
TOBO LA PANYA (44)

SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TATU: Bahati nzuri kwake, wakati huo huo, Lisanga alikuwa anamsogelea kijana huyu, kwa uharaka sana, akitokea nyuma yake, na alikuwa amesha mfikia, na kumfanya Mbwilo aamini kuwa, wanaweza kumdhibiti kijana huyu mdogo, endapo wata mshambulia kwa pamoja. . . ..Endelea…….
Hivyo basi, wakati Lisanga alipokuwa anarusha ngumi kuelekea shingoni kwa kijana huyu, huku Mbwilo nae alikuwa anaanainua mkono wake wakushoto, kwa tabu kabisa, kutokana na maumivu aliyokuwa anayasikia kwenye majelaha, yaliyouwa yanavuja damu kwa wingi, kwenye mbavuni zake.
Ukweli aikuwa kama Mbwilo alivyo zania, maana ile vumba na kufumbua, alimwona yule kijana akibonyea kidogo kukwepa ngumi ya Lisanga, huku akizungusha mkono wake, nyuzi 360, ukipapasa shingo ya Lisanga, na mkono huo ukimaliza safari yake kwenye kwapa lake, ambapo ndani ya sekunde mbili tayari kisu kikari cha kijana huyu, kilikuwa kimesha zama mala tano kwenye kwamba maungio ya kwapa lake la kushoto.
Mbwilo anahisi nguvu zinaanza kupungua mwilini, anazidi kulegea na kuegemea gari aina ya Toyota land cluizer, ambalo lilikuwa karibu yake, japo anazidi kukosa nguvu na kuanza kwenda chini taratibu, akiegemea gari lile.
Kwa macho yaliyoanza kupoteza nguvu, Mbwilo anamtazama Lisanga, ambae anasasa alikuwa amelala chini huku damu zikiwa zina mwagika shingoni mwake, Mbwilo anamtazama Nzala, ambae pia alikuwa amelala chini pasipo pumzi yoyote, Mbwilo anamtazama Malibuka, na ambae pia alikuwa hivyo hivyo.
Kwa macho ya mshangao na kukata tamaa, Mbwilo anamtazama kijana huyu, ambae bado alikuwa mbele yake, anatamani mfanya nyie chochote ambacho kinaweza kumtoa roho huyu bwana mdogo, lakini kiukweli Mbwilo hakuwa na uwezo ata wakukujikuna.
“naomba….. niku ….. nikufahamu,……. kabla sijafa, maana……. toka nizaliwe, sija……. sija ….. sijawai kukutana, na …..na …..na mtu kama wewe” alisema Mbwilo kwa sauti ya chini iliyotoka kwa tabu mdomoni mwake, huku akihema kwa shida, damu zikiendelea kutoka kwa wingi, katika majelaha ya kisu na risasi.
Kijana huyu mdogo, alie simama mbele ya Mbwilo, huku ameshikilia kisu mkonononi, kilichokuwa kina dondosha damu, anamtazama Mbwilo kwa sekunde kadhaa, ni kama vile anajiuliza, kama kuna umuhimu wa kumjibu, au aachane nae, wakati huo kwambali, vilianza kusikika ving’ora vya polisi, sambamba nangurumo za magari yaliyopo katika mwendo mkali, vikija upande huu.
Hance anachuchumaa kambele ya Mbwilo, “unataka kufahamu nini toka kwangu?” anauliza kijana huyu, ambae mimi na wewe tunamfahamu kwa jina la Hance Johnson, huku anamtazama Mbwilo, ambae ata macho yake yalishaanza kulembua.
“hivi…. hivi …… wewe ni nani?” aliuliza kwa tabu bwana Mbwilo, kijana alie aminiwa na Tino Nyondo, kuwa anaweza kutekeleza jukumu alilompatia, “naitwa Panya” alisema kijana Hance kwa sauti ya chini, yenye kunong’ona, kisha akainuka na kuanza kutembea kufwata usawa wa pale aliposimama Anastansia, wakati huo gurumo za magari sambamba ving’ora vya ashirio la polisi, vikianza kusikika kwa ukaribu zaidi.
