TOBO LA PANYA (61)

SEHEMU YA SITINI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI: Wote wakaanza kupandisha suruali zao, kwa haraka ili wamkabiri kijana huyu, lakini kiukweli aikuwa bahati yao, maana kwa kasi aliyonayo kijana huyu wa ajabu, awakuweza ata kufunga zip za suruali zao. ….ENDELEA

Tayari kisu kikali kilikuwa kimesha tembea kwenye shingo za vijana awa, ambao waliponzwa na na tamaa ya ngono, hakika huyu kijana ni mwenye roho ngumu, tofauti na sura yake, Insp Aisha najikuta anatabasamu kimoyo moyo.

Insp Aisha ambae anashindwa kuona aibu, zaidi ya kutamani kuokolewa haraka, kabla bwana Nyondo ajarudi mlendani, na kufanya mambo kuwa mengi, maana lazima mapambano makubwa yangetokea.

Insp Aisha Amary, akamwona yule kijana hatari, anatazama pembeni kwa heshima ya Insp Aisha, kisha anapeleka kisu kwenye kamba, iliyofungwa kwenye mkono wa Insp.****

Yaaaap!, mashariki mwa mji wa Songea, eneo la shule ya msingi mahenge, iliypo kando kando ya mtaa mkubwa wa mabatini, ikitenganishwa na mashamba ya maindi, ambayo sasa yalikuwa yamesha fikia hatua ya kiliwa kwa kuchomwa.

Mashamba hayo yanapelekea giza kuwa nene zaidi, na kutengeneza taswira ya kuogopesha, ukimya na utulivu wa eneo ili, lenye kijinjia kinachoenda kutokea kwenye bara bara kuu, iendayo mikoa ya kusini, linapendezeshwa na upweke mkubwa, maana hapakuwa na mienendo ya watu, zaidi ya mbwa koko na mipaka shume, ili yokuwa ina katiza katika njia ile.

Wakati eneo ili likuwa katika hali ya ukimya, upweke na ugopeshaji, tunamwona mwanadada Farida yani SA-54, akiwa anatembea kwa haraka akikatiza kwenye njia hiyo, mgongoni amebeba begi dogo, akielekea upande wa seed farm, kupitia stend ya Tunduru na njia panda ya Songea boys.

SA-54, anatumia dakika saba, mpaka kuikamata barabara kuu iendayo mikoa ya kusini, ambayo kwa wakati huo ilikuwa bado ya vumbi, huku iki tandwa ta miembe mirefu ya kihistoria, pande zote, yani kushoto na kulia.

Mwana dada Farida, anatembea kwa haraka na tahadhari ya hali ya juu, huku anatazama nyuma kila baada ya hatua kadhaa, mkono wake wa kulia ukiwa unapapasa bastora yake ndogo, aliyokuwa ameibana kwenye paja lake la kulia, kwa kutumia mnda mahalumu.

Mkono wakushoto, akiwa amebeba kitabu cha riwaya chenye jina KIFO CHA MAREHEMU, huku vidole viwili vya mkono huo wa kushoto, vikiwa vimebana kurasa kati ya kwanza na jarida la kitabu.

Mita hansini mbele, Farida anasimama mbele ya banda moja la huduma za simu, maarufu kama call box, anapekuwa mfuko mdogo wa begi lake na kuvhomoa card ya kupigia simu.

Anaichomeka kwenye call box na kubofya namba kadhaa, kwenye kisaani cha namba, na simu inaanza kuita mala moja, nae anatega sikio kusubiri simu ipokelewe.

Simu inaita kidogo, kisha ina pokelewa na mwanaume upande wapili, “habari za jioni, unaongea na bwana Kingumwi….” ilisikika sauti ya mwanaume mtu mzima, toka upande wapili wa simu, lakini Farida akutoa nafasi kwa mzee kingu kumaliza kujitambulisha.

