TOBO LA PANYA (53)

SEHEMU YA HAMSINI NA TATU

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI: Anafungua kabati na kuingiza mkono ndani yake, kisha mkono wake anautoa ukiwa umekumbatia sanduku dogo jeusi, lililotengenzwa kwa ngozi, huku likiwa na maandishi ya kirusia, juu yake … ..Endelea…….

“wala siwezi kushindwa, ata ukitaka naweza kukuandalia na wewe pia” anasema Anastansia kwa sauti ya utani, huku anachukuwa sahani na kujiko cha kupakulia minofu ya samaki iliyo changanywa na ndizi.

Hance ajibu kitu, zaidi ana funua kile kisanduku, ambacho wengine uita briffcsace, hapo Anastansia kwa macho yake anaweza kujionea bastora mbili nzuri za nyeusi, pamoja na mitutu ya kuzuwia sauti miwili ikiwa pembeni, mikebe mi nne ya risasi, kwa mkadilio wa urefu wake, inauwezo wa kuifadhi risasi ishilini.

Nikama Hance alikuwa anahakikisha uwepo wa silaha hizo, anafunga na kunyakuwa lile bricace, kisha anasogea kwenye mzea ya sebuleni anaweka bricase na kueleka kilipo kitanda, yani sehemu ya kulala, ambapo anavuta drow ya mwisho kabisa, na kutoa ibuka na surua nyeusi ya jinsi, na tishert nyeusi, pamoja na jacket jeusi.

Anastansia alie kuwa ananyakuwa sahani yake, na kusogelea meza ya sebuleni, anamtazama kijana huyu, kwa macho ya mashaka, ambae anaonyeha dalili ya kubadiri nguo mbele yake.

Ni kweli anamwona amwona anavua nguo zake zote na kubakia kijibukta kidogo, akiacha mwili wake wakushangaza, ambao tofauti na vile anavyoonekana kikawaida, nakumfanya Anastansia atoe macho ya mshangao sambamba na msisi mko ulio utekenye mwili wake.

Maana ulikuwa tofauti na ule mwili amao ungemwona nao ila siku, akiwa akatika matembezi yake, yani ukiachilia mbali, kifua chake kilicho tuna kama mnyanyua vyuma, na mikono iliyo shupaa kiume, pia tumbo lake lili kuwa lime kakamaa na kugawika katika nyumba sita.

Hivyo vilikuwa ni kama sehemu tu ya mshangao wa mwanadada Nancy, shida ilikuja kwenye bukta, ambako aliweza kuona kitu kilicho tuna vyema mbele ya bukta ya kijana huyu, ikiwa ni utambulisho na ishala ya kile ambacho kijana huyu amejaliwa kuwa nacho, na kuitwa mwanaume.

Licha ya kuwa Anastansia alisha wai kuwa rafiki wa kiume wakati huo kidato cha pili, lakini akuwai kuona kitu kizito kama kile, labda kingefanana na kile ambacho aliwai kukiona mala kadhaa kwenye filamu au picha, japo yeye siyo shabiki wa video au vitu kama hivyo.

Dakika mbili mbele, tayari Hance alikuwa amesha vaa suruali na tishert, na sasa alikuwa anavaa viatu vya ngozi vyenye shingo ndefu, yani buti, “mbona kama unataka kuondoka” aliuliza Anastansia, kwa sauti tulivu yenye kujidekeza.

“yah! naitaji kwenda kukufanyia shoping ya vitu ambavyo hauna kwa sasa” alisema Hance huku amaliza kufunga viatiu vyake, na kuvaa jaket lake jeusi, “kama nini, kwani nimekuambia kunakitu naitaji” aliuliza Anastansia kwa mshangao kidogo.

“siitaji darubin kujuwa kama ujavaa chupi” aisema Hance huku anatembea kuelekea sebuleni, kwenye kona ya kushoto, ambako kuna friji ndogo, huku Anastansia akiachia tabasamu la aibu, maana nikweli hakuwa amevaa chupi wakati huo.

“kama chupi ni muhimu, basi usisahau mbili kwaajili yako, aipendezi uwe hivyo mbele yangu” alisema Anastansia, huku anamtazama Hance, ambae alikuwa amesha lifikia friji, na kulifungua, ndani kikiwa na chupa mbili za pombe kali na mbili za wine, huku kisahani kipana kikiwa kime beba visu nane, vyenye ukubwa na maumbo tofauti.

“kaeni chini wewe na macho yako, mjadiri kuhusu tabia ya kutazama vitu visivyo wausu” alisema Hance na kuhapo kinasikika kicheko kidogo, “angalau leo nimefahamu tabia yako, ya ukorofi” alisema Anastansia, huku anaendelea kula akimtazama Hance, ambae mpaka sasa hakujuwa jina.

“Anastansia anamwona kijana Hance anachukuwa kisu kimoja baada ya kingine na kukiweka kwenye mifuko ya koti lake ya ndani, akimalizia bastora zake mbili ambazo pia aliziweka kwenye mifuko hiyo hiyo, hakika ilishangaza sana, maana niwazi alikuwa anaenda sehemu ya hatari.

