
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI : “pia bwana Nyondo, anajiusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya, anamiliki vijana hatarim, wenye uwezo wa kutumia silaha za moto, na wanao tekeleza majukumu ya mauwaji pale boss wao anapo toa amri …………… ..Endelea…….
“kwa sababu zisizojulikana, polisi awaja wai kumshikilia kwa mauwaji yoyote, wall kumshikilia mmoja wa vijana wake, ni kama vile wanamwogopa, ndio maana ata sasa polisi wanafika eneo la tukio, na kushambuliwa na vijana wa Nyondo, na hakika auto sikia hatua zozote zikichuliwa zidi ya Nyondo na vijana wake” alifafa nua Farida.
“huyo mshenzi, ni lazima aipate faida ya hayo anayofanya” alisema mzee Kingumwile, ambae akuishia hapo, “nivyema kama nitamjulisha Panya, ili afanya kinahotakiwa kufwanywa” alisema mzee Kingumwile kabla ya kukata simu na kuanza kupiga namba nyingine, kisha akaweka sikioni, na simu ikaanza kuita.**
Naaaaam! hospital ya mkoa pana utulivu wa kawaida, shughuri zinaendelea, taharuki iliyotokea lisaa limoja lililopita, ni kile kipigo cha mmoja kati ya majeluhi, waliolazwa hapa hospital, ni wale vijana wa Nyondo, yani wakina kubaga.
Lakini katika utulivu huo, mala ghafla yanaingia magari mawili ya polisi, yote yakiwa na polisi kadhaa wenye silaha, moja likiwa linavuja damu kama gari la bucha.
Wakati gari moja linapitiliza upande wa jumba la kuifadhia miili ya wafu, huku gari la mbele, linasimama mbele ya jengo la dhalula, japo askari waliokuwa nyuma, walishuka kwa haraka, lakini Insp Aisha Amary, alikuwa wakwanza kushuka, na kuzunguka upande wa nyuma, ambako aliweza kuwaona askari wanasaidiana kumshusha SP Ayoub Mzee, ambae bado alikuwa amepoteza fahamu.
Wauguzi wanatoka nje ya jengo ilo wakiwa na kitanda, wanambeba ASP Ayoub Mzee, na kumwingiza ndani ya jengo ilo, kisha matibabu yanaanza kwa mala moja, huku Insp Aisha akifwatilia kwa karibu matibabu hayo.***
Turudi seed farm, nyumbani kwa kijana Hance, ambapo sasa tuna mwona mwanadada Anastansia, akiwa amekaa sebuleni, huku kijana Hance anatoka bafuni akiwa amevalia nguo nadhafu za michezo, yani truck suit na tishert.
“kaka sahamani, naomba uniambie wewe ni nani” alisema Anastansia, huku anamtazama Hance kwamacho ya tahadhari, “sidhani kama itakuwa vyema ukinifahamu, sababu ukijuwa utanisumbua” alisema Hance kwa sauti tulivu, na wakati huo huo kengere ya simu inasikika mle ndani.
Anastansia anacheka kidogo, henye asira kidogo, “sikuwai kufikilia kama wewe ni mwongeaji hivyo, ebu niambie kama polisi au JW, MSA, TSA ARU, au nani sijuwi” anasema Anastansia, safari hii akionyesha kukasirika.
Hance anatazama simu, ambayo inaendelea kuita juu yameza, anamtazama Nancy, ambae anamtazama kwa macho ya hasira, kwamala ya pili Hance anatabasamu, kiasi cha kumfanya Nancy ashangae kidogo.
“nilizani ukitabasamu pekee, kumbe ukikasirika unapendeza zaidi, acha maswali ya ajabu, bila shaka toka asubihi ujaoga, nenda aoge ujiandalie chakula ule ulalale” alisema Hance, huku anasogea kwenye meza ndogo yenye simu, na kunyakuwa mkonga wa simu, kisha anaipeleka sikioni.
Wakati huo Anastansia, anajaribu kuvuta harufu ya kwapa lake, na kumbu kumbu zinamjia kuwa, toka alipoondoka chuo saa nne za asubuhi, akuoga tena mpaka mpaka mida hii.
Anastansia anajiuliza kuhusu nguo, atakayo badiri baada ya kuoga, natamaji kutazama baadhi ya nguo za kijana pengine anaweza kupata moja inayo mtosha, hivyo anamtazama Hance kwa lengo la kumwomba luksa, lakini tayari Hance alikuwa anaongea na simu, bahati nzuri nae alikuwa anamtazama Nancy.
Ata kabla ajaongea, tayari Hance alisha hisi nini Nancy anaitaji, akamwonyesha ishala ya kuendelea na ukaguzi wake, Anastansia anavuta dlow chini ya kitanda, ni ile ambayo Hance aliivuta mwanzo, ambako licha ya kukuta kuna jozi kadhaa ya nguo, lakini pia kulikuwa na bastora moja na mikebe mi nne ya risasi.
Anastansia anamtazama Hance, anamwona anaongea na simu, kuna taharifa chache za Tino Nyondo, nivyema kama utamfahamu rafiki yake ili ujuwe unacheza nae vipi” ilisikika sauti ya mwanaume mtu mzima, toka upande wa pili wa simu, “itakuwa vyema, maana ninampango wa kwenda kuongea nae, aache ujinga wake kabla sija wadondosha wengi zaidi” alisema Hance, ambae baadhi ya watu wanamwita Panya, wachache wanamwita SA-26.***
Sasa twende mateka uindini, nyumbani kwa bwana Augustino Nyondo, tayari waombolezaji walikuwa wameshaanza kuwasiri, pale msibani, wengi wao wakiwa ni wafanyakazi wa Tino Trans,
Tayari mke wa Tino Nyondo, alisha pata taarifa ya kifo cha shemeji yake, na sasa alikuwa ameshaanza safari, ya kuelekea Songea, wakati huo mji mzima ulikuwa umesimama, kwa mshtuko wa kifo cha Lukas, mdogo wa bwana Tino Nyondo, mtu hatari na katili kuliko ukatili wenyewe.
Bwana Tino Nyondo sasa, alikuwa amekaa kwenye kochi nje ya jumba lake la kifahari, akiwa pamoja na waombolezaji wengine, huku watu mbali mbali wakija kumpa pole, na kukwenda kukaa kwenye viti vyao.
Tino Nyondo ambae anaonekana kitazama saa yake ya mkononi kila baada ya dakika mbili au tatu, pia mara kwa mara, anaonekana akipeleka usoni, mkono wake wenye kitambaa cheupe, akipangusa machozi usoni mwake.
Tino Nyondo anawaza kwamachungu, kitu ambacho atamfanyie mtu alie muuwa mdogo wake, “nita mkata kichwa, kisha nikakitundike katikati ya mji, na mwili wake, niukate kate vipande niwatupie mbwa” anawaza Tino Nyondo, kwa machungu makubwa sana.
“hapana, huyu hatakiwi kufa haraka, huyu anatakiwa afe taratibu, huku anapata maumivu makali sana” alijisemea Nyondo, huku anaanza kuwaza kifo ambacho kitamfaa muuwaji wa mdogo wake. …………… ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU