu mahalumu, alilopewa na mkulugenzi wa kituo chake, cha dar es salaam, yani bwana kingumwile, kumfwatilia SA-26, kuangalia usalama wake.

Na ndie aliepewa jukumu la kuhakikisha Anastansia anafika mikononi mwa SA-26, kwaajili ya usalama wake, na kwaajili ya usalama wa siri ya SA-26, ambae ilikuwa ni lazima asiingie mikononi mwa TSA.

“ayaaaa! Kumbe nimekosea gari, nilimkabidhi Nancy kwa polisi” anajisemea Farida, kwa sauti ya chini, yenye kujilaumu, huku anawaona wale jamaa wanne, wenye silaha mikononi mwao, wakiwa wamesimama karibu kabisa na wakina Anastansia.

“kwahiyo we fala, unazani unaweza kutukimbia sisi?” aliuliza Mbwilo, kwa sauti yenye jadhba, huku anainua mkono ulioshika bastora na kuushusha usoni kwa ASP Ayoub Mzee, akitanguliza kitako cha bastora hiyo, iliyoenda kukita kwenye paji la uso kwanguvu, na kumfanya ASP Ayoub Mzee, aanguke chini kama furushi. . ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!