TOBO LA PANYA (57)

SEHEMU YA HAMSINI NA SABA

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SITA: Kwamaana kama aliweza kufanya kosa la kumkabidhi Anastansia kwa polisi, bila yeye kujuwa, je ni wangapi walimwona, inamaana wale polisi awaja mtambua, na kama wamemtambua ato tumika kama ambavyo Anastansia anatumika kumtafuta SA-26, vipi kama mgongaji amemfwata yeye. TOBO LA Panya….ENDELEA……

“nani?” aliuliza Farida, na wote wakatega sikio kusiliza jibu, “bwana heee!, nani nani, mwanawake watupu mnajifungia hivyo mnafanya nini” ilikuwa sauti ya kike, ambayo wanaitambua mala moja, ni ya mwanamke mmoja mwanachuo mwenzao, ambae amechangamka kupita kiasi.

Wanatazamana, na kucheka kwa kuziba midomo, huku Farida akitikisa kichwa kwa masikitiko, “sema shida yako bwana, kwani ujuwi kama ni usiku saa” alisema kwa ukali Farida, “Joy unasubiriwa na mtu wako, nyuma ya bwalo, mpelekee akaigonge” ilisikika tena yule mwanamke, akifwatiwa na vishindo vyepesi, vikielekea upande wambele zaidi, kwenye vyumba vingine.

Nikama mtu mwenye shida, alie pata taarifa ya fedha, iliyo ingia kwake kimakosa, Joyce aliinuka haraka toka kitandani, akiwa amevalia gauni jepesi la kulalia, “dada Farida nakuja sasa hivi, ngoja kwanza nikamsikilize” alisema Joyce, huku ananyakuwa jacket na kulivaa.

Ata kabla Farida ajajibu chochote, tayari Joyce alisha ufikia mlango na kutoka nje, akimwacha Farida anatikisa kichwa kwa masikitiko, huku uso wake umechanua kwa tabasamu.

“niwakati wako binti, jiachia mtoto wakike” anajisemea Farida, ambae anaingiza mkono chini ya mto, na kuibuka na bastora, ambayo anaitazama kwa sekunde chache, ni kama anaikagua huku akitoa kimkebe cha risasi na kukirudishia.

kisha anairudisha chini ya mto, kisha anatoa kitabu kidogo, kilicho andikwa, #KIFO_CHA_MAREHEMU, kilichoandikwa na mwandishi wa hadithi alie bobea mwenye hasiri ya #Mbogo_Land, hapo tunamzungumzia mwandishi #mbogo_edgar.

Kisha anafunua jarada la kitabu iki, hapo unaweza kuona kisu kidogo, kimepachikwa kwenye pindo ya kurasa ya kwanza, iliyo ungana na jarada, anafunika huku akifungua kurasa ya tisa.

Lakini kabla ajaanza kusoma, aya ata moja katika kitabu iki, mala akaona mlango umesukumwa na wakaingia watu wawili wanaume, mmoja akiwa ni kijana na mwingine ni mwanaume mtu mzima, alie valie mavazi kama vile mkulima alie toka shambani mida hiyo.

Inamshtua Farida, ambae anajiuliza awa ni wakinani, na wanahatari kiasi gani kwake, hatua ya kwanza ya kujiokoa, Farida anaingiwa na uoga wa hali ya juu, anajikunyata pale kitandani, huku amekumbatia kitabu chake, “jamani naomba msinipige, nyie wakinani” anauliza Farida kwa sauti iliyo jaa uoga na mtetemo.

Yule mwanaume mtu mzima, anaonyesha ishala ya kuweka kidole cha kwanza kukatiza mdomo wake, “shiiiiiiiiiiiii, yetu yawe ya kwetu, aina aja ya kupiga kelele” alisema mwanaume mtu mzima, kwa sauti ya chini, huku yule kijana akifunga mlango.

“nyie siyo wanachuo, nyie ni wakinani na mnataka nini kwangu?” anauliza Farida kwa sauti ile ile ya uoga, huku amekumbatia kijitabu chake, ambacho alikuwa anajiandaa kukisoma.

“SA-54 unaitajika uongozane na sisi, unamaswali ya kujibu mbele ya ofisi ya upelelezi ya TSA mkoa wa Ruvuma” alisema mwanaume mtu mzima, na kumfanya Farida, atambue kilichopo mbele yake.

Ukweli ni kwamba, Farida alitakiwa kwenda kuhojiwa, na sababu lazima itakuwa ni kuhusishwa na SA-26, kwamaana hiyo basi iwe isiwe, lazima aseme ukweli kuhusu Panya, wauliza maswali watamfanya kitu chochote iliaseme ukweli, kwamaana endapo atakubari kuondoka, na awa jamaa akachague kufa katika mateso, au kusema uweli juu ya sehemu aliko SA-26.

Ila vinginevyo, angetakiwa kujitoa mikononi mwa watu hawa, “mbona siwaelewi, nyie mnaongea nini, SA ndio nini?, au mmekosea chumba” anauliza Farida kwa sauti ya uoga yenye wasi wasi mwingi.

Yule mwanaume kijana anamtazama mwanaume mtu mzima, nikama anauliza unauhakika, lakini mwanaume mtu mzima, anaachia kicheko cha dharau, “tusipoteze muda agent, huyo mwenzio tume mtoa mala moja, ili asielewe wewe ni nani, na akisha mkosa anae mfwata ata rudi sasa hivi, hivyo ni vyema kama tutaondoka haraka sehemu hii…”

Duh!, kaaazi kweli kweli, hakika mwanaume mtu mzima, akipewa nafasi ya kumalizia kuongea, maana haraka kama umeme, alishtuka Farida akifunua kitabu chake na kupeleka mkono mbele, haraka kama umeme….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata