TOBO LA PANYA (59)

SEHEMU YA HAMSINI NA TISA

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE: Mzee Haule anapokea mara moja, na kupitisha mdomoni, “inamaana yeye ndiyo anaona uchafu mdomoni mwako, kuliko mimi mkeo?” anauliza mama Eric kwa sauti iliyojaa wivu. ….ENDELEA

Mzee Haule anacheka kidogo, na kutumia ile tishu chini, karibu na mguu wake wa kulia, kisha anatulia kwa sekunde kadhaa, maongezi yakiendelea, ambapo ilichukuwa dakika nne tu, kusahau jambo lile.

Baada ya kuona mkewe na watoto wamesha sahau jambo lile, mzee Haule anainama chini na kuchukuwa kile kipande cha tishu, kisha anakikunjua kwa umakini, ambapo anakutana na maandishi yaliyoandikwa na karamu ya wino.

“SA-54, ame muuwa SA-101, na kumzimisha SA-240, kabla ya kutokomea kusiko julikana” ndivyo ulivyosema ujumbe huo ndani ya tishu, mzee Haule anaonyesha mshtuko wa kimya kimya.

“kumekucha, huyu mtu uwa atajwi kwenye sherehe, ukisikia jina lake, ujuwe kuna hatari kubwa imetokea au inaenda kutokea” alijisemea mzee Haule, huku anakunja ile tishu na kuimwagia wine kidogo, kabla ajaifinyanga na kutupa chini, huku anashusha pumzi nzito.

“mama Eric, na kuja sasa hivi, wacha nikatazame hapo ndani kama ndani kama naweza kupata simu nipige ofisini” alisema mzee Haule, huku anainuka toka kwenye kiti na kuanza kutembea kuelekea upande wandani ya jengo ilikubwa la ghorofa tatu, huku yule mhuhudumu wakike alie mletea tishu akifwata, kwamaana alijuwa kuna ujumbe wa kupeleka ofisini.****

Yaaaaap!, eneo la chuo cha matogoro, mtafaluku mkubwa umezuka, tafalani imetawara pale chuoni, uoga, wasi wasi na sitonfahamu kwa wanafunzi na walimu wao.

Mida hii ya saa nne za usiku, wanafunzi wote wapo nje ya mabweni yao, wamesimama kwa makundi, magari mawili ya polisi, yakiwa bado yana washa ile taa ya tahadhari juu ya paa yake, yalikuwa yamesimama, kando kando ya bweni la wakina Joyce.

pembeni ya magari yale, anaonekana Joyce akiwa amekaa kwenye kiti cha gari moja la polisi, mlango ukiwa wazi, huku pilisi kadhaa wakiwa wamemzunguka, wanachukuwa maelezo jinsi tukio lilivyokuwa.

Wakati huo polisi wengine, walikuwa wanamaliza kukagua chumba cha wakina Joyce na Farida, na kuanza kuutoa mwili wa mwanaume mtu mzima, na mwanaume kijana, alie bado kuwa amepoteza fahamu.

“unazani Farida yupo wapi na amepatwa nanini?” aliuliza polisi mmoja alie simama karibu na Joyce, “nilimwacha humu ndani wakati natoka nje” alijibu joyve ambae muda wote alikuwa anatetemeka.

“unazani yeye ndie alie wauwa awa watu?” aliuliza polisi mwingine, huku wote wakiandika baadhi ya mambo kwenye vijitabu vyao vya kumbu kumbu,

“sijuwi, maana yeye mwenyewe, sijakaa nae muda mrefu, amekuja hapa mwenzi wakwanza tulipofungua chuo” alijibu Joyce, ambae ata yeye aliwai kuhoji uharisia wa Farida, kwamba ni polisi au JW au TSA.

“Joyce unasema alikuja mwenzio na kukuambia kuwa, unaitwa kule bwalo, huyo mwenzio anaitwa nani?” aliuliza polisi mwingine, “anaitwa Eliza” alijibu Joyce, na hapo yule akari akaagiza eliza aitwe mala moja.

Dakika saba baadae eliza alifikishwa mbele ya polisi pale kwenye gari, huku analia na kutetemeka, “mimi sikujuwa kama yule mkaka ni muongo” alilalama Eliza, kwa sauti ya kuomba aonewehuruma, maana alisha juwa kuwa, tukio la mauwaji limetokea katika chumba cha kina Joyce, ikiwa dakikachache tu, baada ya kijana mmoja kumweleza kuwa akamwite Joyce, na amwambie wakutane bwaloni.

“ondoa wasi wasi Eliza, sisi tunatakla ujibu maswali yetu, kama utadanganya au kuficha jambo, bado ikibainika na wewe utaingia hatiani, moja kwa moja” alisema mmoja kati ya polisiwatatu waliokuwa, wana fanya mahojiano na wanafunzi awa wakike.

Eliza anaitikia kwa kichwa akikubariana na yule afande wa polisi, mwenye cheo cha A-Insp “aya elezea ilivyokuwa” alisema yule afisa wa polisi mwenye nyota moja begani mwake.

“mimi nilikuwa natokea chooni, nikamwona mwanaume amesimama paleee” alisema Eliza, huku anaonyesha upande wa njia ya kutokea bwaloni, kuja pale bwenini.

“nikamsogelea na kumwuliza shida yake, sababu wanaume hawaluhusiwi kuja kwenye mabweni ya wanawake, labda kuwe na jambo muhimu, tena linalohusu chuo kizima” anasimulia Eliza kwa sauti yenye uoga mwingi. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata