
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI
HAMSINI NA MOJA: “hapana, huyu hatakiwi kufa haraka, huyu anatakiwa afe taratibu, huku anapata maumivu makali sana” alijisemea Nyondo, huku anaanza kuwaza kifo ambacho kitamfaa muuwaji wa mdogo wake. …………… ..Endelea…….
“huyu anatakiwa akatwe kiungo kimoja kimoja, akiwa mzima, yani kuanzia vidole vya miguu, na fwata vyamikono, na mng’oa jino moja moja, kisha nafwata macho na masikio, alafu namchuna ngozi akiwa mzima kabisaaaa” aliwaza Nyondo, ambae wakati mwingine alijiziuka na kuongea kwa sauti ya wazi.
Naaaaaam!, wakati Nyondo anaendelea kuwaza ayo, mara akamwona Kichondo anajia pale alipo, kisha anainama karibu na sikio lake, akionyesha wazi anaitaji kumweleza kitu, kwa sauti ya kumnong’oneza.
“boss, kuna taharifa mbaya kuhusu wakina mbiwlo” alisema Kichondo, kwa sauti ya kunong’ona, “kama awaja mpata huyu mwanamke, waambie wasije hapa mpaka wamempata huyu mwanamke, na awapeleke kwa huyo mjinga wamlete usiku huu” alisema Tino Nyondo, kwa sauti ya chini yenye hasira kali.
“lakini boss, wakina Mbwilo wameuwawa wote, amebakia kubaga pekee, amerudishwa hospital” alisema Kichondo, na kumfanya bwana Nyondo ajikute tayari amesha simama, na kuanza kunza kutembea kulufwata gari lake, huku vijana wake wakikimbizana kuingia kwenye magari, tayari kuelekea kule ambako boss wao, bwana Tino Nyondo, alikuwa anaitaji kwenda usiku ile.
Sekunde chache baadae tayari wote vijana walikuwa wamesha jaa kwenye magari, na safari ya kuelekea hospital, ilikuwa imeshaanza huku njiani vijana wakiandaa bunduki zao, maana wao hawakuwa wanajuwa kinacho endelea.****
Yaaaaaaaaap!, kule MAKIMAKULUGA MOTEL, ghorofa namba tatu, ikiwa ni muda mfupi tangu RCO aondoke kwenda kupiga simu, sasa tunawaona wanaume wawili watu wazima, yani RPC na staff officer wake, wakiendelea kupata kinywaji taratibu, huku macho yao yakiburudishwa na warembo wenye kuvalia chupi na sidiria pekee.
Wakati wawili awa wakiendelea kuburudika, mara tuna mwona SP Mpeta akirejea, na kwenda kukaa kwenye kiti chake, “kuna makubwa yametokea huko” anasema RCO Zamoyoni Mpeta, huku anachukuwa grass yake ya pombe na kuiweka mdomoni, anagugumua funda moja la kinywaji ndani ya grass kisha anaweka mezani.
“nini kimetokea Mpeta, ni kuhusu hii inshu ya Nyondo?” anauliza RPC, kwa sauti yenye mashaka, “nani mwingine, ni huyo huyo, alituma vijana kwenda kumteka mwanamke gani sijuwi, huko chuo cha matogoro, taarifa ni kwamba, vijana wake wanne wamechinjwa kama kuku, na ASP Ayoub Mzee, amejeluiwa na kupoteza fahamu, hivi sasa amekimbizwa hospital ya mkoa” alieleza Mpeta, na kuwafanya wazee awa wawili kuachama mdomo wazi kwa mshangao.
“wakina nani hao wanao fanya ili swala linazidi kuwa gumu, unazani Tino Nyondo atakubari kuliacha swala ili, kabla ajawakamata hao watu” alisema RPC kwa kulalama, akionyesha wazi kuwa, akupenda Nyondo azidi kuchokozwa.
“siyo wakinani afande, uliza ni nani?” alisema bwana Mpeta, huku anachukuwa tena grass yake ya pombe na kuinywa, akiwaacha wazee wawili, wakitoa macho kwa mshangao, “sijakuelewa Mpeta, unamaanisha ni mtu mmoja ama?” analiza staff officer, “ndiyo afande, ni kijana mmoja, tena ni yule ambae amemuuwa mdogo wake” alijibu Mpeta.
