
TOBO LA PANYA (50)

SEHEMU YA HAMSINI
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TISA: “kaka unafanya nini..?” Nancy alipiga kelele ya hofu, na uoga, huku akivutika na kuingia ile sehemu ambayo aliambiwa kuwa kuni tobo la Panya, lililojaa giza. . . . . . . . ..Endelea…….
ajamaliza kuuliza, ghafla wanga wataa ya umeme ukamulika mle ndani, Nancy anatazama vyema nakujikuta akiwa kwenye kolido fupi, la nyumba yenye kila dalili ya kuwa imejengwa kifahari, maana kuanzia kuta imara za tofauri za saruji, sakafu ya vigae vya chupa, yani tyles, juu siling boad ya kisasa, mbele yake mlango wa vioo, ulio jengwa kwa aluminium.
“inamshangaza Nancy, ambae anageuka kutazama mlango walio ingilia, anakutana na taswira ya ukuta, ambao akukuwa na na ata dalili ya nyufa yoyote, ambayo inaweza kufunguka baadae.
Anastansia anamtazama Hance kwa macho ya mshangao, anatamani amwulize kitu, lakini anasita, “karibu ndani, maana asubuhi uliishia nje” alisema Hance kwa namna ya utani, uku anausogelea mlango na kuufungua, nao wanaingukia kwenye ukumbi mpana, wenye sura tatu kwa mpigo.
Moja ilikuwa na makocho mawili ya kisasa, yaliyo izunguka meza ndogo ya gharama, huku pembeni kushoto, kukiwa na TV kubwa ya nchi 42, ambamba na seti ya redio yenye speeker kubwa, friji dogo, na kijimeza kidogo chenye simu ya mezani.
Anastansia anajikuta anatabasamu, baada kutazama uapnde wa kulia, wa iki chumba, ambako anaona meza kubwa, iliyoobeba jiko kubwa la umeme, lenye ovena, na vifaa mbali mbali kwaajili ya mapishi, vilivyowekwa katika mpangilio mzuri, yani visu sehemu yake, vijiko sehemu yake na vitu ngine vingi.
Pia nyuma ya meza hiyo ndani ya chumba iki ambacho licha ya kuto kuwa na dirisha ata moja, lakini lilikuwa na hewa safi, palikuwa na kabati ndogo ndogo, zilizo shikizwa ukutani, kwa juu, zikianzia mwanzo wa ukuta mpaka mwisho wa ukuta.
Makabati hayo pia yalikuwa maharumu kwaajili ya vyombo na vifaa mbali mbali kwaajili ya mapishi, bila kusahau friji kubwa mbili zilizokuwa pembeni kidogo ya meza ya jikoni.
Macho ya Anastansia, aya kuishia hapo, anatazama upande wa mbele ya kule anakotazama, yani nyuma ya kochi kubwa, ambako palikuwa na kitanda kikubwa cha futi nane kwa nane, kilicho tandikwa kwa mashuka mazuri, huku kitanda kikiwa kimezukwa na vikabati vidogo vidogo, nyuma ya kitanda.
Upande wakushoto, palikuwa na mlango wa kioo, ambao ata wewe usingeuliza kama ni mlango wawapi, maana jibu limesha patikana kuwa ni bafu na choo.
Hakika ilikuwa ni sehemu nzuri sana kwa Anastansia, ambae licha ya kuishi maisha ya kifahari yenye kila aina ya raha, na upendeleo, lakini akuwai kuishi kwenye chumba kama iki ambacho kina jitegemea kwa kila kitu, na kumfaha mtu kama yeye anae penda utulivu, hakika usingeweza kukumbuka kuwa, sehemu hii ni kati kati ya kichaka.
Anastansia anamwona kijana anasogelea kitanda, kisha anavuta dlow ndefu chini ya kitanda, na kutoa nguo mbili, yani truck suit ya chini, na tishert, kisha anaufwata mlango wa wa kioo, ambao ni unaonekana vyema kabisa, kuwa mlango huo wakuingilia bafuni.
