
TOBO LA PANYA (62)

SEHEMU YA SITINI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MOJA: “pole na msiba jamani” wanasalimia makamanda wapolisi, ambao jioni ya leo walikuwa wamevalia mavazi nadhifu ya kiraia, “tumeshapoa” wanajibu wegeni wengine, lakini bwana Tino Nyondo, anakaa kimya, huku uso wake ukionyesha uzuni ya hali ya juu, nyuma mlinzi wake Nyondo, akiwa amesimama. ….ENDELEA
“samahani bwana Nyondo, tunaomba tusogee pembeni, tuongee kidogo” alisema RPC, kwa sauti yenye nidhamu na tahadhima, “kuna nini bwana RPC, kama ni taarifa ya kupatikana kwa muuwaji wa mdogo wangu, unaweza kuniambia nikamwone” alisema Nyondo, ambae mpaka hapo alijuwa fika kuwa ujio wa makamanda awa, unausiana na Insp Aisha, ambae mpaka sasa alimini kuwa, yupo ndani anafanyishwa kazi za ovyo ovyo.
“hapana bwana Nyondo, ni kuhusu askari wa kike ambae vijana wako wamemshukuwa pale hospital” alisema RPC, kwa sauti ile ile yenye upole wa kuvutia, na kumfanya Nyondo amtazame RPC usoni, huku ametoa macho wa hasira.
“hivi bwana RPC, unaweza kuniacha nimalize msiba wa mdogo wangu, kisha muanze kunieleza izo shutumazenu, sizizo na kichwa wala miguu” aliongea Nyondo kwa sauti yenye hasira na ghadhab, huku anamkazia macho RPC.
“hakuna aja ya kuongea katika hali hiyo bwana Nyondo, ndio maana tumeomba tusogee pembeni” alisema RCO kwa sauti tulivu, yenye busara nyingi, lakini aikusaidia kitu, nikama walikuwa wameuwasha moto.
“kwahiyo RCO, mme ona mtafute kitu cha kunisingizia, ili kufuta lawama zenu, za kushindwa kumpata muuwaji wa mdogo wang…..” alisema Nyondo, ambae alisita ghafla kuongea, na kubakia akiwa ametoa macho ya mshangao, akitazama mita chache mbele yake.
RPC staff officer na RCO, naona wakatazama kama ilivyokuwa kwa Kichondo, na waombelezaji wengine, waliokuwa karibu na wakina Nyondo, wanafwatilia maongezi ya bwana Nyondo na wale makamanda wa polisi, nao wakatazama kule ambako Tino Nyondo, alikuwa anatazama.
Naaaaaaam!, wote kwa pamoja, wanawanaona vijana wawili, yani kiume na wakime, walioshikana mikono, wakitembea kwa mwendo wa kawaida, kulifwata geti la kutokea nje, la kutokea nje, kama vile ni waombolezaji wa kawaida, ata baadhi ya watu awakuelewa kwanini wakina Nyondo wanawatazama wale watu wawili.
Wakati RPC staff officer na RCO, wanatazamana kwa mshangao, Nyondo nae alimtazama Kichondo, kama vile anamwuliza imekuwaje, kisha kama wote wameambizana.
RCO, RPC na staff officer, wanaondoka kuelekea nje, kule waliko elekea wawili wale, huku Nyondo na Kichondo nao, wakielekea upande wa nyuma wa nyumba hii kubwa, sisi tuanze upande wa nje ya geti, ambako ndio karibu zaidi.
Na tuna waona wakina Mpeta wakiongozana kuelekea nje liliko geti, huku wakiwaona Insp Aisha Amary, alie shikwa mkono na yule kijana, wakitokomea nje ya geti, na kuelekea upande wa kulia, ambao ni upande wa kushoto ukiwa una itazama nyumba.
RPC na makamanda wenzake wanatoka nje ya geti, na kuibukia nje, ambako kwa haraka kutokana na mwanga afifu, wanawaona baadhi ya askari, wakiwa wamesimama pembezo mwaaneo lile, mingoni mwa raia wengine, waliokuja kuomboleza.
Ata wapotazama kulia zaidi, awawezi kuona kitu, kutokana na giza na uwepo wa watu wengine wengi, nao wanaanza kutembea kuelekea upende ule, huku macho yao yakianza kuzowea giza la pale nje.
ASP Ayoub Mzee, anawaona viongozi wake, anawafwata kwa haraka, “vipi afande kuna lolote, mbona imekuwa haraka sana” anauliza ASP Ayoub Mzee mala baada ya kuwafikia wakuu wake.
“Insp Aisha ameelekea wapi?” anauliza RPC, huku wanaendelea kutembea, macho kushoto na kulia, kutazama kama wanaweza kumwona mtu wanae mwitaji.
“Insp Aisha, siniliwaambia amechukuliwa na vijana wa Nyondo, nae akiwemo” alisema ASP Mzee, kwa sauti ya mshangao, lakini viongozi wake awakujibu kitu, zaidi ya kusimama na kutazama kushoto na kulia, kama vile wanamtafuta mtu flani.
Macho yao yanaishia kwenye gari moja dogo jeusi, ambalo lilikuwa lina unguruma, ila katika kumbu kumbu zao lile gari lilikuwa vile toka mwanzo, wakati wakuja, maana waliona taa za gari zikiwa zinawaka
“au Nyondo amekataa kuwa awajamchukuwa Insp Aisha?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, “Ayoub Mzee tufwate, wacha tukambane Nyondo, atueleze wamempeleka wapi Insp Aisha” alisema RPC, huku anaanza kutembea kueleka ndani, akujuwa kuwa mita chache mbele yao ndani BMW nyeusi, Insp Aisha alikuwa amekaa kwenye seat ya mbele ya abiria, yani kushoto kwa dereva, anawatazama wakuu wake wakazi. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

