TOBO LA PANYA (55)

SEHEMU YA HAMSINI NA TANO

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NNE: Ina mshangaza kila mmoja, mama Eric anacheka kidogo, mzee Haule anatikisa kichwa kukubari, “kumbe ulishaanza kunywa pombe, sasa ulikuwa unazuga nini, agiza ya kwako” anasema mzee Haule. …..Endelea…….

“lakini baba unakumbuka kuna siku ile, ulimnunulia kaka chupa kama hii, wakati tunaenda kuangalia wanyama selous?” safari hii alikuwa Vestina, ambae aliamua kuwakumbusha jambo wajumbe awa.

“hoooooo!, nilisahau kama hupo hapa” alisema mzee Haule kwa sauti ya masikitoko na fadhaha, huku anashuka kichwa eneo la kipanda uso, kama ambavyo Eric pia alifanya.

“nilijuwa tu, yani Eric akiwa na baba yake, unaweza kusema ni mtu na rafiki yake, anakunywa pombe kama siyo mwanafunzi, alafu leo anajifanya eti hoooo, nitaonekana nakufundisha” alisema mama Eric kwa sauti ya kulalama.

“mama Eric ebu nipumzishe kidogo, kichwa changu kimerugwa, kuna mtu amesha uwa watu sita ndani ya muda mfupi” alisema mzee Haule, nakuwafanya wanafamilia wake wamtazame kwa mashangao.

“achana na hizo habari zako, unawatisha watoto” anasema mama Eric huku anatazama kushoto na kulia, mpaka anapomwona mhudumu wakike, akiwa anakatiza karibu yao, “we dada, tuletee wine chupa moja” alisema mama Eric, na wakati huo huo, mwanamwona mhudumu mwingine wakike akiwa amesimama pembeni yao, huku anasahani ndogo yenye kipande cha karatasi.

“bili kwako mheshimiwa” alisema yule mwanamke, huku anasogeza sahani mbele ya mzee Haule, inamshangaza kidogo mzee Haule, “nani kasema tumemaliza, au ndio utaratibu mpya?” anauliza mama Eric kwa sauti yenye jazba.

Lakini yule mhudumu ajibu chochote, anaondoka na kutokomea upande wa mapokezi, huku mzee Haule anafungua lile karatasi na kulitazama, huku macho yeke yakiwa yamejawa mashaka.

Kama alivyo tegemea na mashaka yake, mzee Haule anakutana na ujumbe mfupi, ulionadikwa kwa karimu ya wino, nae anaanza kuisoma kimya kimya, akijuwa kabisa ni ujumbe wa SA.

“kuna mwanamke anaitwa Farida, yupo chuo cha matogoro, ni SA-54, kuna uwezekano wakuwa anashirikiana na SA-26, alionekana jioni ya leo, akimtorosha mwanadada Anastansia Anthony…….” kabla mzee Haule ajamaliza kusoma, anashtuka karatasi limeondoka mkononi mwake.

Ebu lete hapa, mbona kama kuna mume wamtu anatongozwa hapa” alisema mama Eric, huku aliekwapua lile karatasi, nae analifunua na kuanza kulisoma, akiishia mstari wapili, nakutoa macho kwa mshangao.

“mh! na nyie jamani, ata amueleweki, yani mpo kila sehemu” anasema mama Eric huku anamrudishia mzee Haule lile karatasi, na bila kusema chochote mzee Haule anamalizia kusoma kimya kimya.

“Mahundi ametoa watu wawili, kwenda kumchukuwa mwanamke huyo, ili wamlete kwenye maojiano” hapo ndiyo mwisho wa ujumbe huo, mzee Haule anaikunja ile karatasi na kuiweka mfukoni, “kumekucha, mpaka juwa linachomoza tutakuwa tumesha sikia mengi” alisema Haule kwa sauti ya chini, na wakati huo huo, mhudumu anakuja akiwa amebeba kisaani chenye chupa ya wine na grass.****

Nusu saa baadae, mateka uhindini, mbele ya nyumba ya bwana Nyondo, nje ya uzio mkubwa wenye geti ambalo kwa sasa lilikuwa wazi, wanaonekana watu wengi na magari mengi ya waombelezaji.

Watu walikuwa wamekaa kwa vikundi, wakiongea na kujadiri baadhi ya mambo, huku wengine wenye hadhi na heshima zao, wakiacha magari yao nje na kupitiliza ndani ya uzio.

Wakati huo huo, linaingia BMW jeusi, na kwenda kusimama pembeni kidogo, ya eneo lile, mwisho mwa maegesho ya nje, yani kando kando ya magari, mengine, kisha anashuka kijana mmoja mdogo, mwenye sura ya upole, ambae alivalia suruali nyeusi ya jinsi, na jakect jeusi, chini akivalia buti za kaki.

Kijana yule mdogo, anaacha gari lina unguruma, anasimama nje ya gari lake kwa dakika kadhaa, huku akitazama watu na magari yaliyopo eneo lile, na masikio yake yakinasa maongezi yaliyokuwa yanaendelea, “yani mpaka Lukas azikwe, lazima patakuwa pamechimbika” moja ya maongezi yaliyo ongelewa pale.

Wakati huo huo yanaonekana magari mawili, yani range rover, na Toyota land cluizer, yakiingia kwa speed maali pale, eneo lina tawaliwa na utulivu mkubwa, kila mmoja anashangaa na kutazama magari yale kwa utulivu wa hali ya juu.