Anastansia anaanamtazama kijana huyu alie chafuka damu, mpaka alipo ingia bafuni na kufunga mlango, kisha yeye akiwa amesimama, anatulia kwa sekunde kadhaa, akitafakari jambo.
Kwanza anajitazama jinsi alivyo vaa, kwamaana ukiachilia tauro na kitenge, akuwa amevaa nguo yoyote nyingine, siyo sidiria wala chupi, “nahatari mimi, hivi wale jamaa wangenichukuwa ingekuwaje?” anawaza Nancy, huku anajitazama jinsi alivyo vaa.
“mh!, ndani ya chumba kimoja na mwanaume mpaka asubuhi, hivi ataweza kuvumilia kweli” anajiwazia Nancy huku anatabasamu, “lakini hii ndiyo sehemu salama, hakuna mtu anaweza kujuwa kama kuna nyumba” anajisemea Nancy, huku anasogea kwenye kochi na kukalia.****
Dar es salaam mbezi, nyumbani kwa mzee Kingmwile, sebuleni bado familia nzima hipo pale, yani mke watoto na mzee kingumwile, wote walikuwa nakini kutazana fillamu ya Kiswahili yenye maudhui ya uchekeshaji, huku mud wote wakicheka na kufurahi.
Ilikuwa tofauti kwa mzee Kingumwile ambae alikuwa amekaa kwenye kochi dogo la mtu mmoja, pembeni ya meza dogo iliyo beba simu juu yake, mar kwa mara, alikuwa anatazama saa ya mkononi, huku akirudisha macho kwenye simu ya mezani, ni wazi alikuwa anaisubiri kwa hamu kubwa.
Naaaaam!, nikama tulivyo hisi, mara ghafla ukasika mlio wa kengere ya simu, iliyokluwepo jilani yake, nae akusubiri iite mara mbili, akadaka mkonga wa simu na kuupeleka sikioni, “mr Kingumwile, naongea hapa, nani mwenzangu” alisema mzee Kingumwile, mara baada ya kuweka mkonga sikioni.
“Farida hapa, nimesha kamilisha mpango, mlengwa amepelekwa sehemu salama, lakini Panya amedondosha wanne” ilisikika sauti ya kike toka upande wapili wasimu, “kazi nzuri, Farida, naamini sasa kila kitu kitakuwa safi, mpango mpya ni kumsafirisha Panya, aende sehemu salama zaidi” alisema mzee Kingumwile, kwa saya chini kidogo.
“ni kweli mzee, lakini kwasasa bado kuna changamoto kidogo, maana huyo binti ni mtoto wawaziri mkuu mastaafu wa #Mbogo_Land, bwana Antony, lazima juhudi za kumtafuta zitaongezeka” alisema mwanamke upande wapili wa simu.
“pili mkulugenzi ni kwamba, mpaka sasa polisi wanamfwatilia yule mwanamke, ili kumpata Panya, hivyo wataendelea kumfwatilia, endapo Anastansia ataendelea kutoweka” alisema Farida.
“ebu subiri kidogo, kwanza huyo Nyondo anauwezo gani, na kwanini achukuliwe kwa uzito wa hali ya juu?” aliuliza mzee Kingumwile, kwa sauti yenye kukeleka na mtu ambae anasababisha polisi wanaingia kazini, na kuhatarisha kufichuka kwa siri ya kijana wake.
“mzee nina habari chache za bwana Tino Nyondo, ambae ni ni mmliki wa kampuni ya usafirishaji, anaeusishwa na matukio mengi ya mauwaji, yanayo sababishwa na utetezi au visasi juu ya mdogowake, ambae akutaka guswe au ashambuliwe na mtu yoyote” alieza Farida, akimfanya mzee Kingumwile amsikilize kwa umakini.
“pia bwana Nyondo, anajiusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, anamiliki vijana hatarim, wenye uwezo wa kutumia silaha za moto, na wanao tekeleza majukumu ya mauwaji pale boss wao anapo toa amri …………… ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

