TOBO LA PANYA (54)

SEHEMU YA HAMSINI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TATU: “mbona kama ni mzee Nyondo yule, au amekuja kuangalia watu wake” alijisemea Aisha, ambae akuangaika kuwa fwata, zaidi yeye aliendelea kutembea kuelekea upande wa mapokezi. …………… ..Endelea…….

Ni kwake watu wale walikuwa ni bwana Tino Nyondo na vijana wake wakina Kichondo, ambao waliekea moja kwa moja mpaka kwenye jengo la kuifadhia miili ya marehemu, ambako walifunguliwa mlango na kuonyeshwa wakina Mbwilo.

“inawezekanaje, huyo mtu ninani, na anawezaje kufanya aya mbele ya polisi, ana ubavu gani kuliko mimi” anauliza bwana Nyondo, kwa sauti ya juu, yenye jazba kali.

“mkuu mimi nazani tunaweza kuongea na polisi ambae alikuwepo eneo la tukio, nasikia yupo hapa hapa hospital” alisema Kichondo, “namtaka huyo polisi, sasa hivi” alisema Nyondo, kwa sauti yenye amri, huku anaanza kutembea kuelekea nje ya jengo, yanio kule walikotoka.

Neno moja la Nyondo, lilikuwa nikama amri ya mkuu flani wa majeshi, maana tayari vijana watatu, wakiongozana na Kichondo, walisha ondoka mbio mbio kuelekea upande wa ward za VIP.

Wakati huo mwanadada Insp Aisha alikuwa anatembea taratibu, chupa ya maji yenye jina la mkoa mmoja wa nyanda za juu kusini, kuelekea upande wa ward aliyo mwacha ASP Ayoub Mzee, huku kichwani mwake, akijiwa na picha ya tukio la kule matogoro chuoni, ambako aliweza kushuhudia vijana wanne wakichinjwa kama huku, huku mmoja akitandikwa risasi.

Lakini akiwa anaufikia mlango wa chumba na mbili, mala ghafla akawaona vijana watatu, wenye miili mikubwa ya kibabe, wakiwa wanamsogelea kwa mwendo wa haraka, ni vijana ambao hapo mwanzo aliwaona wakiwa na mzee Tino Nyondo.

Inamshtua kidogo Aisha, kichwani mwake kengere ya tahadhari inagonga, japo anakosa uhakika wa juu ya wasi wasi wake unatokana na nini, ata hivyo Insp Aisha anapata wazo la kuwai kuingia ndani.

Lakini basi, ata kabla ajaufikia mlango, wale jamaa walikuwa wamesha mfikia, “dada boss wetu anamaongezi na wewe” alisema mmoja wao, ambae mimi na wewe tunamfahamu kwa jina la Kichondo.

Insp Aisha anawaza kidogo, kama aende au asiende, kwamaana inaweza kuwa salama au hatari kwake, baada ya kuwaza kidogo, akapata jibu, “sidhani kama nitaweza, maana ninamhudumia mgonjwa……..” kabla Aisha ajamalizia kujibu, tayari mikono yenye nguvu ilisha mshika, na kumnyakuwa juu juu.

“jamani mnanipeleka wapi, afande Ayoub Mzee ni saidie wananikama hukuuuu” sauti kali ya kuomba msaada ya Insp Aisha, ilimfikia ASP Ayoub Mzee, ambae anajaribu kujiinua toka kitandani, lakini anahisi kichwa kizito, kwamaana maumivu ni kali, anarudi kitandani.

“afande wananiteka njoo unisaidie” sauti ya Aisha inaendelea kusikika, safari hii, ikiwa inaanza kusikika kwambali, ni wazi watekaji walikuwa wanaondoka na Insp Aisha.

ASP Aisha anaongeza juhudi, anajaribu tena kujiinua, safari hii anaacha kusikilizia maumivu ya kichwa anafanikiwa kujiinua, na kuanza kujikongoja kuufwata mlango, ambako kila hatua liyokuwa anaipiga, ndivyo alivyokuwa anaongeza mwendo.

ASP Ayoub Mzee anaufikia mlango na kufuufungua, pale nje amwoni Insp Aisha, na wala asikii tena sauti yake, zaidi ya kuona chupa ya maji ikiwa chini, ASP Ayoub Mzee anatazama upande wa mapokezi.

Kwamacho yake ASP Ayoub Mzee anawaona vijana watatu na mzee moja wa makamo, vijana wawili kati yao, wakiwa wamemnyakuwa Insp Aisha, wanatembea kuelekea upande wa nje.

Kijana mmoja akitembea nyuma yao, huku mzee wa makamo, ambae ni wazi kuwa ni mzee Nyondo, akiwa mbele, wote wanatokomea gizani upande wa nje, usawa wamaegesho ya magari.

Hapo bila kujari kuwa, akuwa amevaa viatu wala kandambili, ASP Ayoub Mzee, anatembea kwa haraka kuelekea upande wa mapokezi, akiongeza mwnedo bila kujari maumivu ya kichwa, mpaka anapokaribia mapokezi, ambako kuna watu wachache waliokuwa wanatazama upane wa nje, ambako wakina mzee Nyondo, waliekea na Insp Aisha.

“jamani nisaidieni” sauti ya Insp Aisha inasikika tena, sambamba na na milango ya gari inayofungwa, na wakati huo anasikia ngurumo za magari, yakiondoka pale kuelekea nje ya eneo la hospital.

Ata ASP Ayoub Mzee anapofika usawa mapokezi, sehemu ambayo aliweza kuona vyema magari mawili yakiondoka kutoka nje ya geti, la hospital, na kutokomea gizani, “yani awa watu awaogopi ata polisi” alisikika mtu mmoja akiuliza, “kama polisi wenyewe wanawachekea unazani nini kitafwata” alisikika mwingine, akiongea maneno ambayo yaliuchoma moyo wa ASP Ayoub Mzee.

“waliosema ukicheka na mbwa atakufwata msikitini, awakukosea, na hayo ndiyo matokeo yake” alisema mwingine, na hapo ASP mzee akaona sehemu hii akumfaha tena, zaidi ni kufanya jitiada za kumwokoa Insp Aisha, ambae kiukweli yeye binafsi asingeweza.

“wacha nikatoe taarifa kituoni” alisema ASP Ayoub Mzee, uku anatembea kuelekea kwenye lango la kutokea hapa hospital, “kaka …. we! kaka …….. bado hupo chini ya madoctor, ungepumzika kwanza” ilisika sauti ya muuguzi mmoja, lakini Ayoub Mzee akujari, aliendelea kutembea kutoka nje ya geti na kuelekea kule kwenye maegesho ya magari ya kukodi, maarufu kama taxi.****

Naaaaaaaam!, huko nyumbani lodge, hali ya utulivu imetawara, music laini, una waburudisha wateja, waliokuwa wamekaa kwenye meza zao, na maongezi katika hali ya utulivu, habari kubwa ikiwa ni kifo cha Lukas, yani mdogo wake Tino Nyondo.

Bwana Haule na familia yake, sasa wamesha maliza kukula, wanaendelea na vinywaji, wakati mama na baba wanakunywa wine, ya ~Mbogo_land coco, Eric alikuwa na chupa ya maji, yenye jina la mkoa flani wa kanda ya nyanda za juu kusini, huku eva na vestina, wakiwa wanakunywa juice maarufu za matunda, toka nchi jilani ya #Mbogo_Land.

Eric akiwa pembeni ya mzee Haule upande wa kulia, anajaribu kumnong’oneza baba yake jambo flani, “hivi wewe, akili zako zina waza kama tunavyo waza sisi wengine?” anauliza mzee Haule, kwa sauti ya wazi.

“mpaka hapo tupo tofauti, yani mimi naongea taratibu, wewe unaongea kwa sauti ya juu” analalamika Eric, na kuwafanya wote wacheke, kasoro mzee Haule mwenyewe, “kwahiyo unazani mimi ni mjinga, ni bebe lawama za kwamba nimekufundisha kunywa pomb….” anasema mzee Haule, lakini Eric anamuwai.

“haaaaaaaa! Baba, sasa ndio nini, siungekaa kimya tu, kwani lazima useme” anasema Eric, na hapo kila mmoja anatoa macho kwa mshangao, akimtazama Eric, “inamaana unataka kunywa wine, na bado unatakiwa kwenda shule?” anauliza mama Eric alie kaa upande wa kushoto wa mzee Haule.

“kama ni sumu nyie mngekuywa?” anauliza Eric, kwa sauti yachini yenye manung’uniko, “kwahuyo Eric sikuile ulikunywa pombe kimakosa, kumbe ujaluhusiwa?” anauliza Eva kwa mshangao, huku anamtazama Eric, ambae alikuwa amekaa kushoto kwake.

Ina mshangaza kila mmoja, mama Eric anacheka kidogo, mzee Haule anatikisa kichwa kukubari, “kumbe ulishaanza kunywa pombe, sasa ulikuwa unazuga nini, agiza ya kwako” anasema mzee Haule. …..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!