TOBO LA PANYA (49)

SEHEMU YA AROBAINI NA NANE

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NANE: RPC anamtazama RCO wanapeana ishara ya kukubari, “umeongea point staff officer, ebu waandaeni watu, endapo hao wakina Nyondo wakimkosa, basi vijana wetu waingie kazini, wakamsake huyo mpuuzi kisha wakamkabidhi kwao wamfanye wanavyotaka” alisema RPC akimtazama RCO Zamoyoni. . . . . . . . ..Endelea…….

“sawa afande ngoja niazime simu hapa ndani, kisha nipige ofisini, kutoa ujumbe kwa Insp Aisha Amary, na ASP Ayoub Mzee, ni waambie sasa lathmi wanaluhusiwa kufwatilia jambo ilo, na juku lao ni kuhakikisha wanamkamata muuwaji wa Lukas” alisema RCO Zamoyoni Mpeta, kabla ajainuka na kuelekea mapokezi, kufanyia kazi mpango wao mpya, ambao waliamini unaweza kuleta amani hapa mjini Songea.****

Yaaap!, akiwa katika utulivu wa hali ya juu ndani ya gari, kama anapelekwa machijioni, mwanadada Anastansia anashuhudia gari likikatiza maeneo ya mtaa wa seed farm B, na sasa waliacha eneo lenye nyumba za kifahari, na kuanza vichaka vidogo dogo, na hatimae vichaka vilivyo fungana.

Ni eneo ambalo, leo ikiwa ni mala yake ya kwanza kulifikia, mida hii alikuwa analifikia kwa mala ya pili ndani ya siku moja, kwahakika halikuwa eneo geni kwake, ila lilikuwa linatisha, kwa kukumbuka kuwa, anaelekea kwenye kile kijumba cha udongo, anacho ishi kijana mpole.

Dakika tano baadae, gari lina simama pale pale kwenye kibanda cha udongo, kilichojengwa pembezoni mwa kichuguu, na miti mingi ya hasiri ya ile yenye matunda, eneo lililojaa giza totolooo, toka azaliwe mschana huyu, akuwai kuishi katika mazingira kama aya, ikiwa pale chuoni tu, ilimchukuwa miezi kadhaa kuziowea.

Anastansia anawaza jambo linalo mtia uoga, yani baada ya kutoka kuokolewa kwenye janga la wale watu, sasa anakuja kupambana na mijusi na panya, kwenye eneo ili lenye giza nene.

Gari lina simama, Hance anashuka toka kwenye gari, na kwenda kumfungulia mlango Anastansia, ambae anasita kushuka toka kwenye gari, “dada tumesha fika unaweza kushuka” alisema kijana Hance kwa sauti tulivu, akiwa ameushikilia mlango.

“lakini…. Lakini mwenyezio naogopa” alisema Anastansia, huku anashuku toka kwenye gari, akionyesha uoga wawazi kabisa, “bado ujaeleweka unaogopa kwenda ndani au unaogopa kubakia nje” alisema Hance kwa sauti tulivu, kama angetabasamu tungesema anatania, lakini hakuwa na dalili yoyote ya tabasamu.

Anastansia anashindwa kujibu, anamshuka toka kwenye gari, na kusimama nje pembeni ya gari, anamsubiri Hance, ambae anafunga mlango wa gari, anaanza kutembea, kueleka kuelekea kwenye malango wa banda la udongo, Anastansia anamfwata mpaka Hance anapoingia ndani ya banda la udongo kwa kusukuma mlango dhaifu wa banda ilo.

Anastansia anachungulia ndani ya banda la udondo, aoni kitu, kutokana na giza nene lililo tanda mle ndani, hakika pana ogofya, Anastansia anasita kuingia ndani ya banda, “hapana kaka, siwezi kuingia humu ndani mnatisha sana” alisema Anastansia, kwa sauti yenye uoga mwingi.

“sikulazimishi, ila tambua lazima uingie humu ndani, sababu ndiyo sehemu salama kwako” alisema kijana yule huku anapapasa pembeni kidogo, na kushika kibox cha kibiriti, ambacho anawasha kinjiti kimoja.

Macho ya Anastansia yanweza kupata nuru, na kuona mle ndani, ambamo mlikuwa na vitu vichache sana, meza moja chakavu, yenye sefuria tatu nyeusi kwa masizi, sahani chache za plastic na bati, vikombe na vibakuri, vyote vikiwa juu ya meza hivyo chakavu.

Pia palikuwa na kitanda kidogo cha kamba, juu yake pakiwa na godoro la sufi, ambalo alikuwa limetandikwa, kabisa, huku pembeni yake pakiwa na sturi ndogo, iliyo beba kibatari cha utambi, karibu kabisa na panzia lililo funika ukuta wakibanda iki, kwa kifupi hapakuwa na dalili ya kwamba kuna mtu aishi.

“mungu wangu, inamaana natakiwa nilale humu” anawaza Anastansia ambae anamwona kijana mpole, akipambisha moto wa kile kijibu cha kibiriti kwenye kibatari cha utambi, na mwanga wa una ongezeka ndani.

“sahamani kaka, naomba unipeke kwa mama mjini, siwezi kulala hapa, nitazimia kwa uoga” alisema Anastansia, huku anataka kugeuka na kutoka nje, lakini kabla ajafanya hivyo, anamwona kijana mpole anafunua panzia lililopo ukutani.

“ata mimi sijapenda uwe hapa, maana ni hatari kwangu, ila nimefanya hivi sababu ya usalama wako, kwa sasa auna sehemu salama zaidi ya hapa” alisema kijana mpole, yani Hance, huku anamaliza kufunia pandia, na kuacha wazi, kisha panaonekana sehemu kama kimkebe flani, kilicho pachikwa kwenye kuta ya tope.

“lakini uwezi kuniweka hapa, tena nikiwa hivi, unazani nisawa kaka” alisema Anastansia, kwa sauti ya kulala mika, huku akimtazama Hance, ambae sasa alikuwa anafunua kile kimkebe, na sasa kinaonekana kitu mfano wa kitupe cha kulipia umeme cha shirika la umeme la taifa.

“aito chukuwa muda mrefu, utaendelea na maisha yako, ukiwa salama kabisa” alisema Hance huku anabofya namba flani flani kwenye kile kimkebe, huku Anastansia anamtazama kijana huyu kwa kahadhari, ilikuona kitacho fwatia.

Hance anapomaliza anasogea pembeni kidogo, na kusukuma ukuta wa tope, nao funguka kwa ndani, na kubainisha kuwa nikama mlango, japo macho ya nance yaweza kuna kidogo, kutokana na mwanga wa kibatari, ambapo anaweza kuona ngazi kadhaa zikishuka shini.

Nancy anashindwa kuelewa zile ngazi zinaenda wapi, na kabla ajapatajibu sahihi, ghafla anashtuka Hance akiwa amesha zima kibatari, fumba na kufumbua alikuwa amesha shikwa mkono, “twende” ilikuwa ni sauti tulivu ya Hance.

“huko ni wapi?” anauliza Nancy kwa sauti yenye hofu, “kwenye tobo la Panya” alisema Hance, huku akimvuta Anastansia, ambae akutarajia tukio ilo, na kujikuta tayari amesha vutika na kumiguu yake inakanyaga sehemu laini tofauti na mwanzo.

“kaka unafanya nini..?” Nancy alipiga kelele ya hofu, na uoga, huku akivutika na kuingia ile sehemu ambayo aliambiwa kuwa kuni tobo la Panya, lililojaa giza. . . . . . . . ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!