“tuondoka haraka” alisema Hance, kwa sauti ya chini, mala tu baada ya kumfikia Anastansia, ambae bila kujitazama mala mbili, wala kujari uvaaji wake, nae anamfwata Hance kwa mwendo waharaka, huku mwanadada Aisha akiwasindikiza kwa macho ya mshangao na uoga.
“mbona mtu mweyewe….” anawaza Insp Aisha Amary, huku anawaona wawili awa wanatokomea kwenye vichaka vinavyo zunguka uwanja wa michezo ya wazi, na sekunde chache baadae yanaingia magari mawili iana ya land lover defender, mali ya jeshi la polisi, likiwa na askari kumi, kwamaana ya askari watano, kila gari, wote wakiwa na bunduki zao aina ya SMG, mikononi mwao.
Haraka sana wanazunguka eneo, lile kufanya ulinzi, huku wengine wakianza kukagua majeluhi, wakati huo huo Farida anatembea taratibu kuondoka eneo lile, bila kuonekana.
Upande mwingine, mwanaume mtu mzima, anakokota baskeri yake, kueleka upande wa shule ya msingi ya mazoezi, yani upande wa kusini, huku anaingiza mkono mfukoni mwake, na kuibuka kifaa flani kama redio ndogo.
Mwanaume mtu mzima anabofya kitufe flani kama switch ya ukutani ya kuwashia taa, nayo ina waka kitaa chelundu, nikama mwanaume mtu mzima ajamaliza, anazungusha kitufe flani kama cha kuongezea sauti, ambacho kilikuwa na namba kuanzia moja mpaka kumi tano.
Kile kitufe kinapo gota kwenye namba saba, ile taa nyekundu inabadilika na kuwa na mwanga wakijani, nae anaisogeza mdomoni, huku anabinya kitufe kingine, kilichoandikwa PTT, “hallow Chui toka Sungura, ujumbe toka kwangu over” anapo maliza kusema ivyo anaachia kile kitufe cha PTT, nakusikilizia kidogo.
Hakuna chochote kinacho sikika, mwanaume mtu mzima anasubiri kwa sekunde kama tano hivi, anaminya tena PTT, ikiwa na maa ya Pree To Talk, “hallow Mamba, ujumbe toka kwa Sungura over” mwanaume mtumzima alirudia maneno yale yale.
Lakini safari hii, ikasikika kelele zamawimbi ya redio toka upande wapili, “toka Mamba tuma ujumbe wako over” ilisikika sauti toka upande wapili wa redio, na mwanaume mtu mzima, ana bonyeza PTT, na kusogeza redio mdomoni, “toka kwangu kuja kwako, ni ujumbe kuhusu SA-26, sema kama unanisikia over” alisema mwanaume mtu mzima, kabla ajajibiwa na kuanza kutoa taarifa ya kile ambacho alikishuhudia. ****
Huku nako Insp Aisha Amary, akiwa bado anawaza kile alicho kiona dakika chache zilizopita, macho yake yameelekea kwa polisi wenzake ambao walikuwa wanawakagua watu waliolala chini, japo yeye akili na mawazo yake yalikuwa mbali sana.
“afande nini kimetokea, tumepigiwa simu na uongozi wa chuo, kuwa kuna majibizano ya risasi” alisema askari mmoja mwenye nyota moja begani mwake, ambae alikuwa anamsogelea Insp Aisha.
Insp Aisha nikama anagutuka toka kwenye wenge, anamtazama huyu A-Insp, kwa macho ya mshtuko na kumbu kumbu, “afande Ayoub Mzee” anasema Aisha, huku anaanza kukimbilia upande wa gari la ASP Ayoub Mzee. . . . ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