“Seirra Alpha, figaz tano nne, ni wazi wamesha nishitukia, maana walituma watu kija kunichukuwa chuoni” alisema Farida kwa sauti ya chini yenye tadhari nyingi, huku anatazama huku na huku, kuona kama kunamtu anamfwatilia.

“mh!, kwahiyo wamekuchukuwa?” anauliza mwanaume mtu mzima toka upande wapili wa simu, akionyesha kushtushwa na taarifa ile, “nimewauwa wote wawili, na nimesha toroka toka chuoni, sasa nipo seed farm” alieleza Farida, ambae alionekana kuto kujiamini kwa uwepo wake maari pale.

“ok!, tangulia kwenye shimo la Panya, Panya atakukuta huko, maana ametoka mala moja ameenda kutekeleza jambo moja” alisema mzee Kingumwile, kabla farad ajakata simu, na kuenza tena kutembea kuelekea upande wa seed farm B.***

Naaaaaaam! magari manne mali ya jeshi la polisi, yanaonekana yakikatiza kwaspeed kwenye daraja la mto mateka, ASP Ayoub Mzee mzee na askari wake sita, wakiwa gari la nyuma kabisa, huku gari la mbele likiwa na RCO Mpeta akifwatiwa na staff officer na RPC akiwa katika gari la tatu, yote yakiwa land rover defender yakiendeshwa na madereva wapolisi.

Magari ya pandisha kwa speed kali, kuelekea upande wa uhindini, mtaa uliopo mwishoni kabisa mwakijiji hiki kikubwa cha mateka, kwenye makazi ya bwana Nyondo, ambae ndie mtu anae ogopwa zaidi hapa Songea na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.

Magari yale, moja kwa moja, yanaenda kusimama mbele ya uzio wa eneo, lenye makazi ya bwana Augustino Nyondo, ambapo panaonekana kuwa na watu wengi sana, sambamba na gari yaliyozagaa eneo lote la mbele.

Magari ya mbele yanasimama karibu na geti, kisha wanashuka maafisa wa jeshi la polisi, yani RPC staff officer na RCO, ambao wanaelekea ndani, huku gari la nyuma leyenye polisi wenye silaha, linanda upande wa kulia, mwishoni kabisa, mwa eneo ili la uzio wa bwana Nyondo.

Na madereva wa aya magari matatu, nao wanaenda kuegesha magari yao upande wa kushoto wa eneo ili, ambako ni upande wa barabarani, ndiko ambako limeegeshwa BMW jeusi.

Askari wa jeshi la polisi, wakiongozwa na ASP Ayoub Mzee mzee ambae kichwani mwake anawaza kile ambacho anaenda kufanyiwa Insp Aisha, wanatawanyika eneo lote la mbele.

Watu waliokuwepo pale nje, kwaajili ya maombelezo, wanawatazama polisi kwamacho yenye shahuku, wakitamani kujuwa lengo la ujio wao, huku wakingine wakijaribu kubashiri, juu ya ujio wa polisi awa.

“watakuwa wamekuja kuangalia usalama” alisema mmoja huku mwingine akibashiri karibu na ukweli, “Nyondo atakuwa amesha leta kasheshe huko” alisema yule mwingine.

Lakini huku ndani sasa, tuna waona viongozi watatu wa ngazi za juu, wa jeshi la polisi mkoa wa Ruvuma, wanatembea moja kwa moja, mpaka alipo kaa bwana Nyondo na wegeni wengine wenye hadhi ya heshima.

“pole na msiba jamani” wanasalimia makamanda wapolisi, ambao jioni ya leo walikuwa wamevalia mavazi nadhifu ya kiraia, “tumeshapoa” wanajibu wegeni wengine, lakini bwana Tino Nyondo, anakaa kimya, huku uso wake ukionyesha uzuni ya hali ya juu, nyuma mlinzi wake Nyondo, akiwa amesimama. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!