“hoya Nyondo huyooooo! ameingia, sijuwi nini kimetokea huko walikotoka” alisema mmoja kati ya watu waliokuwepo pale nje, huku wote pamoja na kijana mpole, wakishuhudia magari yale yana gawika.

Range rover linapunguza mwendo, na kuingia ndani kupitia geti kubwa la mbele, huku Toyota land cruizer, likipitiliza na kuelekea upande wa nyuma wa jengo ili kubwa lenye eneo la ekari moja.

“tayari wameshateka mtu, awa mafia” alimmoja kati ya mashuhuda, ambae maneno yake, ni kama yalimshtua na kumkumbusha jambo, kijana huyu mpole alie kuja na BMW.

Maana alianza kutembea taratibu, kuelekea upande ambao, Toyota land cruiser limeelekea, ambapo baada ya hatua kama nane hivi, aliweza kufikia mwisho wa uzio huu mpana, nakujionea Toyota land cruiser likiwa limesimama mwishoni kabisa mwa uzio, usawa wa geti kubwa kiasi, ambalo lilifunguliwa na gari likaingia ndani.

Hapo kijana wetu Hance au Panya kama alivyopenda kuitwa, akaongeza hatua kuelekea upande ule, huku akifungua zip ya jacket lake jeusi, ikionyesha wazi tayari muda wa matumizi ya vitu flani ndani ya koti lile la baridi.

Upande wapili nako, bwana Tino Nyondo, anashuka toka kwenye range rover, sambamba mlinzi wake, kijana mwenye mwili mkubwa, yani Kichondo, kisha anasalimia na watu wawili watatu waliokuja kumpa pole.

Baada ya kusalimia na watu wawili watatu, Tino Nyondo, anaingia ndani ya nyumba kubwa, akiongozana na Kichondo, wakifwata kolido, na kutokea upande wa nyuma, ambako waliekea mbele zaidi ya wakipita majengo mawili matatu, pamoja na mabanda ya mbwa, waliokuwa wanapiga kelele.

Wanalipita geti ambalo, lilikuwa lina watu wawili, waliokuwa wanalinda kwa umakini wa hali ya juu, na bunduki zao aina ya SMG, zikiwa madhubuti, mikoninoni mwao, sijuwi ni sababu walimwona boss wao, au ni kweli huo ndio utaratibu wao wakuhesimu jukumu lao.

Safari ya Tino Nyondo na Kichondo, inaishia mbele ya jengo moja kubwa, lenye mwonekano mfano wa ghara au ukumbi mdogo, Tino Nyondo anasukuma mlango na kuingia ndani, ambako anawaona vijana wake watatu, wakiwa na Insp Aisha alie shikiliwa vyema mikono yake, huku mdomo wake ukiwa umezibwa kwa kitambaa.

Aisha ambae ana uhakika wa kuwa, leo anaenda kushuhudia kile ambacho, amekuwa akihadithiwa kuwa kinawatokeaga wanawake wenzake, tena leo kinaenda kumtokea yeye mwenyewe.

Anamtazama mzee Nyondo, anatamani kumwomba amwachie, lakini awezi, sababu mdomo umezibwa na kitambaa, “Nyambi, naenda kule mbele, wacha kwasasa tukae na watu, ila naitaji majibu mawili, moja kwanini waliacha huyo binti anaondoka, pili waeleze huyo mpuuzi wao anaishi wapi?” alisema mzee Nyondo, kisha akaanza kutembea kutoka nje, akiongozana na Kichondo.

Aisha anatamani kumweleza jambo, lakini anashindwa kuongea, anashindwa kutoa kitambaa mdomoni, sababu ameshikwa mikono, na vijana wawili wenye nguvu, zaidi alisikia maagizo yakiendelea kutolewa, “nataka aongee kwa namna yoyote, mfanyeni aongee huyo mwanamke, nikija nakata shingo” alisema Nyondo, huku anatoka nje ya jengo.

Nyondo na Kichondo wanawapita walinzi walio simama kwa ukakamavu pale kwenye geti la uwani, ambalo lilikuwa limefungwa, huku mkononi mwao wakiwa na SMG zao, “hakikisheni upande huu, aji mtu yoyote, mpaka jukumu la huko ndani likamilike” anasema Nyondo huko anaendelea kutembea.

“ndiyo boss” wanajibu wote kwa pamoja, huku wamesimama kwa ukakamavu, wanamsindikiza kwa macho boss wao, na mlinzi wake, mpaka anapotokomea kwenye mabanda ya mbwa, kisha wanacheka kwa sauti ya chini, “boss bwana, nani anathubutu kuingia kwenye nyumba yak…”

Kudadadeki, kabla mmoja wao ajamaliza kuongea, wote alishtuka kisu chenye mcha kali kikiwa kime kita kifua ni kwake, na kutoboa kikizama ndani na kugotesha mpini wake kwenye mifupa ya mbavu, usawa wamoyo wake.

Mwenzie anageuka kutazama kilikotokea kisu, anamwona mtu akiwa hewani anakuja usawawake, atokea usawa waukuta, wa uzio, visu viwili katika mikono yake, aliyo itanua kama mbawa za mwewe, anaeshuka kuchukuwa windo lake. . …..Endelea……. kufwatilia hadithi hii, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!