“samahani kaka, naomba nifahamu jina lako kabla ujaondoka” alisema Anastansia, kwa sauti ya kubembeleza, akimtazama Hance ambae alikuwa anajiandaa kuondoka.

Hance anasimama na kumtazama Anastansia kwa macho tulivu, anatumia sekunde kama tano hivi, “naitwa Panya, na hapa kwenye shimo la panya, usitake kujuwa mengi zaidi, ni hatari kwako” alisema Hance, kwa sauti tulivu.

“itakuwaje kama hauto rudi, nitawezaje kutoka humu?” anauliza Anastansia, “kunawatu wanafahamu kuwa hupo hapa, watakuja kukutoa” alisema Hance au Panya, “unamaanisha Farida, au kuna mwingine?” aliuliza Anastansia.

“anaweza kuwa, au asiwe, maana ata mimi mwenyewe sijuwi” alisema Hance kisha akaanza kutembea kuelekea kwenye mlango wa kutokea pale ukumbini, Anastansia akimsindikiza kwa macho.***

Saa tatu na robo usiku, mji wa Songea ulikuwa kimya kabisa, taarifa za kifo cha kijana machahali Lukas Nyondo, hofu ilitawara kwa kile ambacho kila mtu alibashiri kinaweza kutokea, baada ya kifo cha kijana huyo.

Mitaa ya kando kando ya mji, palikuwa kimya kabisa, kila mmoja alisha chukuwa tahadhari ya kujifungua ndani ya nyumba yake, kuofia kukutwa na dhahama ya vijana wa Tino Nyondo.

Ata kati kati ya mji, mitaa na barabara zilikuwa kimya kabisa, kasoro baadhi ya sehemu za starehe, ambako ungeona watu wametulia wanapata burudani ya vinywaji, chakula na music.

Maeno ya hospital kuu, ya mkoa wa Ruvuma, napo palikuwa kimya, magari ya polisi yalikuwa yana ondoka pale hospital, yakiwa na polisi wake, wenye silaha mikononi, huku wakimwacha Insp Aisha Amary, akiwa ndani ya ward namba mbili, upande wa VIP.

Ambako tunamkuta Insp huyu, akiwa amekaa kwenye kiti kidogo cha mbao, maarufu kama kistuli, huku anamtazama ASP Ayoub Mzee, aliekuwa amelala juu ya kitanda, sasa alikuwa amesha fumbua macho, “kwahiyo wameondoka na yule mwanamke?” anauliza RPC kwa sauti yenye mshangao.

“yah!, inasemekana, kuwa kuna mwanamke mwenzie, alikuwa anamtorosha, kwa bahati mbaya, akampeleka kwenye gari la wakina Insp Aisha” alieleza RCO Mpeta, ambae alikuwa ametoka kuongea na simu.

“ebu ngoja kwanza, hivi huyo kijana muuwaji ninani aswa?” anauliza RPC, ambae anaonekana kuingwa na mashaka makubwa, “kiukweli sidhani kama kuna anae fahamu, ila kwa uwezo alionao, anaweza kuwa ni polisi mwenzetu, au JW kama TSA, au ata MLA au MLSA, maana kijana ni hatari sana, unaambiwa amewakata shingo bila huruma yoyote” alisema RCO.

“mimi nazani afisa wa zamu, aende hospital akaongee na Insp Aisha, kupata habari zaidi, alafu ufanyike mpango yakinifu, wa kumpata huyo kijana asiendelee kumkorofisha Nyondo” alisema RPC, na hapo hapo RCO akainuka na kwenda tena kupata huduma ya mawasiliano, maana wakati huo, mkoa wa Ruvuma ulikuwa aujafikiwa na simu za mikononi.***

Yaaaaap!, eneo la hospital ya mkoa, ward namba mbili VIP, bado SP Ayoub Mzee anaonekana akiwa amelala juu ya kitanda, cha wagonjwa, huku Insp Aisha akiwa amekaa kwenye ile sturi pembeni yake, wanaongea ili na lile.

“ila nahisi kichwa bado kizito kidogo, unaweza kwenda kuniombea maji ya kunywa kidogo” alisema ASP Ayoub Mzee, kwa sauti ya kuomba, akimweleza Insp Aisha, “wala usiwe na shaka” alisema Insp Aisha Amary, huku anainuka na kwenda kufungua mlango, wakati huo wanasikia ngurumo za magari upande wanje.

Aisha anatembea kwa haraka kuufwata mlango, na kuufungua, kisha akatoka nje, na kuelekea upande wa mapokezi, ata baada ya kutembea mita kama ishilini hivi, kwenye kolido la jengo la hospital, Insp Aisha akawaona watu kadhaa wakitembea kwa haraka kuelekea upande wa jengo la kuifadhia miili ya wafu.

“mbona kama ni mzee Nyondo yule, au amekuja kuangalia watu wake” alijisemea Aisha, ambae akuangaika kuwa fwata, zaidi yeye aliendelea kutembea kuelekea upande wa mapokezi. …………… ..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata