TOBO LA PANYA (63)

SEHEMU YA SITINI NA TATU

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA MBILI: “au Nyondo amekataa kuwa awajamchukuwa Insp Aisha?” aliuliza ASP Ayoub Mzee, “Ayoub Mzee tufwate, wacha tukambane Nyondo, atueleze wamempeleka wapi Insp Aisha” alisema RPC, huku anaanza kutembea kueleka ndani, akujuwa kuwa mita chache mbele yao ndani BMW nyeusi, Insp Aisha alikuwa amekaa kwenye seat ya mbele ya abiria, yani kushoto kwa dereva, anawatazama wakuu wake wakazi. ….ENDELEA………

“kwanini unasema nisikuache kwa wenzako, mbona wapo wengi na anawasilaha?” aliuliza kijana Hance alie kuwa amekaa pembeni yake, kwenye seat ya dereva, “hapana kaka yangu, usiniache hapa, viongozi wetu wana mwogopa sana Nyondo, anaweza kuwatishia na wakaniacha mikononi mwao” alieleza Insp Aisha kwa sauti ya kuomboleza.

“uoni kuwa ni hatari kuwa karibu na mimi, maana watu wengi watataka uwaeleze mimi ni nani, na hakika uwezi kuwa na majibu” alisema Hance, kwa sauti yake tulivu, “siitaji kueleza wewe ni nani, nacho amini mimi umenisaidia naomba ukaniache kituoni, kwamaana awawezi kuja kunichukuwa pale” alisema Insp Aisha Amary, kwa sauti ile ile ya kuombeleza.

Hapo akamwona kijana mtulivu, mwenye sura ya unyonge, ana ingiza giza namba moja, na gari na kuachia cluitch taratibu, kuluhusu gari linaanza kuondoka taratibu, kuelekea upande wa mjini.***

Wakati huo huo kwenye barabara iendayo mikoa ya kusini, tuna yaona magari mawili ya jeshi la polisi, yakija kwa speed kali, huku yakitimua vumbi, kuja upande wa mjini.

Magari yale yanapofika maeno ya makao makuu ya polisi, yanagawanyika bila ishara yoyote, moja lina ingia kwenye lango la makao makuu ya jeshi la polisi, huku moja likinyoosha kuelekea hospital ya mkoa.

Sisi tunabakia na gari ambalo, linaingia makao makuu ya jeshi la polisi, na kwenda kusimama mbele ya jengo kuu la polisi, kisha wanashuka askari wa jeshi la polisi wenye silaha, huku wakiongozana na kijana mmoja alie valia nguo za kiraia, zilizo lowa damu.

“leo ataeleza yeye ninani na alifikaje pale kwenye bweni la wanawake, na kwanini walivamia pale” alisikika mmoja kati ya polisi, huku wakimsukuma raia huyu, alie vikwa pingu mikononi mwake, kuelekea ndani ya jengo kuu la polisi.***

Yaaaaap!!, sasa tumerudi tena nateja uhindini, hapo tunazunguzia nyumbani kwa bwana Tino Nyondo, yani pale msibani, ambako watu walikuwa wanaongezeka kila dakika.

Bado panaonekana kuwa katika sinto fahamu, ukizingatia raia licha ya kuona ujio wa polisi wenye silaha, ila pia wamewaona polisi hao wakizunguka eneo huku viongozi wajuu kabisa, wakiingia nakutoka nje ya jengo ili, kama vile kuna mtu wanamtafuta.

Hiyo weka pembeni, angalia hii, ya upande wa askari wa jeshi la polisi, ambao waliamini kuwa, Nyondo amemwamisha Insp Aisha kwamakusudi, ya kuwakwepa wao, wasije kupata ushaidi wa kumkamata.

Hivyo basi RPC, RCO, staff officer na sasa akiwa ameongezeka ASP Ayoub Mzee, wanaingia ndani kwenda kumweleza Nyondo aeleze anakopelekwa Insp Aisha, vinginevyo waondoke na mzee huyu, bila kujari kama amefiwa na mdogo wake.

Lakini hali hiyo ilikuwa afadhari kwao, kuliko ilivyokuwa kwa Nyondo na Kichondo, ambao kwa macho yao wamemwona Insp Aisha, akiwa ameongozana na kijana mmoja wa kawaida, mwenye mwonekano wa kinyonge, wakitoka nje.

Nyondo ambae kichwani mwake aimeifadhi swali ambalo yeye amejiuliza mala nyingi zaidi, na kupanga kwenda kuwauliza wakina Ndaskoi, kwanini wamemwachia Insp Aisha, na yule dogo ni nani.

Lakini basi, ile awanafika usawa wa geti la mlango wa nyuma, wanakutana na miili ya walinzi wawili, iliyolala chini, kwenye vimbwi vya damu, iliyotoka kwenye miili yao.

Hapo kengere ya tahadhari inagonga kichwani kwa Nyondo, anamtazama Kichondo kwa kwa macho ya mshangao, ambae pia alikuwa anamtazama kwa mshangao.

Kisha kama wameambizana, wanaanza kutembea kwa haraka, kuelekea kwenye mlango wa lile jengo kubwa kama ghara, ambapolicha ya kuwa mlango wake ulikuwa umefungwa, lakini hapa kusikika pilika yoyote ndani.

Wanasikuma mlango na kuingia ndani, na macho yao moja kwa moja yanatazama, miili ya watu watatu, iliyo lala sakafuni, huku eneo kubwa likiwa limejaa damu, kama sakafu ya machinjio.

“mh! hivi ni kweli ninayo yaona, au nipo usingizini” alisema Nyondo, ambae alimini kuwa mtu pekee ambae anaweza akamtikisa pale mkoani, ni jeshi la ulinzi peke yake, na sivinginevyo.

“awa jamaa wanataka nikachome moto kituo chao” alisema Nyondo, kwa sauti yenye ghadhab, “mkuu, mimi sidhani kama ni polisi, ndio waliofanya hivi, huyo atakuwa ni yule kijana, tunaemtafuta” alisema Kichondo, huku wanatoka nje ya ukumbi ule na kusimama nje.

Na hapo Nyondo akamtazama Kichondo, kama vile anasoma maandishi usoni mwake, ila ukweli ni kwamba, mzee Tino Nyondo, alikuwa anavuta kumbu kumbu ya maelezo ya kubaga, ambae nde pekee aliepona katika tukio la pili kule chuo cha ualimu.

“nikweli Kichondo, yule mjinga atukupaswa kumwacha atoke nje geti” alisema Nyondo, na wakati huo huo, wakasikia vishindo vya watu wanatembea kuja upande wa nyuma, nao wakatazama upande ule.

Sekunde chache mbele, wanaibuka watu wanne, ambao ni makamanda wa jeshi la polisi, wakiongozwa na RPC mwenye, “he!, wame kutwa na nini awa?” anauliza RPC, kwa sauti ya mshtuko na mshangao, huku wote wanasimama ghafla wakiishangaa miili ya watu wawili walio lala kwenye damu.

“sidhani kama umemaliza kushangaa bwana RPC, njoo ujionee kazi ya mtu ambae mnajifanya hamumjuwi, wakati anashirikiana na polisi, kuja kuuwa vijana wangu” alisema Nyondo kwa sauti yenye machungu na hasira. ….ENDELEA KUFWATILIA HADITHI HII YA TOBO LA Panya HAPA HAPA

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!