“aiwezekani, lazima utakuwa unatania Mpeta, ni nani huyo ambae anaweza kufanya matukio ya hatari kama aya, au ni mgeni hapa mkoani, na amfahamu Nyondo ninani” anasema RPC kwa sauti ya kuto kuamini.
“yani ni hivi, wakina SP Ayoub Mzee na Insp Aisha, walikuwa wamesha mpata binti ambaae alishuhudia mauwaji ya Lukas, wale vijana wakawavamia wakina Ayoub Mzee mzee na kumchukuwa huyo mschana, lakini kabla awajaondoka nae, nao wakashtuka mtu amewavamia, na kuanza kuwakata shingo kama kuku” alisema SP Mpeta.
“hapa inabidi tufanye jambo, vinginevyo hali ya mji itakuwa mbaya, muda siyo mrefu” alisema staff officer, na RPC akadakia, “haraka inabidi watumwe askari wakamchukue huyo mwanamke, atueleze huyo jamaa ni nani, ili tuweze kumkamata” alisema RPC, na kumfanya RCO Mpeta atabasamu kidogo.
“mkamchukue wapi sasa, huyo kijana ametoweka nae” alisema Mpeta, na hapo wazee hawa wakajikuta wanashusha pumzi ndefu ya mchoko, “upuuzi, huyu mtu ameleta mtafaruku mkubwa sana, na mjuwa Nyondo awezi kukaa kimya, atavamia raia wasio usika na huo na ujinga wake” alisema RPC, akionekana wazi kuwa amechanganywa na jambo lile.
“na tukisema tutoa askari, kwenda kumzuwia asifanye lolote, hapo tujuwe ndio patachafuka zaidi, na kuweza kupote askari, maana wanamatumizi mabaya ya silaha” alisema staff officer, nae akionekana kuvurugwa na jambo ili na kukosa la kufanya.
“mimi nina wazo moja, kama linaweza kusaidia” alisema RCO huku anawatazama kwa awamu wenzake, “lipi ilo bwana Mpeta?” aliuliza RPC, “afande ili swala inabidi tukae mguu nje mguu ndani, tuwaachie wenyewe vita vyao, maana inaonekana jamaa anawamudu, hii itasaidia kupunguza kelo, bila kupata lawama yoyote” alisema bwana Mpeta.
RPC na staff officer wanatazamana kidogo, kisha wanapeana ishala ya kutikisa vichwa vyao juu chini, wakionyesha kukubariana na wazo la RCO Mpeta, “ila inabidi tuweke askari wamfwatilie huyo kijana, inawezekana yeye akawa hatari zaidi yetu” alisema RPC.****
Sasa tumerudi seed farm B, nyumbani kwa kijana Hance yani SA-26, ambako tuna karibishwa na harufu mzuri ya vyakula, ambavyo vilikuwa vina pikwa na kijana huyu, ambae uarfu wake unafanana na Panya, aliekuwa amesimama mbele ya meza kubwa vya jikoni, anakamilisha mapishi yake.
Harufu hii inafika puani kwa mwanadada Anastansia, ambae anatoka bafuni, akiwa amevalia nguo za michezo, yani track suit na tishert nyepesi, zilizo mkaa vyema, huku ziki msanifu mwili wake, kwa namna zilivyo mbana, na kumfanya awe katika mwonekano tamanishi, kwa kila mwanaume lijari.
Anastansia anatabasamu kidogo, “ndio maana unaweza kukaa peke yako, unajuwa kupika vyakula vizuri” anasema Anastansia, ambae anatembea taratibu, akikatiza sehemu ya kulala na kueleka kwenye meza ya jiko.
“napenda kula vizuri, kila ninapo pata nafasi” anasema Hance, wakati huo anazima jiko, la umeme, akionyesha kuwa amesha maliza kupika, “sidhani kama utashindwa kujiandalia chakula, ukimaliza kula, kitanda kile pale, usijaribu kutoka, wala kugusa kitu chochote usicho kifahamu” alisema Hance, huku anasogea kwenye mlango wa kabati la nne, kati ya yale, yaliyopo pale jikoni.
Anafungua kabati na kuingiza mkono ndani yake, kisha mkono wake anautoa ukiwa umekumbatia sanduku dogo jeusi, lililotengenzwa kwa ngozi, huku likiwa na maandishi ya kirusia, juu yake. …………… ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU